Tulonge

KISA CHA KWELI....SOMA UPATE MAFUNZO MAKUBWA.....

KISA CHA KWELI....SOMA UPATE MAFUNZO MAKUBWA.....

USIKU WA HAMU..................

Kijana mmoja mzuri mwenye nafasi nzuri ya maisha, aliamua kuoa. Hivyo alipata mchumba mwenye nisabu yake. Alifanya matayrisho mazuri ya harusi yake. Kwa...
vile alikuwa na uwezo basi harusi yake ilifana na kupendeza mno. Pia ilisifika na ikawa ikizungumziwa huku na kule. Baada ya harusi kumalizika, wana harusi hawa

 kwa hamu walikwenda nyumbani kwao. Wote walifurahishwa na maandalizi ya harusi na vile vile katika nyumba yao. Kila mmoja akiwa na hamu na mwenziwe. Kwa hakika ulikuwa ni usiku wa thamani. Hali hiyo iliwafanya kujihisi hakuna mwingine alie na raha katika usiku ule. Walipokuwa wameketi kula chakula mezani, kengere mlangoni ilisikika kwa sauti. Ama kwa hakika ilimkera sana bwana harusi na kuwaza nani atakuwa katika usiku huo wa dhahabu, usiku alio usubiri muda mrefu. Na atakuwa anahitaji nini kwangu. Aliwaza na kujesemea moyoni, “Laiti huyo angalijua mipango yangu basi, asingalipita hata karibu ya nyumba hii”. Bi harusi aliinuka hadi mlango mkubwa wa nyumba. Alifungua mlango na kuona ni mtu mhitaji. Alirejea na kumwambia mumewe kuwa ni mhitaji. Bwana harusi huyo kwa hamaki ya kukatizwa starehe yake, alifungua mlango kwa ghadhabu na na kuuliza nini alihitaji yule mtu. Nae alsema, “mimi mhitaji naomba chakula kama kipo chochote!” Bwana harusi alianza kumfokea mtu yule. Si hivyo tu bali alimpiga na kumuumiza kisha alimfukuza. Bi harusi hakupendezewa na tukio lile lakini hakusema kitu”. Baada ya kula, hali ilibadilika na bwana harusi akaanza kupiga kelele na kuwa kama aliepata jinni, alikimbia na kutoweka bila kujulikana kamwe.


Binti huyu alibakiwa na unyonge kwa muda mrefu. Kwani hakubahatika kupata ladha ya kuwa mke. Baada ya mika kumi na mitano, posa ingine ilimuijia, bila kusita aliikubali. Na katika harusi hii iliyofana, bi harusi alitamani kuona usiku ule ukimalizika salama kwa matamanio aliyoyaweka kwa muda mrefu saaaana. Wakiwa wemerejea nyumbani wana harusi hawa wlikuwa katika faraja na furaha kubwa. Hamasa kubwa ilikuwepo kwa bi harusi akiwa na matumaini makubwa. Kama vile ilivyomtokea katika wingu la mapezi ya harusi ya mwanzo, kengere ilisikika wakiwa mezani wanakula. Bila kusita, bi harusi alikwenda kufungua mlango. Akumuuliza “wewe nani na unataka nini?” nae alisema hana lingine bali ni chakula tu. Bi harusi alirejea ndani akilia kwa uchungu. Bwana harusi huyu (wa pili) akamuuliza “vipi mpenzi, umepatwa na nini, mtu huyo amekukera, au kuna kitu kimekukera” Bi harusi akasema kuwa mtu yule anaomba chakula. Bwana harusi huyu akajibu, “basi kama ni chakula bora tumpe chakula hiki chetu.

Nitamplekea hapo nje ale hadi ashibe na kitachobakia tutakula sisi” Bi harusi alistaajabishwa kwa hekima hiyo. Bwana harusi alimplekea yule mhitaji kile chakula kisha alirejea kwa mkewe. Akamwambia, “lakini hukuniamabia kwa nini ulikuwa ukilia?” Hapo bi harusi kwa utulivu alimueleza mumewe. “huyo mtu mhitaji ndiye alikuwa mume wangu wa mwanzo. Ilikuwa uskiu kama wa leo na hali kama hii hii. Alikuja muhitaji kuomba chakula, lakini alihamaki na kumpiga na kumfukuza. Hakuwahi kuujua utamu wa harusi katika usiku ule, nae alipatwa na hala ya ajabu na kukimbia. Alitoweka wala sikumuona tena ila leo. Na hivi nalia kwa sababu ya kumuona hali ilivyomgeukia”. Baada ya hapo bwana harusi huyu aliangusha kilio na kutokwa machozi kwa wingi. Bi harusi alishangazwa na kudhani alimuudhi mumewe, hivyo alimbembeleza kwa mapenzi hatimae alinyamza. Bwna harusi huyu hakutaka kupoteza wakati kwani alihisi binti yule atamdhulumika kwa mara ya pili. Bali aliseama, “Mimi nimelia sana kwani yule mtu alieyepigwa na kufukuzwa na huyo bwana, ndie mimi”


Wote walimshukuru Mwenyezi Mungu na kuweka moyoni mwao kwamba:
KAMA TADINU TUDAANU
(Kama utavyomtendea mwenzio basi vivyo hivyo utatendewa).

Ndugu zangu, Hisani hulipwa kwa hisani
Mwenyezi Mungu Anasema: (surat Arrah’maani aya:60) {Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani}
Kamwe usimrudishe muhitaji hata akiwa juu ya farasi. Na tambua kuwa dua ya madhlum (aliedhulumiwa) haina pazia au kikwazo.

 

Views: 1169

Reply to This

Replies to This Discussion

Maisha ni kama GWARIDE ,amri ikitoka kwa Allah " eeh! kaza mguu mbele tembea na amri nyengine kwa Allah - nyuma geuka.....

Ujue ,gwaride wale walio mbele kwa amri hii ya pili watakua nyuma na wa nyuma watakuwa mbele....

NDIO MKASA uliotokea na ndio mambo yanavyokuwa.

Ama kweli mtenda hutendwa.... 

aiseeeeee nimesoma nitarudi baade kucomment

mmh ni nzuri ila inasikitisha.mtotomzuri said:

aiseeeeee nimesoma nitarudi baade kucomment

Reply to Discussion

RSS

© 2022   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*