Tulonge

TUKIO la kusikitisha limetokea hivi karibuni katika Kijiji cha Wenda, Kitongoji cha Lupeta, mkoani Iringa kwani umekutwa mwili wa mwanakijiji aliyetambulika kwa jina la Leonard Kutika (49) ukiwa umechunwa ngozi, hivyo kuvuta hisia kuwa wachuna ngozi wameibuka upya.

Licha ya kuchunwa ngozi, marehemu alikuwa amenyofolewa macho pamoja na kukatwa sehemu zake za siri.

Akizungumza , baba mdogo wa marehemu Leonard, Martin Kutika mkazi wa Lupeta alikuwa na haya ya kusema: 
“ Siku ya tukio nilipigiwa simu usiku na ndugu yetu aitwaye Kibadeni aliyesema kuwa Leonard alikuwa akisumbuliwa na tatizo la akili alikutwa katika nyumba aliyokuwa anaishi huku akiwa amefariki na kuondolewa sehemu za siri na kuchunwa ngozi.
“Ndugu yangu Zawadi Mwenga alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kwenda eneo la tukio na kukuta kweli Leonard amefariki.”

Mwenga naye alikuwa na haya ya kusema: 
“Siku mbili kabla ya tukio marehemu alionekana mitaani lakini baada ya hapo hawakumuona tena hadi alipogunduliwa na mwanamke mmoja akiwa amefariki dunia.”

 Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Wenda,  Dismas Ngweta alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa alitaarifiwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lupeta, Geofrey Dugange.
 
Alisema alikwenda eneo la tukio na walipouangalia mwili wa marehemu waligundua kuwa ulichunwa ngozi, kunyofolewa macho, kukatwa sehemu za siri pamoja na kutobolewa katika sehemu ya mguu.
Ngweta ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, aliwaarifu Polisi wa Kituo cha Ifunda ambao hata hivyo, mpaka mwandishi wa habari hizi anaondoka eneo la tukio walikuwa hawajafika.
Tukio hilo la mauaji ni la pili kutokea kijijini hapo baada ya Septemba 25, mwaka huu kuuawa kinyama dereva wa bodaboda na pikipiki yake kutoonekana.

Views: 999

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on November 8, 2012 at 2:37

Hii ni tamaa tu ya hela kama asemavyo Chaoga.

Dismas.... sie tunao amini Mungu wengi wetu ndio watenda dhambi wakubwa. Kuna mchungaji huko Zimbabwe amewahi shikwa akiwa na ngozi za binadamu tena nyumbani kwake

Comment by Christer on November 7, 2012 at 14:35

Mmmmmh yaani huu ni zaidi ya unyama jamani

Comment by Alfan Mlali on November 7, 2012 at 12:24

Duh... Under the same sun!!

Comment by chaoga on November 7, 2012 at 9:12

kutoamini kwamba kuna mungu wala sio sababu ya kufanya ukatili kama huu @ tulonge

ni tamaa tu iliozidi kipimo ya mwanadam kupata utajiri wa njia ya mkato

Comment by Tulonge on November 6, 2012 at 17:07

Binadamu tuna roho ngumu balaa. Nadhani kuna watu hawaamini kama kuna Mungu

Comment by chaoga on November 6, 2012 at 16:19

daah hatari hii kwa kweli, hivi hela inayopatikana kwa njia hii unaitumia kwa amani kweli?

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*