Tulonge

Rais wa Serikali ya Wanafunzi UDom atiwa mbaroni kwa wizi

Taarifa kutoka kwa Josephat Lukaza zinasema Rais wa Kitivo vya Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha anayefahamika kwa jina Idd Mohamed pamoja na mwanafunzi mwingine ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Kitivo hicho aliyejulikana kwa jina la Ibrahim Matata wanashikiliwa na Polisi katika kituo cha Polisi cha Chuoni hapo.

Wote wakiwa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu katika fani ya BCom Accounting, walikamatwa jana, Alhamisi kwa tuhuma za wizi wa fedha wa kiasi cha Shilingi milioni 15.6 na kulazwa rumande kwa uchunguzi zaidi na hatua za kisheria, kabla ya kufikishwa mahakamani.

Watuhumiwa ealipopekuliwa baada ya kukamatwa walikutwa na kiasi cha shilingi milioni 7,224,000/=, fedha ambazo zinasadikiwa kuwa zilitolewa kwenye akaintu ya Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha na kisha kupelekwa katika kaunti ya mtu binafsi ambaye imefahamika kuwa ni ya mtuhumiwa, Ibrahim Matata.

Awali Raisi huyo alihusika na kosa la kuomba rushwa ya Shilingi milioni 1.1 kutoka kwenye duka lililopo katika bweni namba 13 (Block 13 ).

Habari zaidi ambazo Lukaza imezipata kutoka kwenye vyanzo vingine vya habari zinadai kuwa watuhumiwa hao wanatarajia watafikishwa mahakamani Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa fedha hizo.

Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha cha UDom lilipanga kukaa leo saa 10 jioni ili kutoa uamuzi wa kimadaraka wa watuhumiwa, na kufikisha baadhi ya ushaidi wa sauti wakati Rais huyo alipokuwa akiomba rushwa.

via freebongo blog

Views: 358

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by top on January 5, 2013 at 10:12

sasa uyo jamaa asitoke maana alionekana toka mwanzo hafai ila serikali ya chuo ikamchakachua jamaa aliyekuwa kipenzi cha wengi na alionekana mtu makini. haki itenmde wajibu wake.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*