Tulonge

Video: Mashuduha waelezea tukio la Majambazi kupora fedha Benki ya Habib African Kariakoo leo

Majambazi wapatao saba akiwemo mmoja alivaa sare za jeshi la polisi Tanzania wamepora mamilioni ya fedha zikiwemo dola za marekani 181,885 katika benki ya Habibu African Bank iliyopo mtaa wa Livingistone na Uhuru Karikaoo Jijini Dar es salaam na kutokomea kusikojulikana.

 

Itv ilifika katika benki ya Habibu African Bank Ltd iliyopo mtaa wa livingstone kariakoo jijini dar es salaam muda mfupi baada ya tukio hilo kufanyika ambapo baadhi ya watumishi wa benki walizuia vyombo vya habari kupata maelezo yao juu ya tukio hilo kwa kufunga milango huku wakidai kuwa maafisa wa jeshi la polisi tayari wapo ndani ya benki hiyo kuchunguza tukio hilo iliyogubikwa na utata baada ya kuonekana kwa mmoja wa majambazi alivaa sare za jeshi la polisi kama wanavyoeleza mashuhuda wenyewe

 

Kutokana na tukio hilo kugubikwa na utata baada ya mmoja wa majambazi hao kuvaa sare za jeshi la polisi,baadhi ya mashuhuda wameomba serikali kupitia jeshi hilo kuchunguza wanaohusika kufanya uhalifu kwa kutumia sare za jeshi la polisi jambo ambalo linasababisha maswali mengi katika jamii huku gari aina ya Noah yenye namba za usajili T817 rangi ya fedha ikitajwa kutumika katika tukio hilo.
Baada ya tukio kutokea,kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam CP Suleman kova,alilazimika kuingiza vijana wake kazini haraka kufanya msako mkali dhidi ya majambazi hao ambapo kwa uchunguzi wa awali ya jeshi la polisi limekiri kuwa majambazi hao wapatao saba walisindikizwa na askari wa jeshi la polisi kufanya tukio hilo ambalo lilifanywa kimya kimya na majambazi hao wakiwa na silaha huku ikionekana kuwa taarifa za kufanikisha kwa tukio hilo inaonekana ilitolewa na baadhi ya watumishi wa benki hiyo kwa mujibu wa Kamishna Kova ambaye ametangaza donge nono la shilingi milioni mia moja za kitanzania kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao.

 

Chanzo: ITV

Views: 251

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on August 30, 2013 at 14:58

polisi waliokua wanalinda bank walikuwa wapi? dili za nchi hii haziwezi kuisha

Comment by David Edson Mayanga on August 30, 2013 at 13:10

HAPO YAONEKANA TU WATUMISHI WA BANK NA POLISI WASHIRIKIANA KWA UKARIBU ZAIDI KTK ZOEZI HILI KULINGANA NA MAELEZO HAPO JUU. ILA USHAURINIKWAMBA TUWE WAVUMILIFU KTK TUKIO HILI KWANI SERIKARI YETU INAMKONO MREFU NAKWAKUWA WAMESHIRKIANA NAPOLISI TUTAPATJIBU TU KUWA WAMEKAMATWA KWANI WATAKWENDA HUKO KTK MGOWO WTAZUNGUKANA NA NDIPO SIRI ZITAANZAN FICHUKA HATA KAMA IKAPITA MWEZI.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*