Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kutoa maoni juu ya Dixon,kazi kwako mdau.

Views: 795

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Asante sana Eddie.

 

Nasubiri Maswali yako kwa hamu kubwa! Siku njema.


eddie said:

Hongera Dixon kwa kuchaguliwa mdau wa wiki! Nakutakia heri na baraka katika shughuli zako za kila leo pamoja na family yako!

 Maswali yatafuata baadaye!

Unaonaje hali ya huko ? Mwenzio nimekuwahi..

 

Karibu kwenye kuchangia hapa!


Safari njema

Cha the Great said:

Dah, e bana nikirudi toka Loliondo nitachangia kidogo. Huku ni mshikemshike, nikichelewa, nahofu kukosa tiba kwa wakati.

 

Ila nitarudi.

Umeshiba sasa?

 

Lete maswali sasa.. hope hutaniumiza.. maana ?  lol


Mama Malaika said:

Dixon badi sijamaliza kula nitarudi baadae...

Hello ABD.. Natumaini upo sawa.!

                  1. Asante sana kwa pongezi zako!

                  2. Ule ukweli nilitahamaki nilipo ona nimekuwa mdau wa wiki.. Lakini kwa upande wa kuuza SURA                             hapo.. hahahaa.. Nimefurahi sana! Maana ni "shavu" lakutosha.. hahaa Big up TULONGE!!

                  3. Hii program ni nzuri sana, kwanza ni ubunifu wa hali ya juu sana. Naipongeza TEAM nzima ya TULONGE kwa hili, pili ni kwamba inatoa fursa ya kuwafahamu wadau wa tulonge kwa undani, kimaisha kwa ujumla, kupeana ushauri na kupeana burudani.

 

Naona Muhtasari wako umeanza kwa kasi kubwa, sijui habari kamili itakuwaje.. hahaa.. Natumaini nimekujibu! Asante.


ABD said:

1: hongera kwa kupata nafasi hii ya kuwa mdau wa wiki

2: Vipi wajisikia au ulichukilia vipi ulivyo ona unauza sura hapo home page?

3: Na vipi unaichukulia hii program ya  mdau waki?

 

Huo ulikuwa ni muhtasari wa  maswali na habari kamili itakuja in next few hours

Asante Omary kwa uwepo wako.. Kweli nipo fit kujibu swali lolote litakalojitokeza mbele yangu.. Sidhani kama nitafikia kuwa hoi.. hahaaa.. Nakukaribisha wewe kuwa mmoja wapo wa kuuliza maswali. Karibu.

Omary said:
Kaka hongera sana kwa kuwa hapa mbele ye2 2kuswalike, me ningewaomba wadau waku2nguwe maswali uanze kuyajibu hukohuko kwa Babu mpaka ukirudi uko hoi bin taabani kwa maswali jamani kama kwa Babu hakuna mtandao hata p.o.box? 2mswalike 2 kwa sanduku la baruwa p.o.box .... kwa Babu.

1.Hivi huyu mwanamke wa kizungu ni mkeo?

2.Mmefunga naye ndoa?

3.Kama bado,je unampango wa kufunga naye ndoa?

4.Kwa nini umeamua kuwa na mwanamke wa kizungu wakati weusi wenzio wapo?

5.Familia yako imekuchukuliaje kuwa na mwanamke wa kizungu?

Hongera sna best hivi una miaka mingapi???

Kakaangu me naomba nije kwenyewe swali 1 kwa 1

1 hivi kunywa pombe ni ujanjaau ushamba?

2 je inawezekana m2 kuacha pombe?

3 ili kubolesha kijiji chetu tunatakiwa kuongeza nn?

4 unawachukuliaje? watoto wa mitaani?

5 ww una watoto wangapi? na unawaleaje?

6 huna mtoto mitaani i mean umezaa na mwanamke au ulimuachia mimba halafu hujui alipo?

7 kama ww ungepewa rungu la Jakaya ungeli2miaje kuokowa hili janga la mfumuko wa bei?

8 unaishi mji gani? kwa hapa TZ nina swali lenye maana kuhusu unapoishi bt nitakuuliza utakaponijibu

unaishi wapi. kwa sasa nikutakie majibu mema yenye hekima na busara

9 nawashauri wana kijiji wapunguze ukari wa maneno kwenye maswali ye2.

 

Swali namba moja. Hivi umeshakuwa raia halisi wa Tanzania? Maana kuna habari au tetesi za kiintelejensia kuwa wewe unatokea kule Zimbabwe kwa Mugabe, na unaishi hapa illegally. Ukijibu hilo, utapata zawadi. Halafu mengine yatafuata.

PamoJah

Duh!!! Severin Naona umekuja kivingine kabisa! Kweli huu ndo utamu wa kuwa mdau wa wiki..


                        1. Kwanza huyu bado hajawa Mwanamke.. heheee.. Hatujapata mtoto bado! Huyu Msichana                                          ni MCHUMBA wangu,  Bado hatujawa mke na mume!

                       2.  Jibu la swali lako la kwanza pia linajibu hili la pili pia! Bado hatujafunga ndoa! Tupo kwenye kipindi cha uchumba!

                       3. Mpango wa kufunga ndoa UPO ndio maana tumekuwa wachumba hivi sasa.

                       4. Nimekuwa na mwanamke wa kizungu kwasababu.. Mapenzi hayachagui.. RANGI, DINI, KABILA WALA UTAIFA WA MTU.. Tumependana ndo maana niponae. Weusi wenzangu wapo, ila ni kwamba jicho langu limeona hapo!

                         5. Kuhusu familia yangu.. mwanzo tulipo kwenda nyumbani walihisi ni mapenzi ya "boyfriend na girlfriend".. hawakuipokea vizuri... ILA Walifurahi sana nilipo mpeleka nyumbani mara ya pila kwa baba na mama yangu kumtambulisha RASMI kama MCHUMBA.. kwani waliona sasa tumekuwa serious kwenye uhusiano wetu. Pili si kitu kigeni kwenye familia yangu.. Baadhi ya ndugu yangu pia wameoa na kuolewa nje!

 

Natumaini nimekujibu vizuri.. kama kuna mahali panaitaji ufafanuzi tafadhali usisite kuuliza!

      Severin said:

1.Hivi huyu mwanamke wa kizungu ni mkeo?

2.Mmefunga naye ndoa?

3.Kama bado,je unampango wa kufunga naye ndoa?

4.Kwa nini umeamua kuwa na mwanamke wa kizungu wakati weusi wenzio wapo?

5.Familia yako imekuchukuliaje kuwa na mwanamke wa kizungu?

 


Asante sana Mtemi..

  Mwezi wa kumi mwaka huu natarajia kufikisha miaka 30!

Mtemi said:

Hongera sna best hivi una miaka mingapi???

 

Kaka Cha!! Mimi ni Mtanzania halisi, Baba yangu.. Mr. Fidelis M. Kaishozi.. ni mzaliwa wa Bukoba pia Mama yangu kipenzi.. Mrs Grace K. Kaishozi ni mzaliwa wa bukoba pia! Kwahiyo mimi ni MUHAYA "pure" kutoka bukoba ingawa nilizaliwa mkoani Musoma wazazi wangu walipokuwa wanafanya kazi mkoani hapo wakati huo.

Natumaini nitapata hiyo zawadi kwa kujibu swali lako kirefu.. hahahaa

 

PamoJah

Cha the Great said:

Swali namba moja. Hivi umeshakuwa raia halisi wa Tanzania? Maana kuna habari au tetesi za kiintelejensia kuwa wewe unatokea kule Zimbabwe kwa Mugabe, na unaishi hapa illegally. Ukijibu hilo, utapata zawadi. Halafu mengine yatafuata.

PamoJah

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*