Tulonge

Polisi alivyochakazwa kwa Bomu lililotegwa na kundi la Boko Haram

This is really heart breaking, this was the moment an anti-bomb squad member Sergeant


Views: 489

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on February 18, 2012 at 13:26

Kaka kweli kabisa Africa mimi nashindwa kuelewa nani kairoga!!,halafu kaka umesahau kule mali nako hakujatulia,kuna kikundi cha kigaidi kinaitwa MNLA,kundi hili ni la waasi ambao wana bifu na serikali ya Bamako_Mali,wanaua sana raia jamaa hawa na kukalia kwa mabavu baadhi ya maeneo nchi Mali,wanafanya mashambulizi ya kigolila katika miji na kambi za kijeshi nchini Mali.Mwaka jana mamia ya wamali wamekufa sana na wengine wengi kuyahama makazi yao kwa sababu ya Jamaa hawa waasi wa Serikali.Wanaombw akuacha silaha chini na kuingia mazungumzo na serikali yao lakini jamaa wabishi kama sabuni.

Comment by jemadari mimi on February 17, 2012 at 20:32

jamani leo kila kukicha afrika ni vilio tu,iko wapi afrika ya wazee wetu akina nkwame nkuruma ,patric lumuma,jomo kenyatta,samora machell,walter sisulu,nelson mandela,abeid karume na julius nyerere,hawa waliwapenda watu wao na kuzipenda nchi zao,iweje leo sisi kila sehemu ni vikundi vya mauaji tu mara boko- haram kule somalia al-shababir na uganda naye joseph kony na URA ana sumbua raia,congo drc watu awalali kwa kuogopa vita na sudan nako wamegawana nchi na libya gaddafi wamesham.Nani ametuloga sisi?

Comment by ILYA on February 17, 2012 at 16:00

MTAZAMO WANGU KUHUSU BOKO HARAM.

Boko Haram hawaui kwa sababu za udini,yaani ni watu wametengenezwa pale Nigeria ili kuhatarisha usalama wa nchi ili mataifa fulani fulani yapate kudai kutuma majeshi yao ili kulinda amani,ili yaweze kuvamia visima vya mafuta na kujichukulia chao mapema.Nchi zenye utajiri wa mafuta lazima vikundi kama hivyo vianzishwe na wajanja wenye fikra za kukalia kwa mabavu mataifa mengine ili waweze kutuma vikosi vyao vya kijeshi kuja kuthibiti mafuta.Tumeona Libya kumetokea nini na sasa kuna majeshi ya kigeni elfu 13 yametumwa kama mnakumbukumbu.Na sasa Nigeria inaelekea huko.

Hivyo Boko Haram imeanzishwa kwa ajili ya kufanya vitendo kama hivyo ili mataifa yanayodai usuper power yapate kisingizio cha kwenda pale kulinda amani,nyie mtasikia tu hivi punde majeshi yanatumwa Nigeria.

Boko harama hawana dini maana wangelikuwa wanapigania dini wasingelikuwa wanaua watu wote bila kujali dini zao,na hata kama ni udini hatujasikia wakiristo wa Nigeria wakiwafanya fujo za kidini na Waislaam sasa kwanini waanzishe vita vya udini??

Kama ni udini unawatuma wafanye hivyo basi sidhani kama wangelikuwa wanaua hata waislaam wenzao maana hawa watu hawachagui katika kuua,wanauma makanisani na misikitini,wananyonga watu hata wakikutana nao huko sokoni na kuwatia mikononi basi ni halali yao,sasa wanaingia katika taasisi ya uslama ya nchi na kuua askari usalama na walinda amani wa taifa,je huko nako kwenye jeshi la nchi la kulinda amani kuna udini gani?.

Comment by jemadari mimi on February 17, 2012 at 11:50

Hivi hawa boko-haram wapo kwa maslahi ya nani kweli,maana wamekuwa wakiua ndugu zao,watoto wao na hata kusababishia watu kupata ulemavu wa viungo.Hii inatuonyesha kuwa mwanadamu ana roho mbaya kuliko hata simba,hivi imefikia mahala tunauana ovyo kwa sababu za kijinga tu eti udini ama kwasababu ya mafuta,hii yote ni kwasababu ya kutaka mali kwa kutumia nguvu zisizostahili.

Comment by Alfan Mlali on February 16, 2012 at 19:17

Hahahahahah...Eti kama Nwanko Kanu asingekua Mnigeria...hahahah

Comment by Bonielly on February 16, 2012 at 14:19

hao boko haram siwapendi hata kuwasikia, sio watu kabisa ni wanyama, hawana utu ni binadamu gani,

Comment by Tulonge on February 16, 2012 at 8:10

Naona jamaa wameitoa video, ni noma.Mngeona polisi wa watu alivyo chakazwa. Naamini mkuu Ilya aliiona.

Comment by ILYA on February 15, 2012 at 22:40

Oo my God, This is very scary mtu wangu,usiombe mitafaruku izuke nchini kwako,maana itazoa michafukoge yote ikiwemo mivitu kama hizi z akutegeana mabomu.Askari analinda usalama wako wewe raia lakini wewe unamtegea bomu ili kumsend huko ulimwengu mwingine baada ya huu wa dunia.

Noma sana Boko Haram,halafu ukiwauliza hivi nyinyi Boko Hram ndio nini,wanakwambia tunapiga vita elimu zote za Magharibi,sasa mbona mmezidi nyinyi mijitu, kwani huyu askari ni wa magharibi au? si mnigeria mwenzenu huyu,jamani watu wengine bwana hawajui hata wanachokifanya wapo wapo ati Boko haram.

Siipendi Nigeria mimi we acha tu,kama sio Nwanko Kanu kuwa M-Nigeria ningeifuta kabisa Nigeria kutoka kwenye mind yangu.Itabidi sasa Tanzania kuwasaidia Raia wa Nigeria kuwatumia Jeshi letu lile la ukweli la fanya fujo uone a.k.a FFU liende kulinda amani ya wanigeria na kupambana na Boko Haram.

¬© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*