Tulonge

Na Vitus Ngiliule

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23, Nimezaliwa mkoani Dodoma. Katika familia yetu tumezaliwa watatu yani kaka yangu mkubwa ambaye ananiachia mimi, halafu anafuata mdogo wangu wa kike anayeitwa Magdalena. Tulikua tukiishi na mama Chang’ombe, kwa yeyote ambaye ni mwenyeji wa Dodoma hili eneo litakua si geni kwake . Kwa ujumla familia yetu ilikua ni ya hali ya chini sana upande wa kipato. Mama alikua akijishughulisha na uuzaji wa mbogamboga, japo haikua biashara nzuri sana kwake kutokana na ufinyu wa kipato chake. Mimi nilikua nikisoma darasa la tano, lakini kaka yangu mkubwa alikua kidato cha nne wakati huo. Yule mdogo wetu wa mwisho alikua darasa la kwanza. Hii ilikua ni mwaka 2002. Kuna wakati ulifika hali ikawa mbaya sana pale nyumbani, kiasi kwamba mama akakosa kabisa fedha za kumsomesha kaka yetu. Hivyo ilimbidi kaka akatishe masomo hata kabla ya kufanya mtihani wa kuhitimu. Niliumia sana moyoni mwangu lakini sikua na jinsi tena. Kaka aliamua kuondoka na kuelekea dar kwenda kutafuta maisha, lakini Mungu si Athumani mara baada ya kufika Dar alihangaika huku na kule na kufanikiwa kupata kazi ya kupanga mayai katika shirika moja la wazungu. Mshahara aliokua akiupata ulimwezesha kupanga chumba cha kukodi pamoja na kununua samani za ndani, hakuishia hapo aliweza pia kututumia na sisi fedha za kujikimu pale nyumbani.

Nilipoingia darasa la sita, niliongeza juhudi sana katika masomo yangu kwani nilijua tayari sasa nakwenda kuingia darasa la saba .Si hili tu hata hali ya uchumi pale nyumbani nayo pia ilichangia sana kuongeza kwangu bidii ili nije nimkomboe mama hapo baadae. Mbali na masomo nakumbuka nlikua na tabia moja ya kukaa na watu walionizidi umri, hasa mara baada ya kutoka shuleni. Siku moja ilikua majira ya saa moja jioni, nlitoka nyumbani na kuelekea ile sehemu walipokua wakipenda kukaa watu wazima. Nlifika na kuketi maeneo yale, kiufupi nlikua ni mdadisi sana hata wao walilitambua hilo. Katika maongezi yao kuna kitu kilinishtua kidogo, walikua wakizungumzia majini watu lakini kiukweli swala hili mimi halikuniingia akilini. Kwani sikuwahi kushuhudia kama kuna watu wa jinsi hii katika huu ulimwengu. Waliendelea kuzungumza na kusema ya kua majini wamegawanyika katika sehemu nyingi sana. Kuna wale ambao huwa wana umbo la binadamu kabisa na huwa ni vigumu sana kuwatambua, kwani hawana tofauti kabisa na binadamu. Wakati wakiendelea ghafla nlimsikia mama akiniita, niliitikia wito wa mama na kuelekea nyumbani, nlipofika mama alinifokea sana kwani hakuipenda ile tabia yangu ya kukaa na watu wazima. NIlimuomba mama msamaha juu ya hilo naye hakusita kunisamehe, niliacha ile tabia ya kusikiliza maongezi ya watu wazima lakini jambo la kushangaza ile mada niliyoisikia kutokana na majini watu iliendelea kunikaa akilini mwangu.

Siku zilizidi kwenda hatimaye nikafanikiwa kuingia darasa la saba, nilifurahi sana hata mama alilitambua hilo, shauku yangu ya kusoma ilizidi kuongezeka ukilinganisha na ile ya kipindi cha nyuma. Yale mateso aliyokua akiyapata mama kulingana na hali yetu ya uchumi pale nyumbani, yalinifanya niongeze bidii sana ili siku moja nije niwe msaada mkubwa sana katika familia yetu. Siku zilizidi kwenda hatimaye ule mtihani wa taifa ukakaribia.

Itaendelea jumatatu ijayo..

Views: 1083

Replies to This Discussion

Yawezekana hadithi hii ikawa nzuri,nini subiri party2

Futa subra Yusha, j3 ijayo itaendelea

I'm waiting for part 2 kwa hamu kubwa

Nami nasubiria

aaaah....kumbe ni hadithi???

RSS

© 2023   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*