Tulonge

Rais Kikwete akubali kukutana na Chadema

AAGIZA WAPANGIWE SIKU YA KUKUTANA IKULU,CCM NGOMA NZITO
RAIS Jakaya Kikwete amekubali kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema kusikiliza madai yao juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, uliopitishwa bungeni juma lililopita.Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana jioni ilieleza kuwa Rais amelipokea ombi hilo kwa furaha kwa sababu ni jambo jema.

“Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ili kupanga tarehe mwafaka ya kukutana na viongozi hao wa Chadema na kuzungumzia suala hilo,” ilieleza taarifa hiyo.

Kabla ya Kurugenzi hiyo kutoa taarifa hiyo, Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga akizungumza na gazeti dada la hili, The Citizen alisema Rais amepokea jambo hilo kwa furaha.

“Tumepokea barua ya Chadema muda mfupi uliopita (jana jioni), ikiomba kukutana na Rais Kikwete na bahati njema Rais pia amependekeza kuwa yuko tayari kukutana na viongozi kutoka vyama vya siasa,” alisema Kibanga.

Uamuzi huo wa Rais umekuja siku moja baada ya Chadema kuunda kamati ndogo ya watu sita kwa ajili ya kuonana na Rais Kikwete na kuwasilisha madai yake juu ya muswada huo wa sheria.

Kamati hiyo iliyoundwa katika mkutano wa dharura wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, inataka kujadiliana na Rais kuhusu kile ilichoeleza kuwa ni upungufu uliopo katika muswada huo uliopitishwa na Bunge na kutaka Rais atafakari kama ausaini kuwa sheria au la.

Akisoma tamko hilo kwa vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika makao makuu ya chama hicho, Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kamati hiyo ya watu sita, ilikuwa ikifanya taratibu za kumuona Rais Kikwete.

Mbowe alisema ushiriki wa Chadema katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya utategemea mazungumzo hayo baina ya wajumbe wa kamati ya chama chake na Rais Kikwete.

Ijumaa iliyopita, Rais Kikwete akizungumza na wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kuhusu uchumi na mchakato wa Katiba, alisema atautia saini kuwa sheria muswada huo licha ya kelele za wanasiasa za kuupinga.

Alitoa kauli hiyo huku akipangua hoja zote kuhusu mchakato huo zilizokuwa zikitolewa na Chadema kuwa muswada huo haukuzingatia kanuni zitakazowezesha demokrasia.

Kauli hiyo ya Rais ilikuja saa chache baada ya Bunge kupitisha muswada wa mabadiliko ya Katiba ambao ulisusiwa na wabunge wa Chadema na NCCR-Mageuzi kwa madai kuwa mchakato mzima una kasoro.

Kamati Kuu CCM bado siri nzito

Huko Dodoma, ajenda kuhusu Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ilijitokeza kwa sura isiyo rasmi wakati Kamati Kuu (CC), ilipokuwa ikijadili taarifa ya uchaguzi mdogo wa Igunga iliyowasilishwa na aliyekuwa Kiongozi wa Kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba lakini haikudumu.

Habari kutoka katika kikao hicho zinasema mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akichangia hoja ya uchaguzi wa Igunga alisema hali ya vijana wa jimbo hilo na kwingineko nchini kukichukia CCM ni kutokana na Umoja wa vijana kutotekeleza wajibu wake, badala yake kujishughulisha na mambo mengine yasiyokuwa na tija.

Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Isimani, Iringa alinukuliwa akitoa kauli hiyo baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira kusema kuwa tatizo katika uchaguzi mdogo wa Igunga walikuwa ni vijana wengi ambao walionyesha chuki kwa CCM wakati wa uchaguzi huo, wakidai kutoshughulikiwa kwa matatizo yao.

Uchaguzi Igunga
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zimeeleza kuwa katika siku ya kwanza ya kikao chake juzi, CC ilipokea taarifa ya uchaguzi mdogo wa Igunga ambao ulimwingiza bungeni, Dk Dalaly Kafumu.

Ripoti ya Igunga iliyowasilishwa na Nchemba iliweka bayana kwamba hali katika uchaguzi huo ilikuwa mbaya kiasi cha kuwepo kwa hofu ya CCM kushindwa uchaguzi.

Nchemba alinukuliwa akieleza mitafaruku kadhaa iliyotokea wakati wa kampeni kiasi cha kuwafanya madiwani wa CCM Igunga kutishia kujitoa katika chama na kuingia upinzani, lakini akasema suala hilo lilimalizwa kwa kutumia busara, hatua iliyokiwezesha kupata ushindi.

Baada ya taarifa ya Mwigulu, Mwenyekiti wa kikao hicho, Rais KIkwete anadaiwa kwamba alihoji ukweli wa taarifa za baadhi ya makada wa chama hicho kuwapigia kampeni wapinzani kwa kutumia kauli mbiu ya “Tushindwe ili tuheshimiane”, swali ambalo hata hivyo, halikupata majibu kutokana na wajumbe kukaa kimya.

“Mwenyekiti aliuliza tena kwamba kuna watu waliompigia simu na kumtumia meseji (ujumbe mfupi wa simu wa maandishi), kwamba kuna makada waliokuwa wakiwapigia kampeni Chadema, lakini wote walikaa kimya na ndipo aliposema kwamba tuache majungu na fitina,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya mkutano huo.


Source: www.mwananchi.co.tz

Views: 520

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on November 28, 2011 at 11:05

angela ngoja nikufupishe mimi sio mwarabu hilo la kwanza halafu la pili huko kigogo kwa nyuma siendi labda unipeleke kwako nikakae kwa mbele, nitafurahi sana,

Comment by eddie on November 25, 2011 at 16:28

Bonielly una maana Keith Sweat?

Comment by ANGELA JULIUS on November 25, 2011 at 14:57

Mpendwa wangu Bonielly unajua walichoenda kuomba waingie ikulu kuonana na bwana mkuu kinajulikana na ile ni kamati ambayo iliundwa na chama kwa ajili ya wale viongozi wa chadema waende kuongelea dukuduku lao la Katiba. sasa sidhani kama wanaweza kwenda kumwona mkuu wa nchi wakaomba kwenda kumwona Zitto india au bla bla bla  nyingine hapo nakataa cha mzingi  tusubili muafaka wa kilichowapeleka huko. ila umenivunja mbavu sana mwarabu mwenzangu lol ha ha ha kesho subili nikupeleke kwa mama Sakina pale kigogo kwa nyuma.

Comment by Bonielly on November 25, 2011 at 10:02

mimi sishangilii kuwakubalia wapinzani kukutana no, nitashangilia kitakachoongelewa, ni kitu gani na kinafaida gani kwa wananchi? wanaweza wakaomba kukutana na rais halafu wakaomba na hao waende india kumuangalia zito, au wakaomba safari ya kwenda nje na hao wakapige picha na keyth sweet, kwaio kuomba kukutana sio isssue, kikubwa ni kitugani kinachowataka kufika ikulu? leo tunawashangilia bungeni mimi mpaka leo sijaona faida ya hilo jengo, naliona kwenye picha ni zuri sana lkn halina faida yeyote ni mabishano kelele zisizo na muelekeo wowote mpaka leo mazaga yanapanda maumeme ndio hayo yanapanda, mafuta dora zinapanda, mishahara mpaka sasa haijapanda, 

 

mtazamo wangu mimi niifurahii tanzania kabisa,

Comment by Dixon Kaishozi on November 23, 2011 at 10:44

Mwanzo mzuri.. si kila siku kupigana mabomu.. JE KITA ZAA MATUNDA? AU NDIYO ITAKUWA BALAA KABISA ?

SASA NASUBIRI HATMA YA HICHO KIKAO..

Comment by ANGELA JULIUS on November 23, 2011 at 7:39

NAMPONGEZA JAKAYA KWA UAMUZI WAKE NACHOSUBILI NI KUONA HATMA YA MAELEWANO YAO KWA MASLAHI YA TAIFA. 

Comment by Gratious Kimberly on November 23, 2011 at 1:24

Yeees sasa bora maelewano yaanzie hapo, pia asikilize point muhimu za wapinzani maana nao wana vipengele vya maana kwetu sisi.   bora hivyo wakutane waongee kuliko malimbano ya kila siku!!..........Enhe ukiona hivyo ujue mzee kaona ikulu inaweza kuwaka moto!!

Comment by Tulonge on November 23, 2011 at 1:14

Hongera JK, umeonesha uungwana na kukomaa kisiasa kwa kukubaliana na ombi hilo la kukutana na  viongozi wa Chadema japo bado hatujajua nn hatma ya kukutana kwenu.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*