Nazungumza swala hili na wala sibahatishi, bali nina uhakika kuwa:Utumiaji ulevi (hasa wa pombe) una taathira mbaya za kimwili na kiroho kwa mtumiaji, kiasi kwamba, baadhi ya madhara na athari zake haziwezi kufidika. Hii leo utumiaji ulevi umegeuka katika baadhi ya jamii na kuwa tatizo kubwa na kila siku madhara yake katika jamii hizo yanazidi kuongezeka na kutishia mustakabali wa jamii husika.
Watalaamu wengi wanaamini kuwa, kuna mambo na sababu nyingi zinazowafanya baadhi ya wanajamii hasa katika ulimwengu wa Magharibi kumili(kuelekea) katika ulevi na utumiaji pombe.
Mtafiti mmoja wa Kimarekani anayejulikana kwa jina la Horton baada ya kufanya utafiti katika muongo wa 1940 alifikia natija hii kwamba, kadiri kiwango cha mvurugiko na hali ya kutetereka katika jamii kitakavyokuwa kingi basi ndivyo utumiaji wa pombe unavyoongezeka kwa kiwango hicho hicho.
Anasema kuwa, katika utafiti huo inaeleweka wazi kwamba, endapo thamani na utamaduni unaotawala katika jamii utakuwa ni utamaduni na thamani ambazo zinashajiisha watu kutumiaji ulevi, bila shaka jambo hilo litakuwa na taathira kubwa katika kuongeza kiwango cha utumiaji ulevi katika jamii hiyo.
Wataalamu wa mambo wanataja sababu kuu mbili za kimsingi ambazo anasema zinachangia watu kuelekea katika utumiaji ulevi, sababu ambazo wamezigawa katika makundi mawili yaani sababu za ndani na za nje.
Wanasema kuwa, sababu za ndani ni msononeko, matatizo ya kisaikolojia, hali ya wasi wasi na kutofungamana na misingi ya dini na ya kiakhlaqi. Sababu za nje ni kama vile umasikini, hali mbaya ya kijamii na kiuchumi, kutokuweko uthabiti wa kiutamaduni, kusambaratika maisha ya familia na kujihusisha wanajamii na mambo machafu pamoja na ufuska.
Majimui ya sababu hizi ni mambo yanayotajwa kuwa yanaongeza uwezekano wa kumili upande wa utumiaji madawa ya kulevya na ulevi.
Sio mbaya tukaaashiria katika nukta hii ifuattayo kuwa:
Mwenyezi Mungu mwenye huruma amemuumba mwanaadamu na vilivyomo ardhini na kumleta hapa duniani ili anufaike na vilivyomo katika dunia hii "kwa njia sahihi" na kwa mujibu wa maamrisho na mafundisho ya dini.
Hivyo si vizuri kwa mwanadamu kukata mahusiano na dini na kujiweka mbali na Mola wake,akifanya hivyo ajue hatafuti ispokuwa kuangamia na kupoteza mwelekeo ulio sahihi.
Njia sahihi ya kuwa katika mstari ulionyoka na kupata mafanikio hapa duniani na kesho kwa Mola wako ,ni kumuweka Mwenyeezi Mungu katika maisha yako na kumpa nafasi kubwa ya kuendesha maisha yako,la sivyo ujue kuwa maisha haya ni mafupi mno yenye raha fupi mno kupita maelezo,ni kesho tu utaachana na duniani hii,na utakuja kukutana na Mola wako,hivyo jiandae kukabiliana nae !,ikiwa ulijiepusha nae na kujitenga nae,ukaamua kuwa cha pombe na kufanya utakavyo,hutaki ushauri wa kiroho kutoka kwa yeyote,si padri wala shekh,basi siku hiyo utajutia kuwa mwanadamu,yaani utatamani bora ungeliumbwa mchangwa !! watu wakakutumia kujengea nyumba zao na sio kuwa mwanadamu!,lakini ikiwa ulichagua kumfanya Mola kuwa mwongozaji wa maisha yako,basi ujue siku hiyo unakutana na Mola wako,utakula vya kukaangiza ambavyo havijawahi kutia maguu wala kuonekana hapa duniani.
Tuzingatie kipengere hichi:
Kama tulivyokwisha nena kuhusu maudhui hii siku za huko nyuma ndani ya Tulonge hii ni kuwa, moja ya madhara makubwa ya utumiaji ulevi ni mfarakano katika familia, maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, unene kupita kiasi, utapiamlo hasi, mimba kuharibika na kisukari,na hata kupata mimba za ghafla ghafla kwa mwanamke chapombe! maana ile mijitu maarufu ikimkuta mwanamke mlevi kalewa nzwiiii tena maeneo maalum,basi hapo hakuna cha salamu wala unaitwa nani,ni twende tu!.
Baadhi ya wataalamu wanasema kuwa, utumiaji ulevi una madhara ya aina mbili. Kwanza ni kuathirika kwa mishipa ya fahamu mwilini kote kwa kupunguzwa uwezo wa kufanya kazi kama inavyotakiwa; na pili ni kuungua baadhi ya ogani za mwili hasa tumbo pindi mtu anapobugia pombe.
Enewei,naomba ujumbe huu uwe ujumbe wa busara na wenye faida kwa yeyote mlevi au anayekaribia kuwa mlevi.
Na Chalii_a.k.a_ILYA
Add a Comment
Kaka chaoga wapi Mkuu,maoni muhimu!
mada nzuri kaka Ilya na inaelimisha kwakweli, ni vyema wanywaji wakajitazama upya.
Pombe hatari, jirani yangu baba mtu mzima alianza pombe taratibu, hivi sasa mlevi kupindukia hadi mkewe na watoto wamemkimbia.
Ahsante kwa ushauri huo wa bure. Wengine kuupata hadi wapitie clinics ambapo hulipia !. Pombe ni noooma !.
Asante sana kwa elimu mkuu Ilya. Nadhani Chaoga ataacha pombe sasa teh teh teh
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge