Tulonge

Hadithi! hadithi: Hadith njoo, uongo njoo utamu kolea

JAMAA1 alienda kumnunulia MPENZI wake keki ya birthday, kanunua mwenyewe ya sh elf15 akapanda daladala kaishikilia isiharibiwe, mala akashuka ki2oni akatembea kwa umakin asijikwae keki ikaanguka.

Wakat anafika eneo la 2kio na Range ikawa inapaki nje, bana we! akashuka mkaka very smart(WA RANGE) mh na vijana wawil wakashusha keki ya chocolate ina ngazi3 na zingine2 za pembeni,

JAMAA akajipa moyo kwamba mh bwana yule ni MPENZI wangu atapokea hata hk kidogo,

haa! wakat JAMAA anawaza hayo akaona MPENZI wake kapigilia kigaun cha uchokoz akamkumbatia WA RANGE afu akamkisi shavu la kushoto mwaah, la kulia mwaah kwenye lips mmmh!

JAMAA: (akashtuka) mh mbona na lips zalabwaa mh! (Akajipa Moyo) wacha nijitose.
MPENZI: (alivyomuona akamdaka) ''jaman kaka karibu kwa birthday yangu''
JAMAA : mh mi kakako wewe?
wakat anauliza, MPENZI akasepa kumuwai WA RANGE wakaenda kuketi mbele kulee, wakat JAMAA anaduwaa mashost wa MPENZI wakamdaka,
Mashost: shemej leta keki ikakatwe itawekwa kwenye chakula cha pamoja, afu njoo huku siti yako ipo nyuma.
JAMAA:What? natakiwa nikae na MPENZI wangu mbele.
MASHOSTI: ebu njoo ukae bana.

Mala MUPENZI akasimama akamtambulisha WA RANGE kama ndo kishtobe wake wa moyo, WA RANGE akasimama wakakata keki wakalishana kwa mdomo.

Haa JAMAA akataka kusimama kwenda mbele, mashost wakamvuta chini.
MASHOSTI: Shemeji ebu 2lia, nin lakin kumuaribia mwenzio?
JAMAA: nyi mnaona sawa vile amefanya?
MASHOSTI: pole shemeji hapa hapendwi m2 inapendwa pesa.
JAMAA: (kwa hasira akasema) mwambien asante ananifanyia mim hv (huku anasepa) poa Mungu yupo.
MASHOSTI: (cheko la unafki!)

Views: 2385

Reply to This

Replies to This Discussion

Doh! yaani Dis umeongea maneno ya maana kama mtu kweli?! vile lol.

mwenye mapenzi ya dhati ni mimi pekeangu huwa naangalia moyo wangu unasema nini. ila wadada wa sikuhizi huwa wanaangalia chapaa utakuta anakuahidi vitu viingi kuwa atakuwa na wewe katiak shida na raha hata chini atalala ukikosa atakuvumilia hebu kuwa nae uone?!. kuna rafikiangu siku walikuwa na mkewe kituo cha basi wanasubiri daladala kama mnavyojuwa daladala za bongo asubuhi zinavyosumbuwa akapita jamaa anaendesha Range Rover mwanamke akamwambia mumewe angalia kidume hicho kina mkoko wa maana sio wewe mwanaume suruale rafikiangun ilimuuma sana mpaka kaja kuniambia najikuta nasema mapenzi bila pesa hakuna mapenzi kwa wadada wa sasa.

Duh! Huyo mwanamke ni materialism, hafai. Hakuna kitu kibaya kumuumiza roho mumeo kama kumwambia hivyo. Range Rover ni gari kama gari nyingine ikigonga ni karatasi na thamani yake imeisha.

Omary said:

Doh! yaani Dis umeongea maneno ya maana kama mtu kweli?! vile lol.

mwenye mapenzi ya dhati ni mimi pekeangu huwa naangalia moyo wangu unasema nini. ila wadada wa sikuhizi huwa wanaangalia chapaa utakuta anakuahidi vitu viingi kuwa atakuwa na wewe katiak shida na raha hata chini atalala ukikosa atakuvumilia hebu kuwa nae uone?!. kuna rafikiangu siku walikuwa na mkewe kituo cha basi wanasubiri daladala kama mnavyojuwa daladala za bongo asubuhi zinavyosumbuwa akapita jamaa anaendesha Range Rover mwanamke akamwambia mumewe angalia kidume hicho kina mkoko wa maana sio wewe mwanaume suruale rafikiangun ilimuuma sana mpaka kaja kuniambia najikuta nasema mapenzi bila pesa hakuna mapenzi kwa wadada wa sasa.

Hahahaha Dixon mi nilale chin nimekua na mapenzi ya kiha? Watan zangu waha ndo hata huwe unalala nje atakupenda tu hahahaha.

Reply to Discussion

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*