Tulonge

Yanga yalazimishwa sare ya 1-1 na Zamalek.

Timu ya Yanga imetoka sare ya bao 1-1 na Timu ya Zamalek ya Misri katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


Yanga wamejitahidi kucheza mchezo mzuri hasa kipindi cha kwanza ila wamepoteza nafasi nyingi sana za wazi . Bao la Yanga lilipatikana kipindi cha kwanza dakika ya 36 kupitia mchambuliaji wao Khamis Kiiza. Zamalek walirudisha bao hilo kipindi cha pili. Kama kawaida ya timu za Misri, hupenda kupoteza muda kwa kutumia mbinu ya kujiangusha na kusingizia kuumia pale wanapooa matokeo yanafaida kwa upande wao.
Kwa matokeo haya si mazuri sana kwa upande wa Yanga, kwani wanahitaji kutumia nguvu ya ziada katika mchezo wa marudiano huko Misri.


Kama kawaida ya watanzania, uzalendo umekuwa ni kitu kigumu sana. Hili limeoneshwa na washabiki wa Simba ambao waliingia kwa wingi uwanjani ili kuishangilia timu ya Zamalek. Walitimiza lengo lao la kuishangilia timu hiyo hasa waliporudisha goli utadhani na wao ni wazaliwa wa Misri.

Views: 347

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on February 22, 2012 at 15:41

mmesahau wakati simba inacheza na tp mazembe? au mnaangalia kwa simba tu,,,, acheni hizo na jezi za tp mazembe yanga walivaa, sasa ile timu ya uganda inakuja hapa vaeni tena na nyinyi,

Comment by jemadari mimi on February 19, 2012 at 12:32

Wabongo ni watu wa ajabu kabisa    huwezi kushangilia mtu ambaye humjui hata kama anacheza vizuri,utachotakiwa kufanya ni nkunyama tu pale unapoona mwenzako amezidiwa kimchezo,ushauri wangu kwa TFF NA SERIKALI INATAKIWA KULICHUKULIA SUALA HILI KWA UMAKINI WA HALI YA JUU ILI kuepusha ghasia  na umwagaji damu kwa mashabiki wa vilabu hiviviwili

Comment by Alfan Mlali on February 19, 2012 at 0:52

Kasheshe ni huko Misri Yanga wasipojiangalia watarudi na gunia la magoli...

Comment by ILYA on February 18, 2012 at 21:45

Simba mi nawajua sana,hawana ushirikiano kama yanga pindi kunapochezwa mechi za kimataifa.Nakumbuka simba ilikuwa mwaka jana inamenyana na timu moja kutoka visiwa vya Commoro,Yanga waliunga bega kwa bega na timu ya simba na kuitakia ushindi ikiwemo kuisapoti kisoka,lakini leo hii washabiki wa simba wanaonyesha ni jisi gani hawana uchungu na utaifa wao,yaani wanaona bora kusapoti utaifa wa misri kuliko kusapoti utaifa wa Tanzania.

Nina mashaka na utaifa wa shabiki wa simba,huenda wametokea huko uarabuni hawa.

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*