Tulonge

Sasa "Lulu" atinga uraiani rasmi kwa dhamana

Lulu akiwa na Mama yake ndani ya gari iliyokwenda kumchukua.

Hatimaye msanii wa filamu Elizabeth Michael "Lulu", leo ameingia rasmi mtaani baada ya Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam kuipitisha dhamana yake ikiambatana na masharti lukuki. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake marehemu Steve Kanumba tar 7 Aprili 2012.

Lulu akiwa na Mama yake na Dk.Cheni wakitoka mahakamani mara baada ya kukamilisha mchakato mzima wa dhamana.

Gari iliyokwenda kumchukua Lulu

Views: 510

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 3, 2013 at 0:05

Hongera sana binti kurudi uraiani. Bado mdogo sana. Kuwekwe sheria kali kuhusu mafataki wanaolala na watoto walio chini ya umri wa miaka 18.

Comment by Amina Massawe on January 30, 2013 at 11:42

Jikite kwenye Ibada mwanangu mungu akusaidie kwani kwavyovyote vile utakuwa umeasirika kisaikolojia kwa hili tukio kulingana na umri wako. Na itakusaidia kuwa na muonekano mpya mbele za jamii inayokuzunguka. kila la kheri mamy.

Comment by Christer on January 30, 2013 at 11:16

Machozi ya furaha na maza. poleni na hongera kwa kuwa huru ingawa ni kwa masharti bora kuliko Sero.

Comment by David Edson Mayanga on January 30, 2013 at 1:35

mh mh mh mh mh mh mh mh kaibu binti wangu wawooooooooooooooooooo ntakuja kukupa hai huko tabata sawa lulu

Comment by Tulonge on January 30, 2013 at 1:01

Upo sahihi Ilya. Binafsi nashindwa kuwaelewa wanaopenda Lulu aendelee kusota jela, nimepitia comments za watu kibao ktk mitandao ya kijamii nikagundua wengi wanaotaka Lulu aendelee kusota Jela ni wanawake/wasichana wenzake.Utadhani wana hakika 100% kuwa Lulu alitenda na alitenda makusudi. Yani wamesahau kabisa kuwa 'Leo kwa Lulu kesho kwao'

Binafsi ninamuhurumia sana huyu dogo, natamani kesi yake iishe hata kabisa.

Comment by ILYA on January 30, 2013 at 0:53

Jela Noma,Nakumbuka picha moja ya KANUMBA inayoitwa BIG DADY,katoto kake kanakoitwa SOPHIA ktk picha hiyo kaliendesha gari na hatimae kakabambwa na polisi.Kanumba baba yake akaitwa ktk kituo cha Polisi.Alipohojiwa kwanini unamruhusu mtoto chini ya miaka 18 kuendesha gari,alikosa jibu:Akasema mimi mwenye nashangaa kawezaje kuendesha gari.Polisi wakasema:Wewe unatuchezea sio,sasa lazima ukapumzike Jela! Nilipenda jibu la Kanumba baada ya kuambiwa na Polisi hao kuwa lazima tukutie Lock Up a.k.a JELA,alisema:NDUGU ZANGU MAPOLISI,KWANINI MNAG'ANG'ANIA JELA?!,JELA NDUGU ZANGU SIO MSIKITINI WALA KANISANI,NISAMEHE TU,MIMI NI MZAZNI KAMA NYINYI,LEO YAMENIKUTA MIMI KESHO UNAWEZA KUWA WEWE.!

Comment by Tulonge on January 29, 2013 at 23:12

-Pole na Karibu uraiani Lulu. Tunakuombea soo liishe kabisa.Huwezi jua, hii inaweza kuwa ni njia ya kukufanya ung'ae zaidi ktk kazi yako na kutengeneza life lako zaidi.

-Hongera sana Dk. Cheni, nakumbuka ndiwe uliyemuingiza Lulu kwenye uigizaji akiwa mdogo sana. Na sasa umeonesha kuwa karibu naye sana katika tatizo linalomkabili.Nimeipenda hiyo

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*