Tulonge

Zaidi ya nyumba 400 zimefurika maji kutokana na mvua kubwa mjini Tabora

Zaidi ya nyumba mia nne zimefurika maji na wananchi wanatoka nje kwa tabu kutokana na mvua kubwa iliyonyesha zaidi ya saa nne, mjini Tabora, ambapo imeleta adha kubwa na kusababisha mifugo kama kuku na bata kusombwa hali ambayo imebainishwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kutokana na vyoo kujaa maji.

 

Wakiongea na ITV wananchi wa kata ya Chemu Chemu waliokubwa na mafuriko hayo wamelalamikia ujenzi wa holela pamoja na kutokuwepo na miundombinu ya kupita maji haya ambayo maji yanatafuta njia yenyewe na maatokeo yake ni kuingua majumbani mwao na kuharibu samani mbali mbali.

 

Meya wa manispaa ya Tabora Gulamu Husein, mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw Alfred Mulwanda, na wakuu wa idara waliofika katika kata hiyo mara baada ya kupata taarifa za mafuriko hayo, wamekiri miundombinu duni kusababisha mafuriko hayo na kudai kuwa, hali hiyo itafanyiwa marekebisho ya haraka ili kurejesha hali yake ya kawaida.

Views: 291

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*