Tulonge

Wabunge wa Tanzania wajiongezea marupurupu

Kumekuwa na ghadhabu nchini Tanzania kufuatia uamuzi wa wabunge kujiongeza maelfu ya dola kama marupurupu.

Pesa hizo wanasema ni mkono wa kwaheri.

Marupurupu hayo yatatolewa kwa kila mbunge wa bunge la Tanzania lenye wabunge 357 wakati watakapokamilisha muhula wao wa tano kama wabunge.

Kila mbunge nchini Tanzania, hupokea mshahara wa dola elfu saba kila mwezi.

Wakazi wa mji mkuu Dar es Salaam waliambia BBC kuwa wameshtushwa sana na marupurupu hayo hasa baada ya kuambiwa na serikali kuwa hakuna pesa za kutosha kwa matumizi ya huduma za jamii.

Chanzo: BBC Swahili

Views: 552

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on February 7, 2014 at 15:57
Viongozi/wabunge wanasahau kuwa uongozi ni kujitolea na sio kujilimbikizia mali kwa kuwa nyonya walipa kodi. Viongozi wamejaa "u-mimi" na sio "u-sisi".
Comment by Dixon Kaishozi on February 4, 2014 at 8:58

Mi nashangaa viongozi wanavyosema nchi yetu ni maskini na haina pesa!! hainiingii akilini kabisaa!! Hili bunge la katiba mwanzo lilikua na wajumbe 375.. nasikia tena wameongezeka wengina 201.. na kufanya jumla ya wajumbe 576. ambao kama kikao kikienda vizuri kitakaa kwa muda wa siku 90 au nazaidi kama hoja zitapingana sana. Mimi siyo mtaalamu wa mahesabu ila za kuuzia genge nazijua!! 

Hebu tuache gharama zingine za kila siku za majukumu ya serikali ambazo zinaendelea kama kawaida alafu tuangalie hili la kikao cha katiba tu..

Kila mjumbe alipwe 1,100,000 kwa siku, alafu zidisha mara hao wajumbe 576... unapata 633,600,000 TSH. hiyo pesa ya siku moja!! alafu hiyo jumla tuzidishe tena mara hizo siku 90 unapata 57,024,000,000 TSH. 

Hii ni nchi ya asali na matunda.. watu wanakula na kujiachia huku huduma muhimu zikiwa zinasuasua.. Hii inatia hasira sana!!!

Comment by Omary on February 1, 2014 at 8:14
hao wa dola elfu 7 kwa mwezi wanaafadhali nenda mwanahalisiforums kisha ingia kwenye siasa page ya 13/14 utaona bunge lakatiba wizi mtupu mtu anapewa 1,100,000 kwa siku.
Comment by maembe79 on February 1, 2014 at 4:19

huu mtindo huuthi kwani wao huepuka majukumu waliopewa na wananchi wao, kwani hata hapa  mtindo ni ule ule,magari makuwa maisha ya kifahari, ilhali waliowachagua wanahangaika kule vijijini,vitongojini..aaii..wambungeee...AIBU!!

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*