Tulonge

Tamko la Idara ya Usalama wa Taifa kuhusu kuhusishwa na kutekwa Dkt. Ulimboka

Katika siku za hivi karibuni, kumejitokeza taarifa zenye tuhuma kadhaa dhidi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Taarifa hizo zimekuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari zikiihusisha Idara hii na matukio ambayo yanaidhalilisha na kuzua maswali mengi kwa wananchi. Kati ya tuhuma hizo ni tukio la kutekwa kwa Dr. STEPHEN ULIMBOKA, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari na madai ya kufanywa kwa mipango ya kuwadhuru baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani. Gazeti moja la kila wiki limekuwa likurudia tuhuma hizo mara kwa mara kwa madai kwamba ni habari za uchunguzi na kuihusisha Idara.

Idara inataka kuwahakikishia wananchi kwamba taarifa hizo ni za UZUSHI NA UONGO ambazo zina nia ya kuharibu jina na sifa ya Idara. Taarifa hizo zimekuwa zikiunganishaunganisha vipande vya taarifa mbalimbali ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa na wanaolitumia gazeti hilo. Idara haikuhusika wala haihusiki na matukio yoyote yaliyotajwa katika tuhuma hizo. Hivyo tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo.

Matukio yaliyotajwa katika tuhuma hizo yanachunguzwa na Jeshi la Polisi ambacho ndicho Chombo Chenye Dhamana, na kwa Maslahi ya Taifa si vizuri kuachia upotoshaji huo uendelee.

Aidha, tunapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa uzushi na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Idara hazitatuvunja moyo bali zitatuunganisha na hivyo kutuimarisha katika azma yetu ya kuhakikisha nchi yetu inaendelea kubaki salama kwa kushirikiana na wanachi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.

Imetolewa na Idara ya Usalama wa Taifa,
Makao Makuu,
DAR ES SALAAM

26 Julai, 2012.

Views: 685

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on July 27, 2012 at 15:01

JEMADARI MIMI SINA CHA KUONGEZEA NAONA MASWALI NILIYOTAKA KUULIZA UMESHAULIZA KAZI KWAO WAHUSIKA LOL

Comment by jemadari mimi on July 27, 2012 at 11:54

Waswahili wanamisemo yao ya wanayopendena kusema mmojawapo niLINALOSEMWA NA WATU LIPO NA KAMA HALIPO LINANGOJEA.

Kama si kweli kwanini mseme uzushi na kudai gazeti linatumiwa,na je mnamtambua huyo anayelitumia gazeti hili kuchafua idara hii ya usalama wa taifa.mwanahalisi wamemtaja mtuhumiwa kwa jina lake,kitengo chake na hata picha.

swali ni kwamba mnamtambua huyu mtu au ndio mnanzuga kuwa mwanahalisi wazushi na pia kwanini wawazushie nyinyi tu kwani idara nyingine hakuna

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*