Tulonge

Zimbabwe: Rais Robert Mugabe atumia mil 974.9 kwaajili ya kusherekea 'Birthday' yake

Rais Mugabe na Mkewe wakikata keki ambayo ilikua na uzito wa 89kg

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alitimiza miaka 89 tarehe 21 feb 2013. Katika kusherekea siku hiyo alifanya sherehe kubwa iliyofanyika uwanja wa Chipadze huko Kaskazini Mashariki mwa mji wa madini (Bindura).

Mugabe ambaye ni mmoja wa viongozi waliotumikia nchi zao kwa muda mrefu, alikata keki kubwa yenye uzito wa kilogramu 89 na baada ya hapo aliachia maputo 'balloons' 89 angani.

Ripoti iliyo tolewa na 'Newsdzezimbabwe' imesema Gavana wa Zimbabwe Dk. Gideon Gono alimzawadia Mugabe ng'ombe 89. Zawadi nyingine ni biblia, rosali, ndama, kondoo na vyakula. Pia ripoti hiyo ilieleza kuwa £400,000 (Tsh mil 974.9) zilitumika katika kufanikisha sherehe hiyo.

Katika sherehe hiyo Mugabe alisindikizwa na Mkewe Grace pamoja na watoto wao wawili.Hapa Mugabe akiachia angani maputo 'balloons'Mugabe akila keki, kulia ni mkewe

Views: 1255

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ANGELA JULIUS on March 6, 2013 at 14:46

DAH SINA USEMI NA WALA HATA SIJUI  NIANZIE WAPI NIISHIE WAPI ILA MWISHO WAKE UPO.

Comment by Mama Malaika on March 4, 2013 at 21:14

Huyu bwana na mkewe wana kufuru sana kwa Mungu, na kila mwaka hivi karibuni Mugabe amekuwa akisheherekea birthday yake kwa gharama kubwa sana. Inasikitisha sana kwani Zimbabwe hivi sasa kuna dhiki kupindukia halafu raisi anatumia £400,000 (Tsh mil 974.9) kwenye sherehe isiyozidi masaa 3. Just shaking my head....

Comment by manka on March 4, 2013 at 19:36

mwiziiii, mkubwa huyu!!

Comment by ANANGISYE KEFA on March 4, 2013 at 17:31

ndio maana hataki kuachia madaraka

Comment by MGAO SIAMINI,P on March 4, 2013 at 13:41

wizi na ubadhilifu wa pesa za uma

Comment by Samweli Joseph on March 4, 2013 at 10:22

hii ni kufulu wananchi maskini yeye anatumia paund 400,000 kwa siku tu yakuzaliwa di is bu shit ufisadi wa hali ya juu kweli africa tutatoka never like this

Comment by Georgia Mushashu on March 4, 2013 at 9:01

Mmm amshukuru Mungu tu kwa kuufikia umri huo maana kwa kizazi cha leo ni ndoto

Comment by Christer on March 4, 2013 at 7:48

Mmmmmmh zawadi ya ng'ombe 89 ufisadi mtupu!! keki ina uzito wa kuzidi uzito wa mtu, tena mtu mzima hahahhahaaaaaaaaaaaa aya bwana FISADI tumia pesa!!!!!!!!

Comment by Tulonge on March 4, 2013 at 6:44

Duuh!

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*