Tulonge

Walaghai kwa njia ya mtandao waamua kutafsiri 'email' kwa kiswahili ili kutunasa vizuri

Hapo juu ni moja kati ya 'email' ambazo hutumiwa na wezi kwa njia ya mtandao. Sasa wameamua kuitumia google ili kutafsiri ujumbe wao katika lugha ambayo wanahisi inatumiwa na muhusika. Kwa vyovyote watakua wanatumia wasifu wa mtu ambao ameuweka kwenye ukurasa wake ili kujua sehemu alipo na lugha inayotumiwa eneo hilo.Baada ya kugundua lugha ya eneo hilo, huitumia 'google translate' ili kutafsiri kiingereza kwenda lugha hiyo.

Hapo juu muhusika (Marbel Johnson) ametumia 'google translator' ili kubadili kingereza na kuwa kiswahili aweze kumnasa mlengwa kirahisi. Hata hivyo google haina uweza wa kutoa tafsiri sahihi 100% kama uonavyo hapo juu.Kuna baadhi ya maneno imeshindwa kutafsiri kutoka kiingereza kwenda kiswahili.

Wezi hawa huanza kwa kutuma ujumbe wa kuomba urafiki lakini baadae huanza kukulaghai na usipokua makini unaweza ukamtumia hata fedha kutokana na uongo atakao kwambia. Pia hutumia picha za wasichana warembo ili kuwanasa wavulana vizuri.

Views: 274

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*