Tulonge

Zanzibar: Jaribio la kulipua eneo la biashara lashindikana

Watu wasiofahamika bado, usiku wa kuamkia jana Jumatatu walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa bomu lililokuwa katika mfano wa 'sausage' karibu na eneo la biashara kando ya Barabara ya Darajani mjini Zanzibar.Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis Mkadam akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana kuhusu taarifa hiyo alisema, mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour (36), aliyekuwa kazini kwenye

 Duka la Sahara, aliona idadi
ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakitokea Bwawani kuelekea
Mkunazini, walikwenda uelekeo wa dukani alipokuwa akilinda, na
walipofika hapo walipunguza mwendo, ndipo mmoja wao aliporusha guruneti
upande wake, na kitu hicho kilitua katikati ya masanduku yaliyokuwa
mbele ya duka hilo.

"...lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa,
Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," "Kwa bahati, Amour
alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo
wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku,
" alisema Mkadam,
 akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti
kubwa dakika chache baadaye.

Polisi walifanikiwa kupata mabaki ya unga unga na kukusanya kokoto zilizotokana na athari ya mlipuko huo.

Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, na kuwataka
Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa.

Kilele cha Habari Blog

Views: 347

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by habiba mustafa mlawa on September 25, 2013 at 10:49
majanga hii dunia inakoelekea sio lakni ndo madhumuni ya freemason
Comment by Christer on September 25, 2013 at 0:01

Ilikua tindikali na risasi sasa Milipuko. Mungu tunaomba utuokoe

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*