Tulonge

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa sasa kuhakiki upya vyeti vya wafanyakazi wake wote

Na Heri Shaaban
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake wote kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa uhakiki ili kubaini kama kuna vyeti feki.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Job Masima, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Hifadhi ya Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Alisema kuanzia leo, watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa kuwasilisha vyeti vya vyuo walivyosomea."Natoa mwezi mmoja kuanzia leo hadi Januari, wawasilishe yeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada ya ukaguzi tutafuatilia maeneo waliyosomea ili kubaini kama kuna
askari wanaotumia vyeti feki," alisema.


Alisema askari ambao watabainika kutumia vyeti feki na kupata vyeo wakiwa kazini, watashushwa vyeo ambapo lengo a ukaguzi huo ni kuwataka watumishi hao kusomea katika vyuo vinavyotambulika na Serikali si vya mitaani.


Aliongeza kuwa, mpango huo pia utawahusisha watumishi ambao wamesomeshwa na Wizara ambao nao watatakiwa kwasilisha vyeti vyao upya.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa ajili ya kuweka mafao yao.


Alisema kuna mifuko mingi hivyo kila mtumishi anaweza kuchagua wowote anaopenda kujiunga nao ili uweze kumsaidia dhidi ya matukio yasiotarajiwa.Matukio hayo ni pamoja na maradhi, ulemavu, kustaafu kazi,kuacha kwa hiari au kwa lazima. Akizungumzia changamoto zilizopo katika sekta hiyo, alisema takwimu zinaonyesha wananchi walio katika sekta rasmi wanakadiriwa kufikia milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta hiyo.


Majira

Views: 641

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by David Edson Mayanga on December 17, 2013 at 22:02

makubwa hapo mbona watakamatwa wengi sana

Comment by Mama Malaika on December 17, 2013 at 9:40
Dixon... Na wengi wa hao (wana jeshi) wamo CCM ( Komba, Nawiye Sr. na wengine wengi) na walisha shika nafasi za uongozi kama vile ukoo wa mikoa.
Comment by Dixon Kaishozi on December 17, 2013 at 9:07

Tena wasifanye kwa askari wa chini tu.. kama usemavyo hakuna atakae salia. Nakumbuka mtu alikua akifeli darasa la saba au kidato cha nne.. wote walikua wanakimbilia jeshini/polisi.. na wanaenda huko kwa kutumia vyeti bandia vya ndugu jamaa na marafiki.. sasa huo msako hata pona mtu!! 

Najiuliza kwa mfano ukute kamanda wa kanda maalumu anacheti bandia.. hehehee patachimbika hapo.. hili zoezi litawaumiza wanyonge tu!!!

Comment by Mjata Daffa on December 17, 2013 at 8:47

Wapoti utawamaliza maana vyeti FEKI huko ni fasheni, ukisema ukomae utabaki yako.

© 2020   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*