Tulonge

Na Vitus Ngiliule

Nilijiuliza maswali mengi mno kichwani mwangu yasiyokuwa na majibu. Ile gari tuliyokuwemo iliingia moja kwa moja hadi ile sehemu ya kupaki magari kisha ikasimama mara yule dada akaniamuru nitelemke kwani ule mlango wa nyuma ulikuwa tayari umekwishajifungua. Niliitikia wito wake kwa kuchukua begi langu la nguo kisha nikatelemka. Mara tu baada ya kushuka nilijaribu kuangaza macho huku na kule nikilishangaa lile jumba la yule dada jinsi lilivyokuwa kubwa,lilikuwa ni jumba la ghorofa moja lililonakshiwa kwa rangi za aina mbalimbali zenye kuvutia pia niliona idadi kubwa sana ya magari ya kifari yaliyokuwamo pembezoni mwa jumba hili.

Wakati nikiwa bado nashangaa nisielewe nielekee wapi kwani wenyeji wangu walikuwa bado wamo ndani ya ile gari ghafla nilisikia sauti ya yule dada akiniamuru niongoze moja kwa moja kuelekea kwenye ule mlango wa kuingilia kwenye lile jumba. Niliitikia wito wake na kuanza kusogea taratibu kuelekea kwenye ule mlango  na nilipokaribia tu ghafla ulijifungua wenyewe kisha nikaingia moja kwa moja hadi ndani. Nilikuta sebule kubwa sana lililojaa samani za aina mbalimbali ambazo sikuwahi kuziona katika maisha yangu, hapo ndipo nilipoamini ya kuwa kuna watu wapo Tanzania lakini maisha wanayoishi ni kama vile wapo Ulaya.

Niliongoza moja kwa moja hadi kwenye sofa zilizokuwamo mle sebuleni kisha nikatupia begi langu la nguo juu ya zile sofa nami nikaketi kwa kujitupia kama vile gunia kwani nilikuwa nimechoka sana kutoka na ile safari. Mbele yangu kulikuwa na screen kubwa lililokuwa likionesha picha mfano wa television na watu waliokuwa wakionekana mle walikuwa ni kama vile wahindi, hivyo niliishia kuwatazama tu lakini sikuelewa chochote kilichokuwa kikiendelea kutokana na lugha waliyokuwa wakitumia. Wakati nikiwa bado nimetulia pale sebuleni nikiwatazama wale watu ghafla nilisikia sauti ya mwanamme na mwanamke kutokea kule nje ya lile jumba wakijibizana kwa sauti,ijapokuwa maneno sikuweza kuyasikia vizuri  ila nihisi ule ulikuwa ni ugomvi. Nilinyanyuka moja kwa moja na kwenda kwenye dirisha lenye kioo ili nifahamu nini kilikuwa kikiendelea.

Nilistaajabu sana baada ya kumuona dada Hidaya akigombana na yule dereva lakini wakati nikiwa bado nimesimama pale dirishani, ghafla wote walinyamaza kimya kana kwamba kuna kitu wameshtuka. Baada ya kuona hivyo niliondoka haraka na kurudi ile sehemu niliyokuwa nimeketi, lakini kuna kitu nilikisikia kutokana na  yale majibizano yao kwani walikuwa wakitaja sana neno pini. Hivyo nikajua moja kwa moja itakuwa ni ile pini niliyokuwa nayo mimi. Haikuchukuwa muda kwani mara tu baada ya kuketi nilisikia ule mlango  wa sebuleni ukifunguliwa kwa nguvu.


Itaendelea jumatatu ijayo...

Views: 544

Replies to This Discussion

Na baada ya mlango kufunga.. nikasikia .. Lete ile pini !!! Teheee nikacheka!!!!

Nitaendelea Wiki ijayo.....

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*