Tulonge

Wapendwa swali ni rahisi sana, kama ambavyo linauliza; mimi binafsi ukiniuliza swali hilo--jibu lake litakuwa ni kwamba "naogopa kufa kwa sababu sijatimiza ndoto yangu/zangu".

Ila nina imani wapo watu wanakuwa na hofu ya kifo kwa sababu tofauti tofauti. Wapo ambao naamini kabisa wanaogopa kufa kwa sababu ya kuwaacha wale wawapendao, wapo wanao-ogopa kifo kwa sababu hawajatubu dhambi zao ambazo wamekuwa wakitenda tangu waanze kujitambua, wapo wanao-ogopa kifo kwa sababu wanaogopa kuacha "raha za dunia" mfano si ajabu ukamsikia mtu akisema "naogopa kufa kwa sababu ya kuacha ulabu"--wewe muulize siku moja CHAOGGA au PASCAL swali la kwa nini "unaogopa kifo"--uone kama jibu halitakuwa "nina POMBE  nyingi sana kwenye fridge sijazimaliza kuzishusha". Na wengine si ajabu wakakujibu kuwa wanaogopa kifo kwa sababu ya "kuziacha raha za kitandani".

Zipo sababu nyingi sana ambazo kiukweli zinafanya watu kuogopa kifo. Je wewe unaogopa kifo, na kama ni ndio kwa nini unaogopa kifo? Na kama huogopi kifo ni kwa nini?

PamoJah

Views: 1302

Reply to This

Replies to This Discussion

Mimi naogopa nitakua kaburini peke yangu.Lile giza linatisha kweli

Aisee mimi sina hakika na usafi wangu wa kiroho.Nahisi graph yangu ya dhambi bado ipo juu.Huyo Malaika mtoa roho angoje ngoje kwanza nizipunguze

mimi naogopa kufa kwa ajili ya wanangu. ehe! mungu baba muweza wa yote hebu chelewesha kifo changu mpaka wanangu watakapoweza kujitegemea.

Duuh! Anangisye umenikumbusha sababu yangu nyingine. Sababu uliyoitoa huwa naiwaza pia

Mimi huwa sikumbuki kabisa mambo ya kufa.Hiyo ishu ya kufa inawahusu nyie tu.Niacheni mimi niishi milele kwa raha zangu

Siogopi kufa kwa sababu mwenye mali yake akiitaka, ana haki nayo. Mwache achukue.

 

Kifo kinatisha.. ila hakiepukiki.. Kila nafsi itaionja mauti.. Hakuna sababu ya kuogopa kufa kama Tukiwa wasafi mbele za Mungu. Sasa hapo kwenye kuwa wasafi ndiyo panatutisha!!!!

Kweli kifo hakiepukiki kama anavyosema DIXON,ila kwa kweli kinatisha! Mi nakiogopa kifo kwa sababu moja kuu; kwamba zile fujo zooote za duniani nitaziacha, yaani sitakuwa na nafasi ingine ya kuzifanya.

Halafu vilevile utamu wa juice za embe, nanasi etc....na vilevile kuwaacha washikaji zangu! Dah.....vilevile kumuacha nimpendaye anayenipa usingizi...........vilevile....mengine namezea............!

Ha ha ha ha ha ha ha ha! Unaogopa kubaki peke yako kaburini; we mkubwa bana usiogope giza. Wakubwa huwa wanaogopa mwanga, na sio giza!

Diana said:

Mimi naogopa nitakua kaburini peke yangu.Lile giza linatisha kweli

Wewe kibokoooo!

Severin said:

Mimi huwa sikumbuki kabisa mambo ya kufa.Hiyo ishu ya kufa inawahusu nyie tu.Niacheni mimi niishi milele kwa raha zangu

Kwa upande wangu ningetamani kumwacha mtoto wangu kwenye msing imara, pamoja na kujiwekea mimi mwenyewe mazingira salama ya maisha yangu ya milele huko niendako. Eeeee Mola wangu nisaidie kutimiza mipango yangu. Ameeeen

Ha ha ha ha ha! Wengine wanaogopa kifo kwa sababu ya giza kaburini, wengine wanaogopa kwa sababu ya dhambi ambazo bado hawajazitubu, wengine wanaogopa kufa kwa sababu watoto wao bado hawana msingi ambao wanataka wabaki nao. Sawa sawa!.

Reply to Discussion

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*