Tulonge

TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA

YAH: TAMKO FUPI LA JUMUIYA YA MADAKTARI KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 28.06.2012

Madaktari wote hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini yenye lengo la kuendesha uchunguzi juu ya kutekwa, kunyanyaswa na kupigwa vibaya kwa Dr. Ulimboka Stephen na tunataka chombo huru kiundwe ili kupata ukweli wa tukio hilo.

Pia tunakemea na kuonya juu ya vitisho vyote vinavyotolewa na baadhi ya watawala katika taasisi mbalimbali dhidi ya madaktari mfano Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Bugando, Mbeya na kwingineko ambapo wametishwa na kufukuzwa kwa kutumia mabavu.

Madaktari tunazidi kusisitiza kuwa hakuna njia nyingine yeyote ya kusuluhisha mgogoro huu isipokuwa ni kwa kutekeleza madai na hoja za msingi za madaktari kwa njia ya mazungumzo ya dhati.

Madaktari tumechoka kuona huduma za afya nchini zikizidi kudorora mwaka hadi mwaka, Tumechoka kuona wagonjwa wakilala chini na watoto wakilala wanne katika kitanda kimoja Tumechoka kuona msongamano mkubwa kwa wagonjwa katika hospitali zetu huku kukiwa hakuna mpango wowote wa uboreshaji.

Tumechoka kuona wagonjwa wakikosa dawa, vipimo sahihi na watumishi wa afya wakifanya kazi katika mazingira magumu yanayoviza ubora wa huduma na misingi ya taaluma.

Kwa hiyo, kwa moyo wetu leo tumejitolea kutetea uboreshaji wa sekta ya afya licha ya vitisho tunavyoendelea kuvipata.

Rai kwa Madaktari; Madaktari wote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu, tunashukuru madaktari wote kwa ushirikiano na kuendelea na mshikamano.

Imetolewa na Kamati ya Jumuiya ya Madaktari.

Views: 258

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on June 30, 2012 at 20:55

Na hata hiyo laki 9 wanayopewa watu wanasema ni nyingi kusema ukweli sio nyingi kwa mazingira ya kazi. Nchi za wenzetu wanaojali viwango vya kazi, ugumu wa kazi na mazingira ya kazi kunakuwa na mfumo wa mishahara na malupulupu. Mfano hapa UK, doctor anayemaliza masomo na kuanza kazi mshahara wake ni mkubwa kuzidi mbunge wa jimbo lake. Na mishahara na malipo yote yako transparency. Kwa malipo hayo kutokana na ugumu wake wa kazi anakuwa na allowances nyingi ikiwemo fuel allowance anayolipwa kwa mile/km toka makazi yake kwenda kituo cha kazi. Hiyo inamsaidia kuwa na msimamo wa maisha na pia kazi. Hukuti doctor doctor ana randa randa kikazi sijui leo yuko zamu private hospital kesho government hopital, anakuwa sehemu moja. Na system hiyo ni very effective imefanya kila raia kuwa na family doctor (GP) wake kipindi chote, na doctor yuko ready muda wote unapomuhitaji, na hata usipoweza fika hospital atakuja nyumbani kwako. Sirikali inamlipa kufanya hivyo na sio wewe.

Tanzania na nchi nyingi za Africa mwana siasa anayepiga porojo na kusinzia bungeni ndio anayelipwa pesa nyingi. Na hiyo ndio imefanya baadhi ya medical professionals Tanzania kukimbilia siasa. Na kwetu tatizo la kutojali viwango vya kazi kwenye mishahara na malupulupu sio doctors tu peke yake bali hata walimu nao wamesahaulika kabisaaaa...

Comment by Mama Malaika on June 30, 2012 at 20:24

Usijali Cha the Great... naelewa jinsi ulivyo na uchungu hasa ukizingatia wananchi ndio wenye kuathirika na hili. Kitu kinachonishangaza zaidi ni kwamba kuna watu Tanzania wanaona kuwa madai ya doctors ni ya kisiasa, hivi mtu kudai yake ni siasa? Doctors wanapigania mazingira mazuri ya wagonjwa (ambao wengi ni walalahoi) bado mtu anaona ni siasa. Sijui lini watu vichwa vitamka na kuona mbali? Hospitals za Tanzania hali iliyokwepo miaka 20 iliyopita ni mbali kabisa na sasa, watu hawakulala zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja, hivi sasa hata gloves na pamba kwenye government hospitals vimekuwa adimu, mgonjwa aambiwa akanunue kwenye pharmacy pale kwa gate. Nchi imekwisha.... hata Rwanda iliyoharibika na vita hivi sasa hospitals zao zina huduma nzuri kuzidi hata sie

Comment by CHA the Optimist on June 30, 2012 at 19:14

Mwaka jana kwa mujibu Katibu wa Jumuiya ya Madaktari,Dk Edwin Chitage mwaka jana yaani (2011)  zilitumika kiasi cha bilioni saba kuwalipia wagonjwa matibabu nje ya nchi, na mwaka huo huo, zilitumika bilioni zisizozidi 5 kuendeshea hospitali kama tano hivi nchini, sasa huu kama sio upumbavu ni nini? Samahanini kwa ukali huu wa maneno, inabidi iwe hivi kwa sababu inauma sana si tu kwa mimi bali kwa raia yeyote mwenye akili timamu. Kuhusu mishahara hawa watu wana kila haki ya kudai kuongezewa mishahara, na maelezo kuwa serikali haina hela ni ya kipuuzi ambayo haistahili yasikilizwe, serikali ingekuwa haina pesa wabunge isingewezekana kulipwa milioni kumi kwa mwezi. Huu ni ujinga.

Comment by Mama Malaika on June 29, 2012 at 20:23

Sina la kusema....

Comment by Mama Malaika on June 29, 2012 at 20:23

Duh! Yaani imefikia kitanda kimoja kulaliwa na mtoto zaidi ya mmoja? Sasa mtoto akichangia kitanda na mtoto mwenzie si ndio wanaambukizana magonjwa? Na siku hizi maradhi yalivyo mengi ni balaa

Comment by jemadari mimi on June 29, 2012 at 10:36

Siwezi kuwalaumu madaktari hao kwanindio mfumo wetu ulivyo,hata police ama mwanajeshi akichezea kichapo mtaani ni lzm nao walipize ,sasa la ajabu lipi wao wakisema tunagoma kwa sababu hatuna imani na se

rikali juu ya maisha yetu.

kuhusu kutokuwa na imani na jeshi la police ni kweli kabisa maana hawatatenda haki kama kuna mkono wa serikali ktk issue hii,nadhani sote tunakumbuka ile issue ya DK MWAKYEMBE ,sijui wamesema nini ?haya na ile ya mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge walifunikafunika tu mpaka kuonekana watuhumiwa  hawana hatia.

binafsi ningependa kamati hiikuchunguza issuehii

jenerali ulimwengu-katibu

january makamba-mjumbe

kafulila-mjumbe

john mnyika-mjumbe

bisimba -mwenyekiti

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*