Tulonge

Sababu iliyomfanya Mh.Rosweeter(60) kukubali kuolewa na Kijana wa miaka 26

Mh. Rosweeter Kasikila

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rosweeter Kasikila (60), amejikuta kwenye kashfa nzito ya kufunga ndoa na kijana, kinda wa miaka 26, Michael Christian.

Ndoa hiyo ilifungwa katika Kanisa la Tanzania Assembles of God (TAG), linaloongozwa na Mchungaji Getrude Rwakatare ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu wa CCM. Ndoa hiyo imekuwa gumzo baada ya kuwaacha hoi baadhi ya wabunge, mawaziri na majirani wanaoishi na mbunge huyo.

Baadhi ya watu waliopo karibu na wanandoa hao na majirani wanaowazunguka wamesema kwamba ndoa hiyo ilifungwa Septemba Mosi mwaka 2011, na sasa imebaki kuwa siri kubwa licha ya wanandoa hao kugombana.

Wiki hii yote kumekuwa na kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kumefunikwa na tukio la kustaajabisha linalomuhusu mbunge wa CCM Rosweeter Kasikila mwenye umri wa zaidi ya miaka sitini kufunga ndoa na kijana mdogo Michael Chstiani (26) Mtandao huu umepata taarifa mpya juu ya tukio hilo ambalo kwa sasa liko kwenye mgogoro mzito.

Habari toka kwenye chanzo chetu cha habari zilisema kuwa sababu kubwa ya Mheshimiwa huyo kuangukia kwenye penzi l "Serengeti boy" huyo ni kutokana na ufundi wa hali ya juu wa kijana huyo hali iliyofanya Mama huyo kushindwa kujizuia na kuamua kumfanya kijana huyo kuwa mume kabisa.

Mama mmoja wa makamo ambae alisema ni rafiki wa karibu na Mbunge huyo alisema " Jamani wanangu acheni mapenzi yaitwe mapenzi ambayo hayana macho haya hata mkificha lakini baadae kila kitu kitakuwa wazi huyo kijana ana sifa ya kujua sana mambo anasifika mtaa mzima hivo Mh alizidiwa na uzalendo akaamua kufunga ndoa nae ili kufaidi ndoa vizuri" Alisema mama huyo.

Aidha ishu hii licha kutizamwa kwa jicho la tatu na baadhi ya watu huku ikiwa na mlengwa wa kisiasa pia watu mbalimbali walitoa komenti zao na kueleza kuwa Mh huyo hakuwa na kosa kufanya maamuzi ya kuolewa na kijana huyo ambae kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu huyo kijana ni mtu mzima kwa maana ya kuvuka miaka 18

Via: Tuangaze Blog na Tanzania Daima

Views: 2147

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on December 4, 2013 at 10:06

unaonaeeeee ulijuaje kama mimi ni bata,

Comment by ANGELA JULIUS on November 27, 2013 at 16:35

okeeeeeeeee bata wewe

Comment by Bonielly on November 27, 2013 at 14:50

kwahiyo macho yako poa? sasa jiandae na nguo zako za mwaka mpya bunge likianza nikuombee lift muheshimiwa yeyote akakuache hospt yetu ya matatizo yetu, ukapate dozi zetu, ili upone ugonjwa wetu, ukirudi njoo uchukue kakuku ukapate supu, sawaaaaa?

Comment by ANGELA JULIUS on November 26, 2013 at 15:25

DAH ITAKUWA POWA UKINIRUDISHA BUNGENI KUPATA DOSE ILIYOBAKI MANAKE ILE IMEYEYA.

Comment by Bonielly on November 26, 2013 at 14:26

au tatizo macho? kama macho nisipoteze nauli yangu, 

Comment by Bonielly on November 26, 2013 at 14:24

sasa hapo nilipoweka mayai pembeni yake kidogo sindio nilipokonect  vi mordem vyangu vya voda tigo na zantel, kwanini usivione, yani uone mayai modem usione, basi itabidi nikurudishe bungeni, ukachukue dozi iliyobaki,

Comment by ANGELA JULIUS on November 25, 2013 at 17:02

sasa Boniely naona unanifanya sina akili aku miye sijauona ila mayai nimeyaona

Comment by Bonielly on November 25, 2013 at 12:08

angela acha unafki ulivyokuja kuchukua mayai hujaona mtandao kweli? 

Comment by ANGELA JULIUS on November 20, 2013 at 16:39

UKAJIFICHE WAPI WAKATI HUNA MTANDAO HAPO ULIPO SIJUI HATA UMEAZIMA KWA NANI.

Comment by Bonielly on November 20, 2013 at 16:32

oooooho balaa limeanza ngoja nirudi nilikokua nimejificha

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*