Tulonge

Watoto 3 wa familia moja wamefariki baada ya kugongwa na basi la Mtei wakiwa kwenye pikipiki

Watoto watatu wa familia moja ambao walikuwa wamepanda pikipiki wamekufa baada ya kugongwa na basi la Mtei express katika njia kuu itokayo Singida hadi Arusha ambapo baada ya tukio hilo wananchi wenye hasira waliamua kulichoma moto basi hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Singida SACP Gefrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Mtei Express lenye usajili wa namba T 742 ACU lilikuwa likitokea Singida na kuelekea jijini Arushana pikipiki aina ya Slag yenye usajili wa namba T368 BXZ ambayo ilikuwa imepakia watoto watatu na baba yayo akiendesha.

Katika hatua nyingine kamanda Kamwella amewataja waliokufa papo hapo ni Tabiri Shabani,Kasimu Shabani na Hamza Shabani kafa wakati akipatiwa matibabu na dereva wa pikipiki ambaye ni baba wa watoto hao amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.

Kwa upande wake shuhuda wa tukio hilo ambaye naye alikuwa abiria bwana Nakomolwa Thomas amesema dereva wa pikipiki aliamua kukata kona upande wa kulia bila ya kuangalia kama nyuma kuna basi lina kuja na kusababisha kugongwa na basi na kuburuzwa hadi pembeni mwa barabara.

Naye Nganga Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktali Banuba Deogratius amesema wamepokea maiti mbili , mtoto moja amefariki wakati wanampatia huduma na mwingine ambaye ni baba watoto hao bado anaendelea na matibabu.

Views: 1222

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Dixon Kaishozi on January 10, 2014 at 11:09

Wapumzike Kwa amani.. Umesha sema lile nililo kua nao akilini. @ Mama Malaika. Kama wangetumia pikipiki zaidi ya moja .. basi janga hili lisingekua kama lilivyo sasa. Tutii sheria bila shuruti, ni kwa faida yetu.

Comment by Mama Malaika on January 10, 2014 at 7:32
May their souls rest in peace! Nasikia uchungu kwa hawa watoto. Huyu baba aliyepakia watoto watatu kwenye pikipiki ni muuaji. Pikipiki moja watu wanne??? Masikini sijui hao watoto walivishwa helmet? Sheria za barabarani zikifuatwa huyu baba asingepoteza watoto wake watatu kwa pamoja, tuwe makini na hizi sheria kwani majuto ni mjukuu.
Huyo mama wa watoto jamani sijui analiaje??

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*