Mtoto akijirusha baharini huku Kivuko cha Mgogoni kikiwa kwenye mwendo.
Imekua ni tabia endelevu kwa watoto hawa ambao hudandia hudandia vivuko vya Kigamboni wakati vikianza kuondoka. Kivuko katikati ya bahari watoto hao hujirusha baharini na kuendelea kupiga mbizi. Wakati mwingine watoto hawa hupanda sehemu ya juu ya kivuko na kujirusha baharini, hii ni hatari kwa maisha yao. Haijajulikana kama uongozi wa vivuko vya Kigamboni unaliona hili au la.Maana watoto hao hufanya hayo wakiwa huru kabisa pasipo mtu kuwafuatilia.
Mtoto akining'inia huku chombo kikiwa kwenye mwendo
Muhudumu wa kivuko akiwa bize na kazi, hana habari na watoto hao
Wakijiandaa kujirusha majini
Maji yakiruka juu baada ya mtoto kujirusha baharini toka sehemu ya juu ya kivuko
Add a Comment
Hamna noma, nitawatokea siku moja nichonge nao
Hii ni hatari.. Usiogope kwenda na picha. Maana picha zipo kwenye mitandao ya kijamii tu. Kweli chukua hatua, utakua umeisaidia jamaii kuokoa maisha ya hao vijana kwa njia moja ama nyingine!!
Umesomeka Kisusi, nitawacheck.Ila nitahofia kuwaonesha picha.Maana wameshakataza kupiga picha eneo la feri.Labda kama katazo lao halihusishi kupiga picha ktkt ya bahari.
Kudadeki, yaani hilo limeshakuwa kama mchezo unaokubalika hapo kwny pantoni, zamanai wakati naanza kuyaona hayo nilikuwa najua ni wahuni, vichaa na wavuta unga/bangi ndo wanayafanya hayo lakini kadri siku ziendavyo nimekuja kugundua ni mchezo ufanywao na watu wenye akili zao timamu kabisa, na ninaamini uongozi unayajua yote hayo na kuyaona kwa macho angavu, tatizo ni nani aanze kumfunga paka kengele! Wanakamata mtu anaepita bila kukata tiketi hali ya kuwa wanaruhusu mtu kuning'iniza roho yake kwa kuihatarishia kifo kirahisi namna hiyo! Dismas hebu chukua hatua uende pale kwny ofc zao upande wa magogoni na ujaribu kuwaambia angalau kuwakumbusha majukumu yao, ipo cku yatatokea maafa makubwa sana kwa mchezo huo!
wanasubiria MAAFA. akifa mmoja ndo watakataza
unafikili uongozi haufahamu nina uhakika wanalitambua hili ila ndo hivo wapo busy na maisha yao wao wananchukulia mtoto wa mwenzio ni wako uliyemzaa hapo ni mpaka maafa yatokee ndo watachukua action hii ndo Tanzania kwa kweli.
Hii hatari
© 2023 Created by Tulonge.
Powered by
You need to be a member of Tulonge to add comments!
Join Tulonge