Tulonge

Ukiwa kama mwanaume unaishi katika nyumba yako peke yako mara wahisi kuna mtu anakuwa aingia nyumbani kwako na kula chakula ndani friji lakini hujawahi kumkuta/muona au kumshika na hiyo imekutokea karibu yafikia mwaka. Iwapo siku ya siku unamkuta mwanamke ndani ya hiyo nyumba yako kajificha ndani ya kabati (kubwa za kujengelea) ambayo ndio kageuza makazi yake utamfanya nini?????? Utaendelea kumkarimu kumsaidia??? Kumuachia huru aende zake au kudai malipo yako???????

Kuna kisa kimetokea huko nchini Japan miaka 4 iliyopita homeless woman alijipatia hifadhi kisiri siri kwenye nyumba ya mtu (mwanaume) bila ya mwenye nyumba kujua.

Kwa habari zaidi soma hapa chini...

http://www.telegraph.co.uk/news/newstopics/howaboutthat/2054057/Hom...

Views: 773

Reply to This

Replies to This Discussion

OLIVIA... Tatizo la homeless nchi zilizoendelea mara nyingi inakuwa ni kujitakia kwani kunakuwa na sehemu (majumba) maaum ukijiona uko homeless unaenda huko kuishi unapewa chakula na kila kitu isipokuwa huruhusiwi kunywa pombe, kuvuta sigara au kutumia madawa ya kulevya. Natumai hata Japan wana sehemu hizo pia. Tatizo wengi hawataki kukaa huko na kuhamia mitaani sababu ni ma-drug addicts, alcoholics, wachafu hawataki kuoga, etc.

Kwa UK... nikimshika mtu kama huyo ndani mwangu nitakuwa kama DISMAS kwani nita dial 999 moja kwa moja na kuita police waje haraka ingawa najua police watamuachia akisha maliza kuandika maelezo na kumlazimisha aende kwenye homelesss shelters. ukizingatia kuna kazi nyingi mzungu hataki kufanya lakini mwafrika akija anazifanya na kupata malipo kiurahisi hapo hata huruma sitomuoenea... 

Tuchukulie muda wote huo alikuwa anakuiba kwa sababu ya matatizo na nimnyonge ana mtihani kimaisha,lakini sasa bado hilo si sababu ya kumuonea huruma,maana njia aliyoichagua kukabiliana na hali yake si ya kibusara.Mwizi yeyote sawa sawa awe mnyonge au amejaliwa na Mungu kimaisha,na sawa sawa awe mgonjwa wa HIV hana wa kumsaidia au mzima kiafya,na sawa sawa awe mtoto au mkubwa,mwendawazimu au mzima kiakili,akiiba tu hatakiwi kuhurumiwa maana hata vitabu vya mungu vimeharamisha kuiba na haingii akili kusema mtu anakwiba sababu ya unyonge,so kaka Omary usiseme hivyo kwani alitakiwa kama ni unyonge kutumia njia za kihekima kukabiliana na hali yake kama kwenda sehemu husika kuomba misaada au kumuomba huyo anae mwibia badala ya kumuibia kihivyo.

Na ndio maana mimi nikasema nikimtia mikononi simuulizi una unyonge kimaisha au nini,nikumalizana nae kama ni mwanamke na kumuoa nikigundua tatizo lake ndio hilo ukizngatia mwibiwaji bado bachela zaidi,maswala ya oo kama ana ukiwmi na umesha malizana nae hayo hayapo maana ukiwmi sio uliomtuma akwibe ni mwizi kama mwizi mwingine wa kawaidia, na nitamtandika makonzi kilo kumi kama ni mwanaume,then kufikishana mbele ya sheria kimaelezo zaidi.

namuacha aende siongei nae, atajiua mwenyewe kwa hofu ya kuacha, atajiuliza miaka yote hajanihukumu wala kunisemesha,

Kaka boni yaani namna hiyo utakuwa hujamtedea haki na ni kumdhulumu.!!!!!!Haki yake ni kumalizana nae kwani kuna ubaya gani mkimalizana.??!!1,si bomba tu.

Mmmmhh...Hapa kuna vitu viwili..

1. Kitendo cha kumkuta mtu ndani kwangu tena kwenye kabati lazima nitoke nduki kwanza breki ya kwanza nje ya nyumba....hahahahahahah ndipo nianze kupiga mahesabu ya kurudi kumuangalia ni nani asije kuwa jini akanitoa roho.....

2. Nikiwa na ujasiri wa kumkabili na kugundua kuwa sio mchawi au jini na ni mwanamke lazima anipoze machungu mara mbili..moja la kula msosi wangu na la pili la kunifanya nitoke nduki ndani kwangu..then ndio tutazungumza vizuri kuhusu yeye kuendelea kufaidi msosi na huku akilala kitandani kwangu badala ya kujificha kabatini..tehetehetehteehete

Hahahaaa.. kwanza nduki.. hahaha halafu mengine badae.. @ Alfan!!

DOH!  hatimae Mama kafunguka kikamilifu me nilikuwa nafikiri wa Mama wanahuruma sana wanaweza kukaa nae chini na kumuuliza kinachomsibu mpaka akala chakula cha bule?! kumbe hapahitaji huruma ngumi m2 lol.

  Kwa upande wangu ningeamua kuwaita wazee wa kazi police.

  Maana mwanzo nilikuwa nafikiria kwanza alipe alichotumia, lakini kwa usalama wangu siwezi kujua ni mtu wa namna gani.

  Anaweza akawa criminal aliyekimbia jela au anatafutwa au kichaa au asije akanifia mikononi mwangu nikaleta balaa jingine!!

Kama ulikuwepo kaka Eddie, kuna mchungaji wa kanisa la mji (Bristol-southwest England) si mbali nasi hapa kwetu kauawa na homeless nyumbani kwake kisa alimkaribisha homeless kipindi cha baridi kali ampe hifadhi ya usiku siku hiyo kulikuwa baridi nje minus 12 (-12C), kumbe homeless ni drug addict na pia aliwahi tiwa ndani miaka 2 kwa kosa la kutaka kum-baka binti wa umri wa Secondary School. Basi kamchoma kisu cha tumbo mchungaji wa watu na kachukua pesa na kukimbia, lakini uzuri wa hawa wenzetu waingereza huyo homeless kashikwa alikuwa kakimbilia north England akiwa mbioni kuingia Scotland na hapo ni baada ya police hunting na kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kutolewa sura yake.

Wema umemponza mchungaji wa kanisa, na hicho ndio kinachotuogopesha sana nchi hii kusaidia homeless. Wengi homeless wa hapa si wema kwani ni drug addicts, wahalifu na wengine ni vichaa waliopata nafuu na kukimbia makazi yao (vituoni).

OMARY ndugu yangu na mie nilipokuwa Tanzania nilikuwa mwema sana tu kama wewe, lakini kuishi miaka karibu 20 nchi hii nimejifunza na kusikia mengi kiasi kwamba hata kusaidia mtu nakuwa naogopa. Kuna watanzania tu wenyewe walishaniibia kwa roho yangu ya huruma. Wakuta mtu anakuja wamsaidia sababu ni mtanzania mwenzio kakwama ugenini kumbe mwenzio ni tapeli unakujua kusikia kwa watu baada ya kulizwa (tapeliwa).

Pole sana dada, mimi nilipofika huku nilishangaa kwanini watanzania wanakimbiana. Baadae nilipata jibu kwamba wengi ni matapeli! Inabidi umjue mtu in and out umkaribishe.

Mama Malaika said:

Kama ulikuwepo kaka Eddie, kuna mchungaji wa kanisa la mji (Bristol-southwest England) si mbali nasi hapa kwetu kauawa na homeless nyumbani kwake kisa alimkaribisha homeless kipindi cha baridi kali ampe hifadhi ya usiku siku hiyo kulikuwa baridi nje minus 12 (-12C), kumbe homeless ni drug addict na pia aliwahi tiwa ndani miaka 2 kwa kosa la kutaka kum-baka binti wa umri wa Secondary School. Basi kamchoma kisu cha tumbo mchungaji wa watu na kachukua pesa na kukimbia, lakini uzuri wa hawa wenzetu waingereza huyo homeless kashikwa alikuwa kakimbilia north England akiwa mbioni kuingia Scotland na hapo ni baada ya police hunting na kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kutolewa sura yake.

Wema umemponza mchungaji wa kanisa, na hicho ndio kinachotuogopesha sana nchi hii kusaidia homeless. Wengi homeless wa hapa si wema kwani ni drug addicts, wahalifu na wengine ni vichaa waliopata nafuu na kukimbia makazi yao (vituoni).

OMARY ndugu yangu na mie nilipokuwa Tanzania nilikuwa mwema sana tu kama wewe, lakini kuishi miaka karibu 20 nchi hii nimejifunza na kusikia mengi kiasi kwamba hata kusaidia mtu nakuwa naogopa. Kuna watanzania tu wenyewe walishaniibia kwa roho yangu ya huruma. Wakuta mtu anakuja wamsaidia sababu ni mtanzania mwenzio kakwama ugenini kumbe mwenzio ni tapeli unakujua kusikia kwa watu baada ya kulizwa (tapeliwa).

D u1 Dada hiyo story ya hao wachungaji hata mimi ninayo moja ...hivi karibuni kuna family moja ya mchungaji  kutoka USA na mkewe m-Canada walihamia hapa kwa nia ya kuhubiri injili..!

Ilifika siku moja walimchukua jamaa mmoja njiani kumsaidia nyumbani kwao kwa kumpa chakula na shelter.

Huyo jamaa alikuwa ni mbwiaji wa drugs aliishiwa.

Basi alim-time jamaa na kumpiga na kumg'oa meno. Na alikimbia ..Police walimkamata na walimwita jamaa ili aandike Police statement na kumshtaki ...lakini jamaa alikataa kumshtaki. Ilibidi Police wamuache jamaa ila tu walimuony chochote kitakachotokea watamuweka ndani. Lakini mchungaji kwa woga ilibidi ahamie mji mwingine!

Mama Malaika said:

Kama ulikuwepo kaka Eddie, kuna mchungaji wa kanisa la mji (Bristol-southwest England) si mbali nasi hapa kwetu kauawa na homeless nyumbani kwake kisa alimkaribisha homeless kipindi cha baridi kali ampe hifadhi ya usiku siku hiyo kulikuwa baridi nje minus 12 (-12C), kumbe homeless ni drug addict na pia aliwahi tiwa ndani miaka 2 kwa kosa la kutaka kum-baka binti wa umri wa Secondary School. Basi kamchoma kisu cha tumbo mchungaji wa watu na kachukua pesa na kukimbia, lakini uzuri wa hawa wenzetu waingereza huyo homeless kashikwa alikuwa kakimbilia north England akiwa mbioni kuingia Scotland na hapo ni baada ya police hunting na kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kutolewa sura yake.

Wema umemponza mchungaji wa kanisa, na hicho ndio kinachotuogopesha sana nchi hii kusaidia homeless. Wengi homeless wa hapa si wema kwani ni drug addicts, wahalifu na wengine ni vichaa waliopata nafuu na kukimbia makazi yao (vituoni).

OMARY ndugu yangu na mie nilipokuwa Tanzania nilikuwa mwema sana tu kama wewe, lakini kuishi miaka karibu 20 nchi hii nimejifunza na kusikia mengi kiasi kwamba hata kusaidia mtu nakuwa naogopa. Kuna watanzania tu wenyewe walishaniibia kwa roho yangu ya huruma. Wakuta mtu anakuja wamsaidia sababu ni mtanzania mwenzio kakwama ugenini kumbe mwenzio ni tapeli unakujua kusikia kwa watu baada ya kulizwa (tapeliwa).

Duh,kumbe wavuta unga noma kihivyo,yaani mtu nakukaribisha home ili nikupe hifadhi uokoke na baridi kali then unanitungua kisu kisha kuchukau mshiko wangu???!!! Jamani jamani,hii hatari sana.Sasa watu kama hawa wanatufanya sisi wema tushinde kujua nani kweli anahitaji msaada na nani kibaka.

Na ndio maana mimi mwanzo nilisema nikikukuta ndani kwangu usha kula misosi yangu mwaka mmoja lazima tumalizane hapo hapo,hakunacha HIV wala nini.

Dunia hii yenyewe ya leo watu wanamiliki vifaa vya kupima HIV majumbani mwao,sasa hapo ndio utakopa kwanini ulikikwiba msosi wangu.Labda vipimo vilete noma.Hahahahah

Reply to Discussion

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*