Tulonge

Uso wa mwenyekiti wa chama cha madaktari ulivyo baada ya kupigwa na watu wasio julikana

Mwenyekiti wa chama cha madaktari Dk. Steven Ulimboka akihojiwa na Clouds TV baada ya kupigwa.

  • Kwa muda wa siku tatu nyuma alikuwa akipigiwa simu na watu hao.
  • Alipokutana na mmoja wao, mara walitokea wengine watano na kuwaambia wengine waondoke na abaki yeye (Steven)
  • Walimpiga sana, mateke na kwa kutumia kitako cha bunduki.
  • Walimfunga mdomo ili asipige kelele.
  • Alifikishwa hospital hana suruali, alikua na kamptula ya ndani na tshirt vilivyojaa damu.

 

Views: 597

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on June 27, 2012 at 17:27

Ingawa ni kosa kubwa sanakumtandika na ni kinyume cha sheria bali ni kinyume na haki za binadamu na ni unyama mkubwa waliomtendea ,lakini nikigeuza upande wa pili wa shilingi yangu naona kwamba wacha wamtandike!! hilo ni soma kwa madaktari wengine,na ukizingatia huyu ni mwenyeketi wa madaktari wagomaji!.Hiyo kule Bongo wanaita:

Message sent !.

Tujiulize hao madaktari kugoma kwao kumesababisha vifo vya watu wangapi! watu wengi wamekufa kutokana na migomo yao,wanajali maslahi yao,wanajali matumbo yao,na kuwasusia wagonjwa,wagonjwa wanataabika na hatimae kufa kw akukosa huduma,madaktari wako kwenye migomo ati wanadai kuongezewa fedha katika mishahara yao,wanajali fedha kuliko maisha ya wagonjwa,wajiulize katika hiyo migomo yao ni wangapi wameathirika na migomo yao hiyo,na hata kupoteza maisha yao.?! Ndio ni kinyume na haki za binadamu kumtandika namna hiyo lakini haki za binadamu pia anastahili kuzipata mgonjwa,hivyo ikiwa madaktari wanataka watendewa haki za biunadamu inabidi nao wawe tayari kuzitenda kwa watu hasa wagonjwa mahospitalini. Muhimbili imeshuhudia waziwazi madktari wakiwasusia wagonjwa,na wengi wamekufa kwa kukosa matibabu kutokana na hiyo migomo.!

Sasa ikiwa migomo hiyo wanayoifanya ni sahihi,wafanye basi na mgomo kwa mwenyekiti huyu aliyebongonyolewa midomo,wasimtibu mpaka serikali ijibu matakwa yao!,si migomo ni mizuri,kwanini huyu mwenyeketi anapelekwa huko hospitali,anataka atibiwe na nani wakati madaktari wako katika kipindi cha kuonyesdha uwezowao wa kuwasusia wagonjwa na kuwaadhibi kw akosa lisilokuwa wao!.wananiudhi sana madaktari hao wanaogoma,na huenda hao waliomtandika huyo mwenyekiti wa madaktari ni miongoni mwa wale ambao wameathirika na kupoteza ndugu zao wagonjwa huko mahospitalini (Muhimbili),watu wanahasira wewe!unacheza nini!

Enewei,binafsisiungi mkono kitendo hichi alichofanyiwa huyo mheshimiwa,lakini pia siungi mkono tabia yao ya kugoma na kuwasusia wagonjwa coz wagonjwa wanaonewa tuuuuuuu hwana kosa lolote,wanahitaji huduma ya huko mahospitalini na wanawategemea sana wauguzi na madokta.ni mbaya sana kugoma na kuwaacha vitandani wakitaabika pasina kupewa huduma ya kiafya.NUKTA.

Comment by ANGELA JULIUS on June 27, 2012 at 16:46

dah, nimelia sana lol na nimekilaani kitendo hiki sana, Police wafanye uchunguzi wa kina naimani wahusika watapatikana tuu na first suspect lazima wafanyiwe gwaride la utambulisho labda Dk anaweza watambua.

Comment by wankuru masswe on June 27, 2012 at 16:39

Comment by Omary on June 27, 2012 at 16:38

doh! hii Tz inapoelekea siko watu wanafikia kulipiza kisahoi kiasi hiki? hii mbona sio tamaduni zetu! watu wanatoa wapi?! roho hizi mbaya.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*