Tulonge

Usiku wa saa 7 mama huyu na wanae watatu wakiwa wamelala Feri DSM

Huu ulikua ni usiku mnene eneo la Feri umbande wa Magogoni DSM, nilimkuta mama huyu akiwa amelala ndani ya eneo ambalo abiria hukaa kusubiri kivuko. Mchana mama huyu na wanae watatu huonekana wakiomba hela ili kukidhi mahitaji yao.

Fikiria watoto hawa wanapata wakati mgumu kiasi gani. Wakati wenzao wakiwa wamelala kwenye vitanda vyenye magodoro mazuri, wao wamelala kwenye mabox tena bila chandarua. Yu wapi baba wa watoto hawa? Sikupata muda wa kumuuliza chochote mama huyu ili kujua mengi zaidi kuhusu maisha yake.

Views: 2033

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 9, 2013 at 11:23
Kaka Hassan Damnan kwa hakika umenena. Wanaume tabia hii ya kuzalisha na kutotunza watoto wao wako Mungu huwalaani. Na wanaume wa hivi wako wengi sana
Comment by hassan damnan on December 5, 2013 at 9:53

jamani sikupenda kwake mama huyu nadhani maisha ndiyo yamemzonga sana zaidi nalekeza lawama kwa sisi wanaume maana mzigo aliyonao mama huyu watoka kwetu tunajuwa kupachika mimba lakini mukikosana huwajui hata watoto wako wanaume tunadhalilisha watoto na kina mama tuwajibikeni sana au tutakuja pata shida ambazo huwezi kuzitatuwa na hizo shida ni madhambi ya kuwatesa malaika wa mola wetu lo jamani nampa pole huyu mama na kumwombea dua afanikiwe katika maisha ili awawke watoto wake mahali pazuri

Comment by Omary on December 5, 2013 at 8:10
Asante Mama Malaika. huyu Angela mpaka mwanawe aniletee mjukuu na Faisal ndio ataniheshimu lol
Comment by ANGELA JULIUS on December 5, 2013 at 7:52

kazi ni kwako Omary ha ha ha

Comment by Mama Malaika on December 4, 2013 at 23:46
Usiwe mashaka.. Omary! Najua ni utani tu, maana wewe na Dismas kwa utani wenu siwawez. Ha haa haa haaa
Comment by Omary on December 4, 2013 at 20:32
Doh! jamaniee niwieni radhi sikuwa na lengo wala nia ya kutukana nimekosea kwa bahati mbaya. pia Angela mie sijawahi kugusa kilevi chochote kwakuwa sijawahi kuona faida yake zaid ya hasara pia Mamangu alikuwa anawachukia sana walevi au wanjwaji so ningekunywa nami angenichukia sikuta niwe mbali na mzazi wangu kwaajili ya pombe.
kuhusu kujuwa bei mbona ni jambo dogo sana unaenda kama mteja na unauliza bei akikwambia buku 5 unamwambia una buku 2 atakataa basi unaondoka na jibu au ukiwa na swali jingine unaweza uliza sio lazima ubebe mzigo. Mr tulonge ukiona mtu kakosea hajakusudia kutukana una haki ya kuifuta kabla watu wengine hawajaiona ili kumlindia heshina yake watu wasimtowe maana akaonekana hana Adabu.
Kaka Daffa asante kwa kuniombea radhi wewe unanijuwa mdogoako sio mtu wa matusi.Nawapenda wote Amani kwenu.
Comment by Omary on December 4, 2013 at 20:10
Asante Mama kwa utetezi wako, ila bila shaka yule dada bado yupo ningependekeza aende mteja mmoja kati ya wanatulonge ili atuletee jibu sahihi ila inataka moyo maana mnaweza kuelewana ukamwambia bei ndogo ukitegemea atakataa na asikatae sijui utajiteteje? nawe hukuwa na nia ya kuchukuwa mzigo lazima uyakoge matusi kama sikosei Dis anamjuwa yule Mama tulipita wote siku 1 akasema anatamani kuongea na yule Dada sijui aliongea nae?
Comment by Mama Malaika on December 3, 2013 at 11:01
Ha haa haa .... Omary!! Nitakutetea kwa hiyo touch screen, ila kwa dada wa Aga Khan Hospital anayetoza buku 5 sijui buku 20 kwa penzi sitokutete. Ha haa haa haa haaa......
Comment by Omary on December 3, 2013 at 6:41
Hahahah jamani tatizo mwenzenu nilikuwa natumia cm ya tochi nilipo ondoka nilimuachia Dismas sasa natumia touch screen so kubadilisha mazingira ya utumiaji sio kazi ndogo, ila c mnaelewa bhana acheni fujo lol.
Comment by manka on December 2, 2013 at 15:56
Kweili watu mnachapia mwwee Omari umezidisha.

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*