Wabunge 47 toka vyama tofauti vya siasa wameamua kujiunga na JKT (Jeshi la Kujenga Taifa) kwa ajili ya mafunzo na uzalendo kwa taifa. Baadhi ya wabunge hao ni David Kafulila (NCCR-Mageuzi), Zitto Kabwe (CHADEMA), Halima Mdee (CHADEMA), Freeman Mbowe (CHADEMA), Abdulkarim Shaha (CCM), Esther Bulaya (CCM), Twaida Galusi (CCM), Neema Hemed (CCM), Ezekiel Wenje (CHADEMA), Joshua Nassari (CHADEMA), Raya Ibrahim (CHADEMA), Godbless Lema (CHADEMA) na Nyambari Nyangwine (CCM).
Watahimili vishindo?
Add a Comment
uzalendo haujengwi jkt hasa wanajifunza kujihami fujo wakati wa uchaguzi na maandamano. mbona kuna viongozi kibao wameenda jkt na bado mafisadi
mje na maofisini tupo wengi tu ambao tuliikosa JKT tunahitaji kwenda na kumuenzi baba wa taifa kwa vitendo.
Sipati picha Mbowe akiambiwa "chuchumaa chin". Au aloweshwe maji
Najua MAkamanda wa M4C Watatoboa tu!!! Tumeisha zoea purukushani.. hahahaa
Nawatakia mafunzo mema, ila msije mkatoroka siku ya kwanza. Maana huko hakuna viti vya kuzunguka kama Bungeni
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge