Tulonge

Wivu wa mapenzi wasababisha mchaga huyu kuchoma nyumba yake

Nyumba ya familia moja huko mtaa wa ugombolwa Kata ya Segerea  ikiwa inateketea kwa moto usiku huu mara baada ya Baba wa familia hiyo kuhisi kuwa mke ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mmoja na kuamua kuichoma moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi. 


 Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa


Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog, Dar Es Salaam.Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar  imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyoMpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.

Views: 767

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Hashim Said on December 16, 2013 at 13:59

Ni kweli kabisa Tulonge... Siku hizi kujipiga risasi imekuwa kama fashion!!

Comment by Mama Malaika on December 16, 2013 at 13:37
Hivyo kukosa bastola akaamua kuchukua silaha iitwayo "njiti ya kiberiti" @ Dixon. Teh teh teh...
Wachaga noma... Leo mchaga akija taka oa binti yangu namtoa baruti. Teh teh teh teh...
Comment by Dixon Kaishozi on December 16, 2013 at 10:48

Tena kwa kina Massawee... hahahahaaa.. hawa jamaa ni noma!!!!

Comment by Tulonge on December 16, 2013 at 10:41

teh teh angekua nayo angemaliza wote na yeye angejimaliza.Maana siku hz kujipiga risasi ndo habari ya mujini

Comment by Dixon Kaishozi on December 16, 2013 at 10:19

Inaelekea hakuwa na BASTOLA huyu!!!!

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*