Tulonge

Ujumbe muhimu kwa wasichana toka kwa mdau kuhusu 'Cancer'

Mdau (Wynne Vicent)

Wasichana wengi hawapo tayari kwenda fanya uchunguzi wa cancer ya shingo ya kizazi na matiti. Labda kwasababu wanajiona wako fit lkn ijulikane kwamba inachukua miaka mingi sana kuweza kugundua kwamba una huu ugonjwa na ukisubiri mpaka dalili zitokee inamaana ugonjwa umeshafikia hatua ya matibabu yenye gharama kubwa au haiwezekan tena kutibu.

Nimepata ushuhuda toka kwa mama mmoja anasema yeye alijiona ana kauvimbe kwenye titi tangu akiwa mschana lkn alikapuuzia sababu kilikua hakiumi, sasa ni mtu mzima kabisa na ameamua kwenda hospitali kwavile kimekua kikubwa na kinamuuma sana kiasi kwamba amepewa apointimenti anaona ni mbali na analalamika sana.

Waschana wenzangu wa sasa watu wazima wa baadae tusisubiri hadi hali kufikia hapa, kwani cancer ktk uanzaji wake sio tatizo hata kidogo na matibabu ni rahisi. Si kila uvimbe au maumivu ni cancer kwahyo uchunguzi wa wataalamu ni muhimu, uchunguz unafanyika ktk hospitali ya ocean road na ni bila malipo.

Social worker nimetimiza wajibu wangu kwa jamii (ethical standard; social workers' ethical responsibilities to the broader society ktk kipengele cha social welfare).

Nawapenda sana asubuhi njema!

Ujummbe huu umetolewa na mdau Wynne Vicent kupitia mtandao wa kijamii wa facebook

Views: 616

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on September 24, 2013 at 8:32

Ujumbe mzuri.. Chukueni hatua!!

Comment by Christer on September 19, 2013 at 17:11

Asante kwa ujumbe Wynne

Comment by Tulonge on September 18, 2013 at 18:31

Severin unaomba namba yake ya gari au nyumba?

Comment by Severin on September 18, 2013 at 18:26

Jamani mimi huo ujumbe hata sijauona. Mimi nilikua namtazama huyo mrembo aliyetoa ujumbe jinsi alivyo umbika. Macho yake mmeyaona?? Tulonge naomba namba yake kama unayo

Comment by Mama Malaika on September 18, 2013 at 9:34
Ni wazo zuri. Na kwa wale wenzangu walioko Mbamba Bay na kwingineko mbali kabisa yatakiwa campaign kubwa to raise awareness na ikiwezekana kuwepo vipimo kwenye hospitals za mikoa na sio Ocean Road Hospital pekee ambayo iko mbali na mwanamke wa Mbamba Bay au Kasulu.
Comment by Tulonge on September 17, 2013 at 23:17

Asante kwa ujumbe mzuri mdada

Comment by Belita on September 17, 2013 at 23:14

Ujumbe mzuri na mdada mrembo pia.Asante kwa kutustua

Comment by Joan on September 17, 2013 at 10:53

Asante kwa ushauri shosti

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*