Tulonge

Simba yaifumua Yanga 3-1 katika mchezo wa Nani Mtani Jembe

Timu zilipokua zikijiandaa kuanza mchezo (picha na Salehejembe blog)

Timu ya Yanga leo imekiona cha mtema kuni baada ya kufungwa bao 3-1 na Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Matokeo haya yamekua tofauti kabisa na jinsi watu wengi walivyodhani, kwani nafasi kubwa ya ushindi ilipewa Yanga ambayo imesheheni wachezaji wenye majina makubwa.

Simba waliingia uwanjani kama watoto yatima ambao walitegemea na kutilia maanani mafunzo waliyopewa na kocha wao. Lakini Yanga waliingia uwanjani kwa kujiamini na kucheza bila umakini na kupelekea kupoteza mpira mara kwa mara. Hali hii iliifanya Simba kuanza kutawala mpira.

Dakika ya 13 Simba iliandika bao la kwanza kupitia Hamis Tambwe, kabla ya kuifungia Simba bao la pili dakika ya 43 kwa penati baada ya Davidi Luende wa Yanga kumfanyia madhambi Ramadhani Singano eneo la hatari. Dakika ya 62 Awadhi Juma aliifungia Simba bao la 3.

Dakika ya 87 Emmanuel Okwi aliyeingia dakika ya 57 aliipatia Yanga bao la kufutia machozi. Hadi mwisho wa mchezo Simba 3-Yanga 1.Views: 318

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*