Tulonge

TID na Wema wapendekezwa zaidi kuiwakilisha Tanzania kwenye BBA 2013

Tarehe 26 tuliandika habari kuhusu Mastaa 10 wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa 2013. Katika majina hayo 10, Wema Sepetu, TID, Lisa Jensen na Fezza Kessy ndio walionekana kuwavutia wengi.

Leo kupitia ukurasa wetu wa Facebook tumeendesha kura ya maoni ambapo tumewataka watu wawataje mastaa kati ya hao wanne wanaoweza kuwa wawakilishi wazuri wa Tanzania. Katika kura hizo zaidi ya 800 TID na Wema ndio walioongoza kwa kutajwa zaidi.

Baada ya matokeo hayo tumempigia simu TID kumpa taarifa hiyo aliyoipokea kwa furaha kubwa na kudai kuwa hiyo ni ishara ya jinsi anavyokubalika kwa mashabiki.Tulipomuuliza kama atafikiria kuchukua fomu kwaajili ya kujaribu bahati yake, Top in Dar amesema kwakuwa watanzania wamemtaka afanye hivyo basi ataenda kuchukua.

Chanzo: bongo5.com

Views: 791

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Christer on January 30, 2013 at 11:39

Hahahahahaaaa @ David, yaani kwa mambo yanayofanyika mle ndani hata mimi nampa kura yangu Sepetu ndo atayaweza, wengine watatuzingua tu warudi mapeeema kama wale wa mwaka jana. Ila kwa TID sina hakika. swala la elimu ss sijui itakuwaje.

Comment by Kheri Mtani on January 30, 2013 at 8:51

TID siku hizi anapiga mkeka? naona sijda pale utosini..

Comment by David Edson Mayanga on January 30, 2013 at 1:40

makubwa shure hao wote hawajaenda je itakuwa aje?

Comment by Tulonge on January 29, 2013 at 23:27

Na kweli, Wema kutamfaa sana mule ndani

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*