Huu ulikua ni usiku mnene eneo la Feri umbande wa Magogoni DSM, nilimkuta mama huyu akiwa amelala ndani ya eneo ambalo abiria hukaa kusubiri kivuko. Mchana mama huyu na wanae watatu huonekana wakiomba hela ili kukidhi mahitaji yao.
Fikiria watoto hawa wanapata wakati mgumu kiasi gani. Wakati wenzao wakiwa wamelala kwenye vitanda vyenye magodoro mazuri, wao wamelala kwenye mabox tena bila chandarua. Yu wapi baba wa watoto hawa? Sikupata muda wa kumuuliza chochote mama huyu ili kujua mengi zaidi kuhusu maisha yake.
Add a Comment
Sasa Bw. Mjata naona wewe ndo umechapia mara nyingi kweli hahaahahaa.Hebu ona :-
mnaona hata mm kuna typing erro kwenye kumenti yangu hapo chini nikawida tatizo Omari mkono wake umeterezea paya
mnaona hata mm kuna typing erro kwenye kumenti yangu hapo chini nikawida tatizo Omari mkono wake umeterezea paya
kama ulimi hauna mfupa basi mkono wa mdogo wangu Omari hauna macho namuombea radhi kwa typing error mbaya kama hii. lakini mdogo wangu ulikuwa unawaza nini?
maana kwa kufanaya A kuwa U tu ndio imeleta mjadala, jamani wanatulonge tusije mtafsiri omari kuwa ndio ugonjwa wake mdogo wangu na mjua hana kabisa tabia hiyo.
Na wewe Tulonge mbona umekuwa mpekupeku? wote hatujoa hilo neno wewe umekuwa wakwanza kulina mhh!!!!!!!!! ????????????
He Tulonge hujui kuwa Omary siku hizi amekuwa mlevi? bora ulivomwambia.
@Omary huyo mama huwa namwonaga kumbe ndo hivo lol na umejuaje hadi bei zake inavoelekea na wewe ni mmoja wa wateja zake binuka inuka ukweli ndo huo lol nimekutoa dhamani mzee mwenzangu dhamani yako itarudi ukiniletea zawadi nzuriiiiii ile uliyoniahidi ya QUEN LATIFAH PAFYUME HA HA HA
Hahahhaa Omary chizi sana ww. Halafu type kwa makini, naona kuna sehemu umetukana.
Angalia neno linalofuata baada sentensi hii. Na hiyo shuka wameitowa wapi? na .....
nimekusoma anjela, na nikweli hawaonyeshi kama ni watu wa kutangatanga na mji kama tuliowazoea ambao asilimia kubwa huwa wachafu,kwa mtazamo mwingine nahisi inawezekana huyu mama na wanawe wanaishi kigamboni na hapo walikuwa wakisubiri usafiri ambao haukuwepo wakati wamefika na pengine ulichelewa sana na hakuwa na jinsi zaidi ya kutandika mabox na kuwalaza watoto,
nahisi lkn, yote yawezekana.
Poleni, hata sipati picha nikifikiria mbu wanavyo ng'ata.Yani utafikiri wanachoma na sindano ya viatu
Kila tunachokiona, kila tunachosikia, na kila tunachohisi ni lazima tukifanyie kazi kwa hatua.
Matumaini yangu ni kwamba kupitia picha hizi; kuna kitu ambacho kila mtu lazima awe amejifunza. Na tusibaki tu kuongea, bali tuende mbele zaidi ya kuongea.
Hawa ni Watanzania wenzetu; ambao wanastahili kuishi vizuri. Kusaidia au kumsaidia mtu haihitaji uwe na pesa nyingi kama Reginald Mengi wa Tanzania, au uwe na pesa nyingi kama Billgate wa America. Kutoa ni moyo, na wala si utajiri.
Blessed Is The Hand That Giveth--Than The One That Takeths.
Mwenye Masikio na Asikie, Mwenye Mdomo na Aseme na Mwenye Macho Aone!
PamoJah
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge