Tulonge

Zaidi ya kilo 200 za madawa ya kulevya zimekamatwa katika bahari ya Hindi.

Zaidi ya kilo 200 za madawa ya kulevya zimekamatwa katika bahari ya Hindi.

 

Zaidi ya kilo 200 za madawa ya kulevywa aina ya heroin yamekamatwa na kikosi cha polisi wanamaji katika bahari ya hindi yakisafirishwa kutokea nchini irani pamoja na mabaharia kumi na wawili kutoka nchi ya Irani na Pakistani.

 

ITV imefika katika eneo la bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia jahazi hilo linalosadikiwa kutokea nchi ya Irani likiwa na shehena hiyo ya madawa ya kulevya ambapo kamanda wa polisi kikosi cha wanamaji Mboje Kanga akielezea.

 

Tukio hilo lililotokea usiku wa tarehe 4 majira ya saa sita usiku waliweza kukamata jahazi hilo na mabaharia kumi na mbili wote wakiwa hawaijui lugha ya Kiswahili wala kingereza na jahazi lao halikuwa na utambulisho wowote wa sheria za majini.

 

Mkuu wa kitengo cha kudhibiti dawa za kulevywa godfrey nzowa amesema jahazi Hilo liliweza kukamatwa baada ya kikosa cha polisi cha wanamaji kuendelea na operesheni zake za doria majini na mara baada ya kulitilia shaka waliweza kulikamata na baada ya kulikagua walikamata shehena hiyo ya madawa ya kulevya Aliyoyataja kuwa ni aina ya Heroin ambayo mengi huzalishwa nchini.

 

Matukio ya kukamatwa kwa dawa za kulevywa nchini yamekuwa endelevu na kipindi hiki mbinu imebadilika tofauti na awali amabapo mengi yamekuwa yakikamatwa kwenye bandari kavu ambapo mwaka juzi zaisi ya kilo 200 zilikamtwa bandari kavu ya Lindi lilo 179 bandari hiyo hiyo,kilo 97 na kilo 81 zilikamtwa kwenye bahari ya hindi yakitokea Irani.

 

Chanzo: ITV

Views: 1109

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by CHA the Optimist on February 10, 2014 at 16:30

DIXON  nipo pamoja na wewe:

Hehehehee.. Ngoja kwanza nicheke kidogo!!! Nashindwa kuelewa labda ni kwa uwelewa wangu mdogo.. "Eti wahusika walio kamatwa bado hawajafikishwa mahakamani kwa KUKOSA MKALIMANI anaye jua lugha yao "Ki-iran.""  Hivi kweli ubalozi wa IRAN hauwezi toa msaada kwa hilo ?  Mbona kuwakamata walishirikiana na Makachero wa uingereza na Marekani.. Na hao pia wameshindwa kutoa msaada kwa hilo... Sijui wanaona "Mimi" ni fala kiasi hicho ? Nisaidieni jaman..

Wajua haiwezekani kwa issue kama hii Ubalozi washindwe kutoa msaada kwa maana ya mkalimani...haingii akilini. Na kama wao (Ubalozi) wameshindwa kutoa msaada wa hili, yawezekana hawakuombwa, na kama waliombwa--na wakashindwa kutoa msaada, basi hakuna uhusiano mzuri baina ya nchi hizi mbili Tanzania na Iran.

Comment by Bonielly on February 10, 2014 at 13:41

jamani tumuombe mungu azidi kutuonyesha kama hivi, vijana tunaathirika vibaya sasa kilo 200 zote unategemea nini? zikiingia mashuleni si msiba huo?

Comment by Dixon Kaishozi on February 6, 2014 at 8:36

Hehehehee.. Ngoja kwanza nicheke kidogo!!! Nashindwa kuelewa labda ni kwa uwelewa wangu mdogo.. "Eti wahusika walio kamatwa bado hawajafikishwa mahakamani kwa KUKOSA MKALIMANI anaye jua lugha yao "Ki-iran.""  Hivi kweli ubalozi wa IRAN hauwezi toa msaada kwa hilo ?  Mbona kuwakamata walishirikiana na Makachero wa uingereza na Marekani.. Na hao pia wameshindwa kutoa msaada kwa hilo... Sijui wanaona "Mimi" ni fala kiasi hicho ? Nisaidieni jaman..

Comment by CHA the Optimist on February 5, 2014 at 14:43

Hizi dili nazisaka sana wadau. ikipatikana nishirikisheni. Najua niki-win tu, Millions of Tshs kiulaini, serious.

Comment by MGAO SIAMINI,P on February 5, 2014 at 12:05

hii ni noma

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*