Tulonge

Taarifa ya Afisa Uhusiano wa hospitali ya Muhimbili kuhusu hali ya huduma ilivyo leo

Taarifa niliyopata kutoka kwenye Kurugenzi ya Tiba, Kurugenzi ya Upasuaji, Kurugenzi ya Tiba Shirikishi na Kurugenzi ya Uuguzi ni kama ifuatavyo;

Kurugenzi ya Tiba:Huduma zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kati wagonjwa ni wachache wanaokuja kutibiwa.

Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa wote na Registrar wote wamefika kazini na wanafanya kazi. Interns 11 wamefanya kazi. Major ward round zimefanyika. Kliniki zote za leo zimeendelea kufanya kazi pia cliniki za mchana zitafanyika.

Idara ya watoto, Madaktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi wapo wadini wanaona wagonjwa. Changamoto ni kwamba inabidi pia wafanye kliniki za wagonjwa wa nje na wanajitahidi kufanya hivyo.

Idara ya magonjwa ya nje.Registrars na Daktari Bingwa wote wapo na wanafanya kazi.

Idara ya magonjwa ya afya ya akili, Madaktari Bingwa wote wamefika kazini . Bada ya wagonjwa wote kupelekwa wodini, walionwa na madaktari. Wagonjwa katika kitengo hiki ni wengi ukilinganisha na idadi ya madaktari bingwa, lakini kliniki zimeendelea kufanyika kwa kiwango cha kati. Kiliniki ya wagonjwa wajidunga imefanyika.

Idara ya magonjwa ya dharura,Registrar wote wamesaini lakini wliofanya kazi ni wawili tu. Daktari Bingwa yupo na anafanya kazi.

Idara ya mazoezi ya viungo,Wafanyakazi wote wapo na wanafanya kazi.

Kurugenzi ya Upasuaji:Huduma za upasuaji zinafanyika lakini siyo sawa na jinsi zilivyokuwa zinafanyika kabla ya mgomo kwani wagonjwa ni wachache kwenye baadhi ya kliniki na baadhi ya kliniki wagonjwa wanakuwa wengi. Wagonjwa wa upasuaji walioko wodini wanaonwa japo ni wachache ukilinganisha na hali ilivyokuwa. Baadhi ya huduma za upasuaji (operations) zimefanyika ingawa wagonjwa ni wachache kwa vile idadi ya wagonjwa wanaokuja kliniki au waliolazwa kwa ajili ya upasuaji ni wachache.

Huduma za Tiba Shirikishi: Vipimo vya maabara na vile vya uchunguzi wa radiolojia vinaendelea kufanyika kama kawaida ingawa idadi ya vipimo vimepungua ukilinganisha na kabla ya mgomo. Idara ya famasia pia inafanya kazi kama kawaida. Idadi ya wagonjwa wanaoandikiwa dawa ilipungua ukilinganisha na kabla ya mgomo.

Kurugenzi ya Uuguzi Huduma za uuguzi zimeendelea kutolewa kwa kiwango cha kawaida.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 3, 2012

Source: http://www.wavuti.com

Views: 322

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*