Tulonge

Pande za China: Mtoto aokolewa maisha yake,almanusura aanguke kutoka ghorofa ya 4 !!.

Sio siku nyingi,ni siku tatu tu zimepita tangu tusome habari hapa tulonge iliyomhusu mtoto kuponea chupuchupu kuliwa na simba katika Zoo moja inayokwenda kama ifuatavyo:Bahari Zoo.Ni zoo inayopatika katika jiji  nene la Dar -es- Salaam,maeneo ya Tegeta.

Habari hiyo ilikuwa inatia hofu kubwa kwa moyo ukizingatia hatari yenyewe "Simba", na aliyekabiliana na hatari hiyo ni "Mtoto" !.
Hilo liliwastua sana watu wengi waliokuwepo mahala hapo,lakini kwa bahati nzuri mtoto huyo alifanikiwa kuiona nyota ya bahati, baada ya kuokolewa kutoka mikoni mwa simba mwenye njaa na hasira !.


Tukiwa bado tunaendelea kupoteza poteza hofu hiyo iliyoambatana na hatari bin danger,ili ikiwezekana tusahau kabisa tukio hilo,tunakumbana na hofu nyingine katika tukio lingine linaloshabihiana na tukio hilo la Bahari Zoo !,mara hii tukio hili si tena pande za Tanzania,bali linatokea kule  pande za China.Kwa ufupi tukio hilo lilileta hofu kwa wengi ,hofu ambayo imepita kiwango cha hofu ,na kuingia moja kwa moja katika kile kiwango kinachojulikana kwa jina: Mstuko wa moyo!.

Enewei,tukio lenyewe lilikuwa kama ifuatavyo:

Mtu mmoja kusini mwa China,aliyaingiza maisha yake katika hatari kwa sekunde kadhaa ili kujaribu kuokoa maisha ya mtoto asianguke kutoka Ghorafa ya nne.Mtoto huyo shingo yake ilikuwa imekwama katika kitu kama vyuma hivi vilivyokuwa juu kabisa katika ghofa ya nne,kiasi kwamba hiyo shingo ingechoropoka kwenye vyuma hivyo kabla ya man yule kufika pale kumuokoa,basi bila shaka mtoto huyo angelisalimiana na ardhi kwa salamu moja babu kubwa!.

Lakini Mwenyeezi Mungu Mbora wa wenye kuokoa, kajaalia Mwanaume huyo shujaa akaweza kumuokoa mtoto na hatari hiyo iliyotikisa na kutetemesha mioyo ya waliokuwa wakitizama tukio hilo!,maana wengi wao walikuwa washa kata tamaa kwamba sasa mtoto wamempoteza pamoja na man huyo shujaa, maana kwa jinsi man alivyokuwa amejibanza ukutani juu kwa juu katika ghorofa ya nne,ilikuwa ni hatari sana kwa maisha yake.Wataalamu wanakwambia: Katika hali kama ile,kupoteza maisha yako ni asilimia 99 na nusu !!.

Lakini kauli hiyo ya wataalamu inapinduliwa na kuzidiwa na nguvu na kauli ya Mwenyeezi Mungu Mola wa viumbe kwamba yeye ndiye "Mwenye Nguvu" kuliko wenye nguvu,ndiye "Mwenye Huruma" kuliko wenye huruma,ndiye "Mpole" kuliko wapole,ndiye "Mwokozi"kuliko wenye kuokoa,bali wote wenye kuokoa humtegemea yeye Mwokozi.Na uokozi wake Mola ni mpana,hauna kikomo,hauna muda,na wala hauna mipaka,hata kama zimebaki sekunde mbili roho kuchomoka,Mwenyeezi aweza kumuokoa mja wake!.

Unaweza kukandamiza link ifuatayo ili kutizama video ya tukio hilo!.

http://en-maktoob.news.yahoo.com/child-rescued-from-deadly-fall-in-...

 

Na Chalii_a.k.a_ILYA.

Views: 991

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on June 12, 2012 at 21:11

Aisee mtoto mtundu sana huyu, umakini unahitajika juu yake

Comment by ILYA on June 12, 2012 at 21:03

Mtoto huyu akiwa mkubwa,akawa akicheki hiyo movie yake ya kunasa sehemu hiyo,bila shaka siku zote za maisha yake atakuwa ni Mtu wa kumshukuru Mola bali atampenda sana Mola Mwema!

Comment by Mama Malaika on June 12, 2012 at 19:48

Duh! Mungu ni waajabu... mtoto akiwa mtundu hasikii hata umfanyeje.

Comment by manka on June 12, 2012 at 17:13

duh kweli hapa Mungu tu ashukuriwe.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*