Muonekano wa mji wa Lindi, picha hii niliipiga nikiwa muinuko wa Mtanda kwa Mla Mbwa. Mkoa wa Lindi una mji mdogo sana. Hapo unapo paona ndiyo mji mzima wa Lindi.
Hiki ni kisima kilichopo katika muinuko wa Mtanda. Kisima hiki husambaza maji baadhi ya maeneo ya mkoa wa Lindi.
Hapa nikiwa mtaa wa Santorini ambao upo karibu kabisa na Bahari. Mtaa huu ni balaa sana usiku.Ni mwendo wa wawili wawili kukumbatiana barabara nzima.
Hapa nikiwa kijiji cha Somanga nilipokua nikielekea Lindi
Majengo ya Lindi Sekondari kwa mbali
Hospitali ya Mkoa wa Lindi (Sokoine)
Hili jengo nililiona mitaa ya Lindi mjini nikaamua nilipige picha ili niwafurahishe washabiki wa timu flani hapa TZ.
Naona watanzania uzalendo umeanza kutuingia. Diamond akiwa amechorwa kwenye kibanda mtaa wa Msonobarini karibu na ofisi ya NMB Lindi
Chama cha walimu Tz mkoa wa Lindi, hapa ni mtaa wa Msonobarini karibu na Ofisi ya NMB Lindi
Hapa ni NMB Lindi mtaa wa Msonobarini. Ofisi hii utadhani ni nyumba ya kuishi mtu
Hiki ni kituo kikuu cha mabasi ya mikoani. Mimi nilidhani ni kituo cha daladala, kumbe ndio kituo kikubwa cha mabasi
Mambo ya kujipendelea korosho, hapa ni kituo cha mabasi
Wakati wa kurudi kuna mtu alikua anakula mahindi kama Ngedere hahaaahhhaha
Unaweza dhani ni gari ya mizigo, tuliionea kweli hii gari.Hapa ni kijiji kimoja kipo Shaurimoyo
Add a Comment
mmmmmmm Omary kweliiiiiii au unatufurahisha tuu
Safi sana dogo n hongera kwa tour. Hahahaahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa Omary umetisha! eti Bha!! kweli? teheeheteeheheeeee huyo hukumuacha bwana acha kututotosha hapa.
-Acha uongo wewe Omari, huyo binti hukumuacha wala nn. Nani asiye kujua wewe?
-Nilikutana na jamaa mmoja, nikamuuliza kitu. Duuh! kiswahili alichoongea ni balaa, nilidhani ananitania. Baadae niliamini anaongea hivyo baada ya kukutana na mwingine anaongea vile vile.
Hahahahaaa.... ya kweli hayo Omari? Eti ninamuongezea buku 2 alafu ukamuonea huruma!! hahahaaa
Baah bwana wewee Ah Aaaaaaaaaa umekula samaki nchangaaa?
pungo kwa nchelee kunogaaa doh! nimesahau kumbe tuliambiwa tuseme mbuzi wa usiku badala ya pungo hhahahaha Mama JK nisamehe kumwe na wewe ni wa kulekule alikotoka Dis hhahahah.
Dis ungechelewa kurudi ungekwama si unawajuwa wadada wa kule weeee! wangekung'ang'ania mpaka ungerudi na 1 me nilikwenda nikafikia hotel 1 hivi ipo kandokando ya bahari vijumba vya duwara vizuri sana ndani kila kitu sasa baada ya kumaliza kulipia nipo geto baadae nasikia nagongewa kufunguwa mlango naambiwa mwenzio huyo doh! roho ilinienda mbio nikakubali aingie baada ya kumuuliza akaniambia yeye kashalipwa na mwenye hotel hanidai doh! nikamuonea huruma kweli ila nilikuwa nasikia raha kiswahili chake nikamuongeza buku 2 nikamwambia sihitaji huduma achape lapa hakuamini akaniuliza bah! kweliii? nikamwambia ndio.
Georgia- Mambo yalikua poa sana ndani ya Lindi
Angela- Niliwatoroka kimtindo, nilienda kushangaa watoto wa Pwani kama asemavyo Mathias
Kunambi- Pa1 mkuu
Nashukuru kwa kuja kututembelea kijana
DUH NDO MANA NILIKUWA SIKUONI KWA MAMA SAKINA KUMBE ULIKUWA UNAKULA UPEPO WA PWANI, ASANTE KWA MATUKIO
Thanks Dismas mambo yalikuwa safi kabisa inaonyesha.
Nimekusoma mama
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge