Tulonge

Wapendwa swali ni rahisi sana, kama ambavyo linauliza; mimi binafsi ukiniuliza swali hilo--jibu lake litakuwa ni kwamba "naogopa kufa kwa sababu sijatimiza ndoto yangu/zangu".

Ila nina imani wapo watu wanakuwa na hofu ya kifo kwa sababu tofauti tofauti. Wapo ambao naamini kabisa wanaogopa kufa kwa sababu ya kuwaacha wale wawapendao, wapo wanao-ogopa kifo kwa sababu hawajatubu dhambi zao ambazo wamekuwa wakitenda tangu waanze kujitambua, wapo wanao-ogopa kifo kwa sababu wanaogopa kuacha "raha za dunia" mfano si ajabu ukamsikia mtu akisema "naogopa kufa kwa sababu ya kuacha ulabu"--wewe muulize siku moja CHAOGGA au PASCAL swali la kwa nini "unaogopa kifo"--uone kama jibu halitakuwa "nina POMBE  nyingi sana kwenye fridge sijazimaliza kuzishusha". Na wengine si ajabu wakakujibu kuwa wanaogopa kifo kwa sababu ya "kuziacha raha za kitandani".

Zipo sababu nyingi sana ambazo kiukweli zinafanya watu kuogopa kifo. Je wewe unaogopa kifo, na kama ni ndio kwa nini unaogopa kifo? Na kama huogopi kifo ni kwa nini?

PamoJah

Views: 1302

Reply to This

Replies to This Discussion

Sina hofu ya kifo! We're all wonderful Divine creation of God!

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*