Tulonge

Ukweli kuhusu maisha ya Gabriel na Christina kabla tukio la mauaji kutokea juzi


Kushoto ni marehemu Gabriel aliyetekeleza mauaji hayo, kulia ni Christina aliyekua mchumba wa Gabriel.
Juzi jumanne asubuhi hapa Dar es salaam kulitokea tukio la kutisha la mauaji na kuliacha jiji hili la Dare es salaam na maswali mengi na kila mtu kusema lake.Tukio hilo la kutisha liliikuta familia ya Alfred  na Hellen Newa katika nyumba yao iliyopo Ilala sharif Shamba.Familia hiyo ina watoto wanne Caroline Newa,Alpha Newa,Christina Newa,na Mlowi kaka yao.
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Gabriel Munishi (35) mkazi wa kitangiri Mwaza alifika katika nyumba hiyo na kufanya mauaji na kujeruhi kwa kutumia bastola

 
Wahanga wa mauaji hayo

Captain Francis Khianga Shumila raia wa Kenya na ni mume wa Caroline (amefariki) Alpha Alfred Newa(alifariki)


 Christina Nando Alfred Newa mpenzi wa zamani wa Gabriel(alijeruhiwa)

Hellen Newa mama yao mzazi(alijeruhiwa)


Gabriel Munishi  mkazi wa Kitangiri Mwanza mpenzi wa zamani wa Christina(alijiua baada ya kuua na kujeruhi)

 

Chanzo cha mauaji haya

Gabriel na Christina walikuwa ni wapenzi  Gabriel akiwa anaishi Mwanza maeneo ya kitangiri.Katika mapenzi hayo yalijaa ukatili na unyanyasaji ambao Christina alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana na Gabriel.Chanzo cha haya yote ni Gabriel kutokukubali kuachwa.

Mahusiano ya kimapenzi kati ya Gabriel Munishi na Christina Newa

Wawili hawa walikuwa wapenzi lakini mapenzi yaliyojaa mateso ya hali ya juu.Gabriel alikuwa akimtesa sana Christina kwa vipigo na vitisho vya bastola kuwa atamuua.Miezi miwili iliyopita Gabriel alikuwa amemfungia Christina ndani ya nyumba akimpa vipigo na akiwa hawezi kutoka nje.Tukio ambalo ilibidi ndugu zake watoke Dar es salaam mpaka Mwanza  na kuhusisha polisi Dar es salaam na polisi Mwanza kuomba msaada ilikumtoa ndugu yao ndani ya nyumba hiyo.Baada ya kufanikiwa kumtoa wakarudi Dar es salaam na Christina kusitisha uhusiano huo.Baada ya kufanya hivyo Gabriel akawa akitoa vitisho kwake akimwambia akimuacha ataiteketeza familia yake.
Kabla ya tukio Gabriel alikuwa akibembeleza sana Christina amrudie lakini Christina alimwambia apumzike kwanza kwa miezi mitatu na akamshauri atafute psychological help.Amekuwa akimuona ni mtu wa hasira kila wakati,vipigo visivyoisha na mbaya zaidi akimtishia kumuua mara kwa mara  kitu ambacho sio cha kawaida hivyo ni bora akamuone daktari.Akishapata msaada ndio atakuwa tayari kuwa nae tena ila kwa sasa amuache kwanza.
 

Siku ya tukio miezi miwili toka christina na Gabriel kuachana
Kabla ya tukio Gabriel alikuwa akifika mara kwa mara maeneo ya nyumbani hapo.Alikuwa akifikia katika hotel ya Double M anakaa juu gorofani na kuchunguza kila kinachoendelea kwenye nyumba yao.Maana ukiwa hotelini juu unauwezo wa kuona nyumbani kwao sababu ni pembeni tu ya hotel.

Siku ya tukio Christina alikuwa akisafiri kwenda syprus.Kwenye gari alikuwa akiendesha mume wa dada yao Caroline marehemu captain Fransis Shumila,pembeni alikaa mdogo wao Alpha ambae ni marehemu.Nyuma alikuwa amekaa Christina na mama yao mzazi.Wakiwa wanatoka nyumbani walikuwa wanaenda kumdrop Alpha kazini ambae alikuwa akifanya kazi Barclays bank,Christina akamalizie shopping zake za mwisho halafu wampeleke airport.Wakiwa wanatoka getini ndio Gabriel akatokea na bastola akafyatua risasi na kufanya mauaji ya Alpha na Fransis aliyefia hospital jana kisha kuwajeruhi mama yao mzazi pamoja na Christina.Alipomaliza aliona kashaua na yeye kujiua kwa kujipiga risasi.


Maelezo haya ni kwa mujibu wa dada yao Caroline Newa aliyezungumza na clouds fm leo.

Malalamiko ya Caroline kwa polisi
Caroline na familia wamesikitishwa na polisi kushindwa kuwapa ushirikiano.Baada ya kupokea vitisho kutoka kwa Gabriel kuwa atawauwa na kuteketeza familia nzima waliripoti polisi.Wanasema walishafika mpaka kwa CID Ilala kumueleza juu ya vitisho vilivyotolewa na Gabriel wakaomba wapewe hata RB lakini polisi waliwaona wazushi.Matokeo yake madhara yamekuja kutokea wakati polisi walikuwa na uwezo wa kutoa msaada kabla ya hili.Pia alielezea kwa familia ya Gabriel kushindwa kuwapa ushirikiano toka mwanzo wakiwajibu hayo ni mambo yao ya kimapenzi wao hayawahusu walivyokutana hawakuwepo.


< Marehemu Alpha na mumewe na watoto katika picha enzi za uhai wakeMarehemu kuzikwa Goba jumamosi hii shambani kwa mama yake ameacha mume na watoto wawili mmoja wao akiwa na miezi 6 tu.

Pole kwa familia zote zilizokumbwa na majanga haya Mungu awape wepesi wa kupita kwenye kipindi hiki kigumu.

Chanzo: dinamarios.blogspot.com

Views: 1587

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by habiba mustafa mlawa on November 25, 2013 at 9:25
sasa hussein mtu anamtishia kumuua mara kwa mara atamuachaje polepole, na kama anampenda kwa nn amnyanyase kwa nn amnyanyase, mnakera wanaume mbona sisi tukiachwa tunakubali matokeo wny nyiyi muue kama mtu unampenda hakuna basi sababu ya kumyanyasa bana
Comment by shij hussein mtebwa on November 24, 2013 at 11:40

nasema yule bwana hakuona raha kuachwa na mtu anae mpenda, nahao ndugu inaonekana walikuwa wanaunga maamuzi ya huyo dada, bira kujua jamaa anaumia kiasi gani nandio maana aliona wote wanausika kuvunja mausiano yao na kuwajumlisha wote, pia mapenzi hayana sheria kwani utamu wake  haufananishi na kitu nawashauli wakina dada mnapopata wapenzi wengine mume mnavunja mausiano polepole

nausikubali kumshabikia anemuacha mwenzie vinginevyo mtakuwa mnakalibisha matatizo na kulaumu jeshi la police je wangefanya nn? wangemuweka ndani siku zote?

Comment by CHA the Optimist on November 22, 2013 at 18:43

Bless Me God! CHA THE OMNISCIENT!

Comment by ANGELA JULIUS on November 22, 2013 at 14:59
Hussein mtebwa sijakuelewa hata kidogo unamaanisha nini.
Comment by shij hussein mtebwa on November 22, 2013 at 10:43

mm naamini yule bwana alikuwa anampenda sana huyo dada ndio maana hakuona raha mtu mwingine

achukue mzigo na hao waliokuwa naokwenye gali walitakiwa waamue mapema hayo ni mapenzi hata ungekuwa ni ww huyo aseme ukweli yy ndio wakulaumiwa mapenzi yake yanaingiza familia zote kwenye mateso.

Comment by shij hussein mtebwa on November 22, 2013 at 10:38

tatizo hawa wanawake wanaingia kwenye uhusiano halafu wanageuka bira kuona itakuwaje na kujidai

kuwa police watawasaidia badala ya kutatua wenyewe sasa hata faililingefunguliwa ingesaidia nn/

Comment by Tulonge on November 22, 2013 at 7:57

Hawa polisi wetu wanashangaza sana.Walishapewa taarifa mara kadhaa lkn hakuna hatua waliochukua.Ukiwauliza sababu ya kutofuatilia sijui watasemaje

Comment by ANGELA JULIUS on November 22, 2013 at 7:42

MH HURUMA SANA POLISI NAO NAPASWA KULAUMIWA KUMBE MTU ALIKUWA TAYARI AMESHATISHIA MARA NYINGI MH.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*