Tulonge

Video: Kijana wa Kihindi (House Boy) akipokea kile kipigo cha Nyoka aliyeingia ndani ya nyumba!!

Kutumia maguvu,ukali katika kuadabisha mwanao au kijana uliyemuajiri ,naweza kusema tena kwa kujiami kuwa sio kitu cha kujifakharisha wala kujivunia.Katika sehemu ifuatayo ni link ikionyesha kijana wa kihindi (Mfanyakazi katika familia hiyo) akipokea kipigo kikali kutoka kwa waajiri wake wa kiarabu.Mdau,naomba kwanza ukandamize LINK HII utizame kwanza video yenyewe jinsi kijana anavyoendelea kupokea  vibao na kukabidhiwa maumivu  zikiwemo  ngumi za Kick Boxer, kisha rudi ili uendelee kusoma gazeti langu.

http://www.rasheed-b.com/2008/02/08/video-indian-man-severely-beate...

Kipigo kama hicho hukipata nyoka aliyekosea njia na kuingia nyumabani kwa mtu.Sijui kwanini wanandugu hawa wameamua kutumia njia hiyo kumuadhibu kijana huyu ikiwa ni sehemu ya kumuadabisha.Kwanza kabisa nieleweke hapa kwamba mimi na si mimi bali walio wengi wako dhidi ya kitu kinachoitwa kupiga au kutesa au kuadhibu pindi mwanafamilia au mwanao anapokuwa kafanya kosa.

Lakini kwa upande wa pili naweza kusema tunatakiwa kuangalia aina ya kosa.Kuna wakati mwingine mzazi au mlezi utahitaji kutumia kichapo lakini si kwa kila kosa bali kwa makosa kama yale yenye uzito kilo mia.Mfano:

Ikiwa itabainika kuwa ( kijana huyu wa kihindi) kafanya kitendo kisichoashiria kuwa na tabia nzuri dhidi ya watoto wa familia,basi hapo hutakuwa na njia nyingine ya kumuadabisha tofauti na kutumia nguvu kama kumchapa maana mwanadamu inatakaiwa heshima yake kutunza na heshima ya wanawe wa familia au heshima ya familia yake kwa ujumla.

Lakini kama itabainika kuwa kosa alilolitenda (kijana huyo wa Kihindi) ni la ina nyingine kabisa lisiloshusha heshima ya mwanadamu mwenzie kama vile (kuiba,kufanya udanganyifu ...na makosa mengine kama hayo ambayo yana uzito hafivu) hapo kuna uwezekano bali inatakiwa kutumia njia nyingine za kumuadabisha na kuepukana na njia za kumpiga ,kumtesa na kumnasa vibao vizito kama vile vya Mr:Big-Show mcheza mieleka wa WWE kwa wale wenye kufuatilia mchezo huu.

Kusema ukweli dini zote za Mbinguni zinatufundisha kuwa na huruma,kuwa wapole na wema kwa wanetu na kwa watu wote,hazitufundishi kutumia maguvu mazito katika kurekebisha tabia za watoto wetu pindi wanapokosea,au wafanyakazi wetu pindi wanapokosea,hazitufundishi pia kulipizana visasi kwa wasaidizi wetu nyumbani (wafanya kazi) ,na kuwaonyesha umgambo katika suala zima la kuwalea au kuwalekebisha kama wafanyavyo mgambo wa city.

Dini zinatufunza upole zaidi na huruma zaidi na kwamba tunatakiwa kutumia njia salama na nyepesi kurekebisha ambazo zitamfanya mtoto wako au mfanya kazi wako kujirudi na kukuona wewe ni The Best father/Mother in the world, au The Best Employer in the World.

Katika viumbe ambao historia imewatambua kwa kuwa na jeuri,kiburi,uovu na unyambisi,ni Fir'aun wa Misri.Fir'aun si kwamba alikuwa jeuri tu bali pia alifikia hatua ya kujiita yeye ni Mungu wa viumbe na kuwataka watu wote wasikilize na kutenda amri zake.Fir'aun huyu alimkosea sana Mwenyeezi Mungu (s.w) Muumba kwa kufikia hatua hiyo ya kujitangaza kuwa yeye ni Mungu.Lakini cha ajabu Mwenyeezi Mungu alikabiliana nae kwa upole na huruma ili kurekebisha tabia yake.

Hivyo ndivyo historia ilivyothibitisha.

Mwenyezi Mungu anatusmulia katika Qur'an kuhusu yaliyojiri kati ya Fir'aun na Nabii Musa.

Historia inasema:

Pindi Mwenyeezi Mungu (s.w) alipomtuma Nabii Musa (a.s) na Nduguye Harun (a.s) wamuendee Fir'aun alisema kwa kuwambia (Yaani Nabii Musa -a.s- na Nduguye Harun -a.s-):

"Nendeni kwa Fir'aun kwa hakika Fir'aun amevuka mipaka,na mzungumze naye kwa kauli laini huenda (kupitia kauli hiyo laini) atashika mawaidha au ataogopa".(20:43-44.)

Fir'aun zama hizo alikuwa mbabe,anatisha,anaogopwa,mpaka Nabii Musa na Harun (a.s) walikuwa wakimuogopa kutoka na ujeuri wake.

Wakamwambia Mwenyeezi baada ya kuwapa kazi hiyo ya kumuendea mbabe huyo:

Ewe Mola wetu!,Hakika sisi tunaogopa asije kutufanyia matata au kutudhulumu".(20:45).

Mwenyeezi Mungu (s.w) akawajibu kwa kuwambia: Msiogope,bila shaka mimi niko pamoja nanyi,nasikia na naona.":(20:46).

Kisha Mola akawambia:

"Basi mwendeeni na mwambieni:Kwa hakika sisi ni Mitume wa Mola wako,kwa hiyo wapeleke pamoja nasi wana wa Israel na "usiwaadhibu".Hakika tumekuletea mujiza utokao kwa Mola wako,na amani iwe juu ya anayefuata muongozo."(20:47).

Walipofika mbele ya Fir'aun na kumfikishia ujumbe kutoka kwa Mola wake,Fir'aun akaanza kuonyesha ugaidi wake na ujeuri wake kwa kuwauliza:

"Mola wenu ni niani ewe Musa?":(20:49).

Musa (a.s) akasema:

"Mola wetu ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake kisha akaongoza":(20:50)

Kisha Musa akaendelea kumtajia sifa za Mwenyeezi Mungu kuwa ndiye aliyekufanyieni ardhi kuwa tandiko,na akakuwekeeni humo njia,na akayateremsha maji kutoka mawinguni,na tukaotesha kupitia hayo maji mimea yetu mbali mbali,kisha akasema kuleni na walisheni wanyama wenu,bila shaka katika hayo kuna dalili kwa wenye akili.

Musa (a.s) akaendele kumuweke wazi Fir'aun kwa kusema kuwa Mwenyeezi Mungu ambaye ni Mola wangu anasema:

"Katika (Ardhi) hiyo tumekuumbeni,na humo tutakurudisheni,n akutoka humo tutakutoeni kwa mara nyingine." (20: 53-56)

Fir'aun alionyeshwa kila dalili na miujiza yote lakini alikadhibisha na kukataa,akawa akizidi kuleta jeuri mbele ya Musa na Harun (a.s) huku akimtuhumu Musa na kumuita mchawi.

"Fir'aun alimuuliza Musa (a.s):Umetujia kututoa katika nchi yetu kwa uchawi wako ewe Musa?" (20:57)

Akamwambia ikiwa umekuja na uchawi wako:

"Basi sisi tutakuletea uchawi kama huo,kwa hiyo (unatakiwa) ufanye ahadi ya mkutano baina yetu na yako ambayo hatutakiwi tuivunje sisi wala wewe(katika) mahala patakapokuwa sawa." (20:58).

Musa (a.s) akakubaliana na wazo hilo na akamwambia, ewe Fir'aun:

"Miadi yenu ni siku ya mapambo na watu wakusanywe asubuhi." (20:59).

Basi hapo Fir'aun akatoka mbio kwenda kukusanya hila zake,akafanikiwa kukusanya hila zake kisha akaja akiwa na group kubwa la wachawi wake waliobobea katika sekta ya uchawi waongo kupindukia.

"Musa akawambia:Ole wenu!, Msizushe uongo juu ya Mwenyeezi Mungu,asije akakufuteni kwa adhabu,na amekwisha shindwa anayezua uongo." (20;61).

"Basi wachawi wale (baada ya kupokea onyo hilo) wakazozana kwa shauri lao wenyewe na wakanong'onezana kwa siri." (20:62).

"(Kisha) wakasema:Hakika hawa wawili (yaani Musa na Harun) ni wachawi ,wanataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wao,nakuondoa desturi yenu iliyobora kabisa." (20:63).

Musa akawambia:

"Kwa hiyo kusanyeni hila zenu,kisha mfike kwa kujipanga safu na kwa hakika amefuzu leo atakayeshinda".(20:64.)

wachawi wale walikijiamini na uchawi wao wakijipa moyo kuwa ndio watakaotoka kidedea mbele ya miujiza na Nabi Musa (a.s).wakawa wanajiuliza waanze wao kuonyesha mbwembwe za kutupa uchawi wao uwanjani au wasubiri anze Musa.

Wakamuuliza Nabii Musa (a.s):

"Ewe Musa!, Je:wewe utatupa au tutakuwa sisi wa kwanza kutupa?":(20:65).

Musa akawambia waanze kutupa kwa kusema:

"Bali tupeni!,(wakaanza kutupa miuchawi yao ya uongo) Mara kamba zao na fimbo zao (hizo) zikaonekana mbele yake (Musa), (ikiwa ni sehemu ya) uchawi wao zikienda mbio." (20:66).


"Basi Musa akawa na khofu katika nafsi yake (baada ya kuona uchawi huo)".20:67).

Mwenyeezi Mungu (s.w) anatusimulia katika Qur'an Tukufu alivyomwambia Musa baada ya uchawi wao kuwa mbele yake namna hii:

"Tukamwambia (Musa): Usiopgope,hakika wewe ndiye mwenye kushinda." (20:68.)

Wakamaliza wachawi wale kuonyesha uchawi wao mbele ya Nabii Musa na Harun (a.s).Ikafika sasa zamu ya Nabi Musa kuonyesha uwezo wa kimiujiza kwa Nguvu za Mola wake Muumba.

Nabi Musa (a.s) alikuwa siku zote akitembea na fimbo yake ambayo alikuwa akichungia Kondoa na kuitumia kwa kazi zingine,siku hiyo katika uwanja ule ambako zoezi la kuonyesha uwezo wa uchawi lilikuwa likiendelea pia alikuwa na fimbo yake hiyo kama kawaida katika mkono wake wa kulia.

Na sasa ni zamu yake kuonyesha mioujiza mbele ya watu wale wa Fir'aun ambao uchawi wao au vinyoka vyao walivyovitengeneza baada ya kurusha kamba na fimbo zao uwanjani vilikuwa vikizidi kwenda huku na kule mahala pale vikitamba na kutishia na kuwapa jeuri wachawi wale na Fir'aun wao.

Mwenyeezi Mungu (s.w) msimulizi wa kisa hicho ndani ya Qur'an Tukufu anatwambia kuwa alimwambia Musa (a.s):

"Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia kitavimeza walivyovitengeneza,hakika wametengeneza hila za mchawi,wala mchawi hatafaulu popote afikapo".(20:69.).

Musa akafanya hivyo kama alivyoelekezwa na Mola wake,mara fimbo yake hiyo ikageuka kuwa bonge la chatu,ikavimeza vinyoka na viuchawi vyao vyote pale uwanjani.Wachawi wale wakaogoapa sana baada ya kuona Fimbo ya Musa inaonyesha maajabu kwa kumeza meza uchawi wao wote.Wakakubali kwa hakika wameshindwa.

"Basi (hapo) wachawi (hao) wakaangushwa kusujudu,wakasema: Tumemwamini Mola wa Harun na Musa." (20: 70).

Baada ya wachawi hao kuonyesha utii kwa kukubali kwa kusema hakika sisi tumemwamini Mungu wa Harun na Musa;

"Fir'aun akasema (akiwambia wachawi wake): Jee,Mnamwamini (Musa)kabla sijakupeni ruhusa!.Bila shaka yeye ndiye mkubwa wenu aliyekufunzeni uchawi.Kwa hiyo,hakika nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha (yaani kukata mkono wa kulia kwa mguu wa kushoto au mguu wa kulia kwa mkono wa kushoto) na lazima nitakusulubuni katika mashina ya mitende,na bila shaka mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na (mwenye) kuiendeleza (adhabu yake)." (20:71).

Wachawi wale waliamini kabisa, na baada ya kuwafikia hoja zilizowazi na hila zao kufeli hawakuwa tena na shaka na hoja za Musa (a.s) zilizo wazi.Hilo liliwafanya wasiogope vitisho vya Fir'aun,wakamwambia Fir'aun:

"Hatukutangulizi kabisa juu ya hoja wazi wazi zilizotufikia na (hatukutangulizi) kuliko yule aliyetuumba,basi fanya unavyotaka kufanya,(lakini ujue kwamba) unaweza kutoa hukumu inayohusiana na maisha haya ya dunia tu." (20: 72.)

"Kwa hakika tumemwamini Mola wetu ili atusamehe makosa yetu na uchawi uliotulazimisha kuufanya,na Mwenyeezi Mungu ndiye bora na wa kudumu." (20:73).

Hivyo ndivyo Fir'aun alivyoshindwa baada ya kukusanya hila zake,lakini akazidi kuwa jeuri na kutokubali kushindwa.Baadhi ya watu wake wakamuasi na kukubali ujumbe wa Nabii Musa,lakini wangine wakazidi kuwa pamoja na Fir'aun.Fir'aun akawapoteza watu wake na kwa hakika hakuwasaidia chochote.

Mwishowe Mwenyeezi Mungu (s.w) akamuangamiza Fir'aun na majeshi yake katika bahari.

Kisha Mwenyeezi Mungu (s.w) akaamua kumfanya Fir'aun awe ni sababu ya mazingatio kwa vizazi vijavyo vya kina sisi na watakao kuja baada yetu kwa kuubakisha mwili mwake.Hakuzikwa Fir'aun na mwili wake hauozi bali upo hadi leo hii,watu mbali mbali wanaosafiri kwenda Misri kwa ajili ya kuutazama mwili huu hubahatika kutazama ukiwa sehemu yake uliko hifadhiwa.

Alikuwa Fir'aun mwenye maguvu,anamiliki kila watu,mfalme,anafanya anachotaka katika ardhi hii ya Mwenyeezi Mungu (s.w),akimwaga damu za wanadamu,akifanya kila aina ya ufisadi katika ardhi hii,si hayo hayo bali kiburi chake kilifikia hatua ya yeye kujiita Mungu na kuwatangazia watu kuwa Yeye ndiye Mungu wao,lakini pamoja na jeuri hiyo historia imeshuhudia mwisho wake unakuwa mbaya,bada ya kukutana na amadhabu ya MOla Muumba.Na leo hii abebaki kuwa dhalili na kiwili wili chake kikiwa mfano wa mazingatio kwa wale watala wenye kufuata nyayo zake.

Watafanikiwa kukwepa adhabu za Mungu (s.w) wale tu watakao kuwa na mazingatio na visa kama hivi ambavyo Mwenyeezi Mungu (s.w) anatusimulia katika vitabu vyake vitukufu ikiwa si kwa lengo lolote ispokuwa kutukumbusha na kututaka tuzingatie.

Huyo ndiye aliyekuwa Fir'aun muovu kupindukia,lakini pamoja na uovu wake tumeona Mwenyeezi Mungu (s.w) anamtaka Nabii Musa (a.s) na Nduguye Harun (a.s) wamuendee na kuzungumza nae kwa lugha ya upole,kwa kauli laini,akisema huenda atakuwa na mazingatio kwa kusikia mawaidha au kuogopa.

Hivi ndivyo tunavyotakiwa kuwa wapole katika kauli zetu kuelekea waliofanya makosa ili kuweza kuwarekebisha,tusitumie maguvu na kauli za ukali,kwa hiyo si njia bora ya kujenga bali hubomoa na kumfanya mtu asifikie malengo yake ya kumjenga mtoto awe na tabia nzuri.

Laiti wazazi hawa ambao binafsi siamini kama ni wazazi wake bali waajiri wake wa kiarabu hasa ukifuatilia mazungumzo yao yanavyosika kwa video wangelizingatia mafunzo kama haya na kusoma visa vizuri kam hivi,basi wangejizolea mafunzo mengi sana kutoka ndani ya visa hivi,na wasinge changua njia hii ya kumjenga kitabia au kumuadabisha kijana huyo wa kihindi kwa kumpiga kipigo hicho kiumizacho tena kwa kuchanganya  na 'Kick Boxer' kama video hii inavyoonyesha kwenye link hii ifuatayo:

http://www.rasheed-b.com/2008/02/08/video-indian-man-severely-beate...


Na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 2057

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on January 30, 2012 at 10:41

Asante kwa mistari na mafunzo ya Muumba wetu.. Hivi vyote ni vitendo vya unyanyasaji.. Ndiyo maana kwenye ile article ya wakenya wanavyo nyanyaswa nilisema "nyumbani ni nyumbani hata kama niaje" Mi nakwambia kama ingekuwa ni mimi basi bora waniue tu.. maana hapo nitawapiga kata za kutosha alafu narudi zangu nyumbani hata kama nakula ugali na chumvi.. ebo.. yani wamenipa hasira hao waarabu!!!

Comment by Alfan Mlali on January 28, 2012 at 20:05

hahahahahahah! Hiyo nimeipenda mkuu ILYA..mshahara kwa makonzi..tehtehetehet

Comment by ILYA on January 28, 2012 at 19:41

Brother Alfan unapenda kazi au !,Yani bosi wako akikukabidhi manundu unasema na wewe lazima ujibu,hapoi sasa utetema kazi maana hata bosi huyo anajua huwezi kureply coz kibaru kitaota nyasi.Kijana huyu ni wa kihindi na inaonekana kwao alikotoka kuna Hard Life maana kama ni mimi ukinitwanga namna ile nakutolea uvivu kisha natambaa zangu home.Kwani kazi mpaka nifanye kwako tu na mpaka nifanye kazi hiyo tu,kuna kazi kibao bwana.Waarabu hao wanaompiga kijana huyu ni wabaya sana na hawana utu.Mara nyingi waarabu hawa wa maeneo hayo huwatesa sana wafanyakazi wao,na hii ni tabia mbaya sana.Natamani siku moja aje muarabu kwenye shirika langu la kutengeneza ubuyu kuomba kazi,kila mshahara atakuwa anaupokea kwa makonzi.

Comment by Tulonge on January 28, 2012 at 19:27

Duuh! watu wana roho ngumu aisee.Ishu ya kupiga mtu huwa ni ngumu sana kwangu. Ila ukinikera sana lazima nikuonje kidogo.

Comment by Alfan Mlali on January 28, 2012 at 19:08

Sijasoma maelezo yote maana ni marefu sana.. Video nimeiangalia ila ninachojiuliza hujo kijana anayepigwa kwanini kakubali kupigwa kiasi kile bila kujitetea??? Mimi huwezi kunipiga vile hata kama mko 10 lazima na mimi niwatwange kidogo!!!

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*