Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kumwaga lolote juu ya mdau wetu wa wiki kwa kuzingatia maadili mema.Kazi kwako mdau

Views: 759

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion


 Ahsante kaka Chibiriti kwa bahati nzuri pasaka  nilikuwa hapo Makalala nadhani unakipata hicho kijiji cha hapo jirani ndo anakaa mamaangu mzazi nimekaa kwa muda wa siku kama nne na napenda sana kufika hapo makalala kwa watoto yatima nilikuwa nikimwambia mama kuwa siku moja tufanye mazoezi anipeleke hapo nije nione hao watoto
BARAKA FRANCO CHIBIRITI said:

Asante sana kwa majibu yako, kumbe wewe ni mjomba wangu kabisa. Mimi napenda sana Iringa, nimekaa sana kijiji cha Migoli karibu na bwawa la Mtera kwa kazi mbalimbali, kila nijapo likizo lazima niende Iringa, Mafinga - makalala, huko kuna kituo cha watoto yatima ambapo mimi binafsi nakifuatilia kwa muda mrefu kwa ukaribu sana na kukipenda sana tena sana. kwakweli ni furaha sana moyoni mwangu kushirikiana kwa ukaribu na kituo hicho cha Makalala, sasa tuna watoto 38, ambao wanaendelea vizuri sana kwa kila huduma, karibu kila wiki napata taarifa kwa njia ya simu, pia mwanzilishi wa kituo hicho kwasasa yupo huku kwa likizo ya uzazi, tunaonana kila mara kubadilishana mawazo mbalimbali kuhusu Makalala Home Children. Karibu sana Makalala dada Agnes. Ujionee mwenyewe na utawapenda sana watoto, naamini.

Jinsi ulivyojibu maswali ya wadau wengi hapa, sina tena maswali zaidi ya kukuuliza...maana mengi walishanitangulia kukuuliza, ila nimependa majibu mengi ulivyojibu na kueleza vizuri, safi sana na hongera sana. Nakutakia kila laheri katika haya maisha. 

Agnes Nyakunga said:

nakujibu kaka Franco kama ifuatavyo:-

 

1) mimi ni mzaliwa wa Iringa, kabila langu mhehe

 

2) kitu nachokipenda sana katika maisha ni kubadilishana mawazo na watu mbalimbali wa rika lolote!

 

Ahsante kaka Franco nasubiri mawsali mengine kutoka kwako

BARAKA FRANCO CHIBIRITI said:

Haya sasa zamu yako dada; Na mimi nakutwanga maswali haya;

1). Wewe ni mzaliwa wa wapi? Kabila gani?

 

2). Kitu unacho kipenda sana katika haya maisha ni nini?

 

Ukinijibu haya nitakuuliza na mengine mengi tu mpaka uchoke.


Ahsante dada Belita

 

maswali yako yanachangamoto sana kwangu, na katika maswali niliyokuwa niki yasubiria ni kati ya haya ulioniuliza nafikiri mtizamo wako na wangu tukiufanyia kazi tutafika mbali

 

1. sawala la utoaji mimba, wakulaumiwa sana msichana mwanaume ni kiumbe ambaye ameumbwa tofauti na mwanamke hormone zao zinastimulate muda wote kwa hiyo anapokuja kwako wewe msichana kukutongaza na imani kabisa una akili na utashi wa kutoa jibu fasaha ambalo litakuepusha wewe katika njia hatarishi, unapofikia uamuzi wa kumkubali mvulana unajua nini kinafuata iweje unapata mimba halafu unaitoa? kinachotutofautisha ni maumbile tu wakati mwingine huyo mvulana ndo yuko katika harakati za kubarehe basi yeye muda huo anahangaika na msichana sasa na wewe ukiwa umelegea habari ndo inakuwa hiyo (wasichana kuweni makini) kuepusha utoaji mimba ovyo!

 

2. kwa kweli dada Belita cjawahi kutoa mimba nakuhakikishia

 

Ahsante kauli mbiu yangu (wasichana epukeni mazingira hatarishi)
Belita said:

Hongera dada Aggy kwa kuwa mdau wa wiki.

1. Unalichukuliaje suala la utoaji mimba?Nani wa kulaumiwa (mvulana au msichana)?

* Nina imani wewe ni mkristo wa kweli,endapo utadanganya kwenye jibu utakalo litoa ktk swali lifuatalo utakuwa unazidi kujiongezea mzigo wa dhambi zako.Ni bora usijibu kuliko kudanganya.

2. Umewahi kutoa mimba au hapana? Kama ulitoa, kwa nini uliamua kutoa?

Dah Dada Agnes nakupa nyota 1 kwa kujibu maswali ipaswavyo me umeshanimaliza yaani umejibu mipini ya maswali yakufa m2 bt mtt wakike full kujiamini safi sana nimependa sana  

 

jibu numbar 9 na 7 kiujumla  umejibu vzr maswali yote.

Hongera sana kuchaguliwa kuwa mdau wa wiki. Kumbe wewe ni mtani wangu. Mie huwa napita Iringa niendapo kwetu hivyo sitokuuliza maswali maana usije nizibia njia siku moja napopita na gari Iringa kuelekea nyumbani kwetu. Mungu akubariki

Hongera kwa kuchaguliwa kuwa mdau wa kijiji! Mimi nina swali moja tu kwani naona maswali mengi wameshauliza na nimefurahishwa na majibu!

Swali langu ni hili. 

Muhimbili unafanya kazi gani?

Nakutakia kila la heri katika maisha kwa ujumla!

Ahsante sana kaka Omary, kujiamini ni jambo la muhimu sana

 

kazi njema!

Omary said:

Dah Dada Agnes nakupa nyota 1 kwa kujibu maswali ipaswavyo me umeshanimaliza yaani umejibu mipini ya maswali yakufa m2 bt mtt wakike full kujiamini safi sana nimependa sana  

 

jibu numbar 9 na 7 kiujumla  umejibu vzr maswali yote.


Ahsante mama Malaika

 

Ucjali cwezi kukuzibia njia tena maana ushajihami, ubarikiwe sana!
Mama Malaika said:

Hongera sana kuchaguliwa kuwa mdau wa wiki. Kumbe wewe ni mtani wangu. Mie huwa napita Iringa niendapo kwetu hivyo sitokuuliza maswali maana usije nizibia njia siku moja napopita na gari Iringa kuelekea nyumbani kwetu. Mungu akubariki


Ahsante kaka Eddie

 

mie ni personal secretary niko upande wa chuo cha madaktari (MUHAS)
eddie said:

Hongera kwa kuchaguliwa kuwa mdau wa kijiji! Mimi nina swali moja tu kwani naona maswali mengi wameshauliza na nimefurahishwa na majibu!

Swali langu ni hili. 

Muhimbili unafanya kazi gani?

Nakutakia kila la heri katika maisha kwa ujumla!

Unadhani ni kwa nini wadau hawawatwangi maswali mamen wakiwa wadau wa wiki?

 

Tulonge unatakiwa siku moja uwe mdau wa wiki tukuue na maswali yapo lukuki.
Hhahaahaaaa Okoka najua sana kuwa nikiwa mdau wa wiki MTANIUA kwa maswali,ila usijali wala nn.Siku moja nitakuwa mdau wa wiki.

okoka jailo mgavilenzi said:
Tulonge unatakiwa siku moja uwe mdau wa wiki tukuue na maswali yapo lukuki.
Hongera sana dada Agnes kwa kujitahidi kupambana na maswali mazito toka kwa wadau.Nadhani kwa sasa tumemfahamu vizuri ndugu yetu Agnes zaidi ya hapo mwanzo.Endapo una cha zaidi juu yake unaweza kumfuata kwenye ukurasa wake,muda wake wa kuwa mdau wa wiki umeisha. Jiandae kumpokea mdau wa wiki katikati ya mwezi huu wa tano.Pamoja sana.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*