Tulonge

Shinyanga: Wachawi wawili waanguka na ungo wakiwa watupu

WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)

Watu wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.

Watu hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.

Katika maelezo yao wazee hao wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa wanaelekea.

Sambamba na hayo imeelezwa kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo na mama mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.

Jeshi la Polisi la Wilayani humo likiri kutokeakwa jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.
Wakiwa ndani ya gari kuelekea kituo cha polisi
Eneo hili ndipo walipo anguka

Views: 2383

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on April 10, 2013 at 1:12

African doctrine, wangekuwa wachina mngewasifia kwa technologia bomba ya muda mfupi bara moja hadi jingine kiulaini watufundishe tukasome shule za day ulaya na malekani maana huku elimu si tia maji tia maji. tuache ushabiki anae kataa kwao ni mtumwa.

Comment by ANGELA JULIUS on April 9, 2013 at 11:33

duh wanatia aibu kweli arobaini yao imefika

Comment by KUNAMBI Jr on April 8, 2013 at 12:18

Duuuh noma

Comment by Christer on April 8, 2013 at 10:21

Arobaini si kwa wezi tu hata Wanga.

Comment by sharon peace on April 8, 2013 at 1:27
Wanalaana hawa maana hata huo uchawi cjui unawasaidiajee kwa umri wao, wao bado wanapinga ule usemi wa "shetani akizeeka huwa malaika"
Comment by Tulonge on April 8, 2013 at 1:19

Wenzao wengi wa umri wao wamemrudia Mungu ili awasamehe dhambi zao walizozifanya nyuma. Sasa wao ndo wanazidi kujiongezea dhambi.

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*