Huu ulikua ni usiku mnene eneo la Feri umbande wa Magogoni DSM, nilimkuta mama huyu akiwa amelala ndani ya eneo ambalo abiria hukaa kusubiri kivuko. Mchana mama huyu na wanae watatu huonekana wakiomba hela ili kukidhi mahitaji yao.
Fikiria watoto hawa wanapata wakati mgumu kiasi gani. Wakati wenzao wakiwa wamelala kwenye vitanda vyenye magodoro mazuri, wao wamelala kwenye mabox tena bila chandarua. Yu wapi baba wa watoto hawa? Sikupata muda wa kumuuliza chochote mama huyu ili kujua mengi zaidi kuhusu maisha yake.
Add a Comment
Ni kweli Mjata, huyu mama na familia yake anateseka sana kuliko kijijini kwao... lakini bado hatuwezi jua kilichomtoa kijijini, amekwepa balaa kubwa hadi akaona ni bora kutesekea kwingineko!
VERY SAD KIBELAA
Nimewaelewa, nitajitahidi kumtafuta halafu nitarudi tena kwenu
kweli inauma sana ila wewe uliyepiga picha hii inawezekana ulawa msaada sana wa wana jamii kuwapa msaada hawa ndg ,nakuomba weka no yako ya cm ili tuweze wafikia hawa wana jamii kwakuwapatia msaada veyema japo kimawazo au kipesa ,yawezekana baba wa familia yupo sehemu anapata starehe tu .
Frank my dear huyu mama wala si kwamba shuka kajifunika mwenyewe kawafunika hadi watoto wake sema huyu mdogo wa kati kalala vibaya si unaona mguu mmoja kauweka juu ya paja la mama yake ndo huyu wa mwisho kushoto hana shuka lote kalilalia huyu mdogo.
Pili watoto wanaonekana wana afya nzuri sana na pia ni wasafi si unaona wanaonekana wameoga kabisa hapo nampa huyu mama hongera ya usafi.
Tatu sitaki kuhukumu moja kwa zote kwani sina haki hiyo ni Mungu pekee ndo wakuhukumu sijajua hii familia chanzo cha wao kulala hapo ninachowaombea maisha yenye mafanikio katika kila walifanyalo kwa haki na kweli.
jamani kweli hawa ni watanzania na wanahaki yakuishi popote but this is too much.
mjni patamu lakini kwa mtindo huu bora kurudi village.
yah! hatujui undani wa wao kulala nje,ila kwa mtazamo wa harakaharaka huyu mama anawatesa watoto wake, kwanza yeye kajifunika shuka watoto wako wazi, pili arudi akalime tu.
Next time uliza ili tujue maisha yao kiundani
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge