
WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI (70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)
Watu wawili wamenusurika kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya kishirikina.
Watu hao waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80) wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za kishirikina.
Katika maelezo yao wazee hao wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani, ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa wanaelekea.
Sambamba na hayo imeelezwa kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo na mama mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.
Jeshi la Polisi la Wilayani humo likiri kutokeakwa jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.

Wakiwa ndani ya gari kuelekea kituo cha polisi

Eneo hili ndipo walipo anguka
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge