Tulonge

Uso wa mwenyekiti wa chama cha madaktari ulivyo baada ya kupigwa na watu wasio julikana

Mwenyekiti wa chama cha madaktari Dk. Steven Ulimboka akihojiwa na Clouds TV baada ya kupigwa.

  • Kwa muda wa siku tatu nyuma alikuwa akipigiwa simu na watu hao.
  • Alipokutana na mmoja wao, mara walitokea wengine watano na kuwaambia wengine waondoke na abaki yeye (Steven)
  • Walimpiga sana, mateke na kwa kutumia kitako cha bunduki.
  • Walimfunga mdomo ili asipige kelele.
  • Alifikishwa hospital hana suruali, alikua na kamptula ya ndani na tshirt vilivyojaa damu.

 

Views: 747

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on June 28, 2012 at 19:38

Jemadari umetoa point nzuri sana. Tatizo wengi wetu hatutambui kuwa chanzo cha mgomo huu ni sirikali kutotatua matatizo. Tuamke jamani... mazingira ya kazi ya hawa watu yakiwa magumu ni hatari sio kwao doctors tu bali ni hatari kubwa kwa wagonjwa. 

Iwapo hao waliompiga walikuwa wamefiwa na ndugu zao kutokana na mgomo, ilipasa wajiulize kwa nini wabunge na viongozi wakiumwa wanakimbia kutibiwa south Africa au nje ya bara la Africa?

Comment by jemadari mimi on June 28, 2012 at 15:16

Kwanaza nachukua nafasi hii kutoa pole kwa DK ULIMBOKA kwa kile alichofanyiwa na watu inaosemekana hawajulikani.

ndugu zangu wanatulonge naona mnatoa mawazo yenu ktk pande mbili tofauti,kuna wale wanaona ni sawa kwa kufanyiwa kitendo hicho na wengine wanapinga ,mie binafsi sifurahi na wala siungi mkono kwa kupigwa dkt huyu.

Ninachotaka kusema kwa wale wanahemuona dkt huyu ni kikwazo wanakosea sana,kwani yeye ni msemaji tu wa chama chao.ni kama Nnauye ktk ccm ama ezekiel kamwaga ktk klabu ya simba,wao wanapokea toka kwa wahusika wengine na kwa nafasi yake anayatoa kwa vyombo vya habari,sasa sijui tatizo lake lipo wapi?

jamani tunapowalaumu madaktari kwamba wanaua ndugu zetu kwa sababu ya mgomo,tunakosea sana,kwani wao wanatambua ugumu wa maisha wa mtanzania na ndio maana wanapiga kelele sana serikali iboreshe mazingira ya utendaji wao ili uwe na manufaa kwetu tunawaona hawafai.

Bado sijaelewa tuna matatizo ngani ya kutokusema ukweli pindi unapoona utendewi haki,na ni kwanini tulaumu pale tunapoangukia na si pale tulipojikwaa,maana tunawalaumu madaktar  lkn mbona hatuigusi serikali ambao ndio wanapaswa kutekeleza yale yanayohusu afya ya mtanzania

Tumeona dkt ulimboka akipata kichapo kwa sababu ya msimamo wao,hivi najiuliza hawa walimu na wafanyakazi wa mashirika mbalimbali wanaotaka kugoma nao wafanyiwe kama ulimboka.maana tunatakiwa kutatua matatizo na si kuyapandikiza na kuongeza chuki na hasira kwa watendaji waliobaki juu ya serikali au wananchi

Comment by Christer on June 28, 2012 at 12:22

Pole sana Dokta, Mungu atakusaidia utapona

Comment by Abasi Mikidadi on June 28, 2012 at 7:16

Mi nahisi ni waliofiliwa na ndugu zao kutokana na Mgomo ndio waliofanya hivyo..

Comment by Mama Malaika on June 27, 2012 at 22:45

Au goodfellas walitaka kum-Kolimba nini? DISMAS please nakuomba utupe updates kuhusu huyu Doctor.

Comment by Gratious Kimberly on June 27, 2012 at 19:34

Duh noma hii......Hizi zote ni propaganda..!  Ilya poa sana....  kila penye mwanga ujue pana giza pia! Ndo maana kila anunuaye kiatu uangalia soli yake kabla ya kukikubali! Huo upande wa pili unaweza kuwa na sababu zake...Lakini ni kinyume na sheria pia na ni unyama kumfuata mtu mmoja eti kwa sababu ni chairman...labda anapigwa presha na wenzake ?

Comment by tulamvone mwenda on June 27, 2012 at 19:18
masikini mboka sasa kama kuna mgomo atatibiwaje? Labda aende private hosp. Pole sana ulimboka
Comment by ILYA on June 27, 2012 at 18:21

Hahaha,Shem Angela@: Duniani wawili wawili bwana,hata shilingi ina pande mbili,Hahahaha,

Enewei,kusema ukweli kitendo cha hao jamaa waliomteka Mheshimiwa Dakta Ulimboka, na kumtandika kihivyo ni kitendo kibaya sana,na hatuwezi kukipatia anuni sawia inayokwenda sawa na kitendo chenyewe ispokuwa  ujambazi !,maana wametumia mpaka bunduki katika kutoa maumivu hayo kwa Mheshimiwa huyo.

Hao jamaa waliomteka Daktari huyo na kumpiga hivyo, ikiwa kweli wana machungu kwanini wasiende kuwateka Mafisadi  ambao kazi yao kuu ni kuwaua watanzania kwa ufisadi wao wa kuminya mabilioni ya watanzania na kuwaacha solemba wakitaabika na hali mbaya ya kiuchumi huku wao wakisepa zao ulaya na kuhifadhi mabilioni hayo kwenye mabank ya pande hizo.!

Mimi nina mashaka hao majamaa waliomjeruhi huyo Daktari watakuwa ni washirika wa mafisadi !!.

Kama wamemchukia yeye na madaktari kwa kosa la kugoma,basi naweza kusema chuki zao ilitakiwa wazielekeze kwa mafisadi,maana Madaktari kugoma kwao ni mojawapo ya madhara ya mifisadi hiyo, miradi ya maendeleo haifanikishwi inavyotakiwa, watumishi hawalipwi vilivyo kwa sababu mifisadi wamechota fedha za umma.

Daktari huyu kapata maumivu bure,hayo maumivu hayakuwa maumivu yake,hiyo message ilitakiwa itumwe kwa mafisadi wanaosababisha madaktari na wafanyakazi wengine kugoma kutokana na wao kula pesa za umma ambazo zingelitumika kuwaongezea mishahara yao ili wafanye kazi katika misingi inayotakiwa.

So naweza kusema: wameandika message safi,lakini katika kuItuma wakakosea namba,na hayo ndio matatizo yenyewe ya "Wrong Number" !!

Comment by Mama Malaika on June 27, 2012 at 18:08

Duh! Yaani Tanzania imfikia hivi? Sina la kusema...

Comment by ANGELA JULIUS on June 27, 2012 at 17:39

EBOO IL YA SEMA MOJA NDUGU.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*