Tulonge

Pale mapacha walipomchanganya Diamond na kushindwa kung'amua yupi ni yupi (video)

blind date-2

Umeshawahi kujikuta umekutana na msichana mrembo au mvulana mtanashati, halafu siku ya pili ukakutana na pacha wake wanaofanana hadi ukucha na ukaendeleza maongezi mlipoishia jana bila kugundua si yule wa jana? Basi ndicho kilichomtokea Diamond Platnumz.

 

Coke Studio walimuandalia Platnumz ‘blind date’ ya mtoto wa kike mrembo, ila bila yeye kujua kuwa wako wawili mapacha wanaofanana (identical twins) na kumchezea mchezo. Baada ya kukutana na msichana wa kwanza anayeitwa Rose, walizungumza kwa muda mfupi kisha mtoto huyo wa Kikenya akaomba kwenda washroom. Huko alikuwa anasubiri pacha mwenzie aitwaye Janet ambaye walibadilishana, aliyerudi kwa Diamond hakuwa yule wa mwanzo.

 

Ila mwisho wa mchezo meneja wa Diamond alijifanya kumuita pembeni kumuelekeza jambo, ndipo hapo walipojitokeza mapacha wote wawili na kuketi pale pale alipokuwa Diamond, aliporudi akapigwa na butwaa asijue ni yupi aliyeanza kuongea naye maana hata nguo walizovaa zinafanana.

Tazama video ufahamu ‘blind date’ iliishaje

Via: bongo5.com

Views: 844

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on December 21, 2013 at 16:53

Ngoja niwasindikize kwa kicheko kidogo--ha ha ha ha!

PamoJah sana!

Comment by Mama Malaika on December 21, 2013 at 2:15
Ha haa haa haaaa.... CHA unaniua kwa kucheka. Ha haa haa haa haaa.....
Comment by Dixon Kaishozi on December 18, 2013 at 19:43
Hahahahaaa.....kaka CHA.. nimecheka mpaka basi.. .. thisi fudi izi tuumachi pilipili... hahahaaaa ..
Comment by CHA the Optimist on December 18, 2013 at 18:36

Kweli Dixon, hata mimi kila siku lazima nimeze angalau misamiati miwili ya lugha ya Denzil na Malaika. Sasa hawa wanaoitwa waigizaji na waimbaji wa Tanzania,hawaangalii mbele, wana maono mafupi sana--hawana maono ya mbali. Wanafikiria kuuza movie zao Sumbawanga, Shinyanga, na Karatu. Hawafikirii siku moja kuuza movie zao Texas, California- (USA), hawafikirii kuuza kazi zao Kingston--(Jamaica), hawafikirii kuuza kazi zao London na kwingineko duniani.

Comment by CHA the Optimist on December 18, 2013 at 18:27

Ha ha ha ha ha hah!

Sijabahatika kuisikia hiyo "who can i love you" natumia desktop now ambayo haina speaker.

Ila sishangai sana--ndivyo Wabongo walivyo, wanapenda sana kuongea lugha ya Denzil na Malaika, lakini hawataki kujifunza, hawataki kujisomea vijitabu, hawana ile tunaita udadisi--au --kwa lugha ya Denzil na Malaika "curiosity".

Kuna mcheza sinema mmoja kwa sasa ni marehemu anaitwa KANUMBA katika scene moja ya sinema yake hata sijui inaitwaje ile sinema, anasikika akisema hivi na ninanukuu "this food is too much pilipili". Basi huwa nikisikia vile huwa sina mbavu.

Si hao tu, ukitaka kuona ujinga wa ndugu zetu, tazama hizi movie za BONGO, yale maandishi yanayoonekana pale chini--sijui mnaitaje wenyewe, Kiingereza kinachotumika pale, unaweza kutapika. Sasa hapa kinachoonekana ni kwamba, team nzima inayohusika na uandaaji wa movie hizo ni mambumbumbu--na inaonesha ni watu wasiooshaurika.

Bado sana......

Comment by Dixon Kaishozi on December 17, 2013 at 9:24

Hehehee.. Yani bado sielewi.. Sijui ni tangazo ama nini @ Chaoga!!! Na kama ulivyosema.. yupo kwenye ardhi ya Africa Mashariki.. Hao mapacha wanaongea kiswahili.. yani ni mapicha picha tu... Ulimbukeni mbaya sana... hahahaaaaa

Comment by chaoga on December 16, 2013 at 14:27

NI KWELI USEMAYO DIXON NA ISITOSHE YUKO KWENYE ARDHI YA AFRIKA MASHARIKI KULIKUWA HAKUNA HAJA YA KUTUMIA KIINGEREZA, MBONA WAKATI AKIONGEA KISWAHILI SUBTITLE ILIKUWA IKITAFSIRI KWA KIINGEREZA? sasa hawa cokestudio wanatengeneza tangazo la kuonyeshwa ulaya au...!!?

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 13:08
Dismas... rafiki yako Tawonga Dingani ana pacha wake na wako identical, akija Kulwa utasema ni Tawonga (ambaye ni Doto), huwa wanawasumbua sana vijana. Ha haa haa haaaaa.........
Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 12:57
Ha haa haa haaa... Dixon! Mambo ya Bongo Flava,
Comment by Dixon Kaishozi on December 16, 2013 at 11:35

hahahaa.. Siyo umbea.. unajua lugha ni kujifunza... kunashida gani kurudi darasani ukajifunza lungha ? huku ni kujizalilisha.. basi ongea kikwenu inaleta maana sana kuliko kuchapia.. toka clip ya kwanza hicho kingereza we acha tu.. mimi nipo mwenyewe kwenye computer yangu lakini naona AIBU kuangalia.. je kwenye umati ? 

Tukumbuke Raisi wa china alipokuja.. alitoa hotuba kwa kichina...  kwani alishindwa kuongea kingereza ? 

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*