Tulonge

Waziri mkuu kukutana na Tume ya uchunguzi wa matokeo ya kitadato cha IV 2012 kesho

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda (pichani) kesho (Jumamosi, Machi 2, 2013) atakutana na Tume maalum aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa Februari 18, mwaka huu.


Mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi.

Tume hiyo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges (TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia masuala ya elimu.

Wadau wengine wanatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa Jumatatu wiki hii, asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Chanzo: Issamichuzi Blog

Views: 443

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by MGAO SIAMINI,P on March 3, 2013 at 12:56

WALIMU JUUUUUUUUUUU! MPAKA WAWATAMBUE MWAKANI 80% SIFURI

Comment by ANANGISYE KEFA on March 2, 2013 at 13:35

hii nchi bwana wanafanya madudu ili watudanganye kwa kuunda tume

Comment by Tulonge on March 1, 2013 at 17:40

Tunawasubiri kwa hamu tuwasikie

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*