Tulonge

Morogoro. Wasomi nchini, wamehimizwa kujifunza lugha ya Kichina, ili washiriki katika kukuza uchumi wa nchi kwa kuzingatia kuwa uchumi wa dunia unategemea sana bidhaa na mchango wa China kwa sasa. Rai hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Saidi Amanzi. Hotuba hiyo ilisomwa katika uzinduzi wa ushirikiano wa ufundishaji wa lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha mjini Morogoro. Bendera aliwaasa wasomi kutumia fursa ya Kichina, kujifunza kwa bidii na kupanua wigo takaayowawezesha kuwasiliana katika kufanya biashara kati ya Watanzania na Wachina. Katika uzinduzi wa ushirikiano huo, Makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Hamza Ngozi, alisema kuwa ni vyema wanafunzi wakajifuza lugha hiyo na kuitumia kama nyenzo ya kutafuta maarifa zaidi katika dunia ya utandawazi. Alisema chuo kikuu hicho ni tatu nchini kuanza kufundisha lugha ya Kichina, baada ya Chuko Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma. Wanafunzi wa chuo kikuu hicho walisema ushirikiano huo ni mzuri na upaswa kuigwa na vyuo vikuu vingine.

Chanzo: www.mwanachi.co.tz

[English yetu iko poor! Kiswahili chetu chenyewe, hatukijui vizuri bado wanahimiza kujifunza Kichina--kama si upuuzi huu ni nini]?

Haya ndio matatizo ya mtu kukurupuka--yaani mtu anaongea jambo bila kutafakari. Mtu unashauriana na mke wako then unaamka asubuhi na ku-present kwa jamii.

Views: 1535

Reply to This

Replies to This Discussion

CHA the great, naona unajiita the OMNISCIENT sasa!.....................Ila acha vijembe, vijembe vyako vinachoma kumoyo...lol

CHA the Omniscient said:

Naposema hatujui Kiswahili au English ninamaanisha--maneno yangu yanajidhihirisha katika maoni ya dada yangu Habiba.
Dada Habiba, wewe mwenyewe Kiswahili hujui, narudia tena kwa msisitizo dada Habiba Kiswahili hujui vizuri, ndio maana basi umekosa neno au msamiati wa Kiswahili wa neno "comment" ndio maana basi umeishia kusema "unacomment" hakuna neno katika lugha ya Kiswahili kama hilo la "unacomment". Vilevile hakuna neno "kingereza" (rejea maoni yako) katika lugha ya Kiswahili, badala yake kuna neno "Kiingereza". Mengine namezea tu.
Amani iwe nawe dada.
PamoJah.

Sipo teyari kujifunza Kichina kwanza hakivutii. Kiswahili kwanza tujifunze, Kiingeredha na inatosha. Lugha nyingi za kazi gani. Siwezi mie. Lol!

waacheni wanajua wajifunze tusicombine watu, kusema watanzania masikini sema mm masikini

shost yangu Habiba, kubali yeishe. na ukitaka kupigana vita hakikisha yule unayetaka kupigana naye unamjua. Usipofanya hivyo atakutandika tu. Cha the great ulimchukulia pouwa sana, ana fujo huyo, ana makeke huyo, unapomvamia ujipange. Ila amani itawale kijijini kwetu. Love you all!

habiba mustafa mlawa said:

waacheni wanajua wajifunze tusicombine watu, kusema watanzania masikini sema mm masikini

Nimekukubali. Wewe kweli ni The Great. Ingekuwa ni mimi Habiba, ningekutafuta nikuombe msamaha. Yaani kama ni vita, basi umechokoza jeshi la Wamarekani. LOL

CHA the Omniscient said:

Naposema hatujui Kiswahili au English ninamaanisha--maneno yangu yanajidhihirisha katika maoni ya dada yangu Habiba.
Dada Habiba, wewe mwenyewe Kiswahili hujui, narudia tena kwa msisitizo dada Habiba Kiswahili hujui vizuri, ndio maana basi umekosa neno au msamiati wa Kiswahili wa neno "comment" ndio maana basi umeishia kusema "unacomment" hakuna neno katika lugha ya Kiswahili kama hilo la "unacomment". Vilevile hakuna neno "kingereza" (rejea maoni yako) katika lugha ya Kiswahili, badala yake kuna neno "Kiingereza". Mengine namezea tu.
Amani iwe nawe dada.
PamoJah.
Hilo jina tu "the Omniscient" mie tayari nilisha kuvulia kofia na kunyanyua mikono juu, sina ubishi @ CHA. Ha haaa haaa....

Ha ha ha ha! Dada (Mama M)....umenifurahisha sana. Waogopa jina la "the Omniscient"--najua unaogopa kwa sababu unajua maana ya "OMNISCIENT" kwa asiyejua hawezi kushtuka au kuogopa.

Mama Malaika said:

Hilo jina tu "the Omniscient" mie tayari nilisha kuvulia kofia na kunyanyua mikono juu, sina ubishi @ CHA. Ha haaa haaa....
Ha haaaa haaa haaaa haa haaa haaaa... Jina hilo lina maana kubwa na la kufaa wewe tu kwani you're a man of integrity.

CHA the Omniscient said:

Ha ha ha ha! Dada (Mama M)....umenifurahisha sana. Waogopa jina la "the Omniscient"--najua unaogopa kwa sababu unajua maana ya "OMNISCIENT" kwa asiyejua hawezi kushtuka au kuogopa.

Mama Malaika said:

Hilo jina tu "the Omniscient" mie tayari nilisha kuvulia kofia na kunyanyua mikono juu, sina ubishi @ CHA. Ha haaa haaa....

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*