Tulonge

Huu ndiyo uwanja wa kutoa maoni juu ya Dixon,kazi kwako mdau.

Views: 798

Replies are closed for this discussion.

Replies to This Discussion

Nami najibu 1 kwa 1


1. Kunywa pombe sipendi kusema ni ujanja! Bali ni starehe ya mtu mwenyewe.. haimaanishi ukinywa pombe basi wewe ni mjanja au kutokunywa pombe wewe ni mshamba! Mimi kama mimi niliache hilo kwa mtu binafsi yeye mwenyewe ndiye atajibu kuwa ni ujanja ama laa.


2. Hakuna lisilowezekana chini ya jua.. ni maamuzi binafsi.. wapo waliokuwa wanakunywa pombe na wameacha. kwa maana hiyo inawezekana kuacha pombe.

 

3. Kuboresha kijiji nadhani wanakijiji tuwe karibu zaidi ya hapa tulipo.. nakiri mimi mwenyewe nimepotea kiasi flani kutokana na pilika pilika za hapa na pale.. kusafiri na shughuli nyingine.. natumaini si mimi tu mwenye pilika za kupambana na haya maisha. so Pindi tupatapo nafasi basi tujuliane hali na tupeane mawazo mbali mbali kama hivi mdau wa wiki inavyokuwa.

4. Watoto wa mitaani wanahitaji kusaidiwa. ingawa si wote wanakubali msaada. Tulishawai kumchukua kijana wa mtaani na kukaa nae, kumlipia shule ya ufundi stadi na mambo mengine.. lakini alikimbia na kutuacha! so wapo wanao hitaji msaada wa aina zote na wapo ambao hata ufanyeje kisha chagua maisha yake.

5. Nimebaahatika kupata mtoto 1 wa kiume.. "Kelvin". anasoma shule ya bweni "boarding school" namchukua kipidi cha likizo kama nipo TZ.. na huwa anakuwa pia kwa baba na mama yangu kwani mama yake aliolewa baada ya mimi kuchelewa kufunga nae ndoa wakati yeye alikuwa tayari anataka kuolewa. So sasa hivi namlea mwanangu as single parent!

6. Sina Mtoto mtaani. jibu la tano linatoa maelezo kwa hili.

 

7. Mimi siyo mwanasiasa na sipendi siasa.. kwani WOTE ni waongo. Nchi yetu imebarikiwa SANA.. Tuna Rasilimani nyingi kiasi kwamba siwezi kuzielezea hapa.. Ukichukulia Madini, Bahari, Maziwa, Mabonde na Mito, Mbuga za wanyama, Milima, Gesi, Aridhi ya rutuba na Rasilimali watu, Hali ya hewa, N.K.. kama hawa viongozi.. si JK pekeyake kwani yeye kama yeye pekeake hawezi. WANGEJITOLEA KUWATUMIKIA WATANZANIA KUTOKA MOYONI.. basi tungekuwa na maisha mazuri zaidi na zaidi ya haya, pia vitu kama mfumuko wa bei visinge pata nafasi kwani uchumi wa nchi ungekuwa JUU. tusizungumzie mfumuko wa bei tuu.. upo na uozo mwingine mwingi.

 

8. Ninaishi mkoa wa ARUSHA.

 

Asante sana bwana Omari kwa maswali yako MAZITO. Natumaini nimekujibu vizuri na kama unalo dukuduku la kitu hujakielewa usisite kuuliza. Karibu.

Omary said:

Kakaangu me naomba nije kwenyewe swali 1 kwa 1

1 hivi kunywa pombe ni ujanjaau ushamba?

2 je inawezekana m2 kuacha pombe?

3 ili kubolesha kijiji chetu tunatakiwa kuongeza nn?

4 unawachukuliaje? watoto wa mitaani?

5 ww una watoto wangapi? na unawaleaje?

6 huna mtoto mitaani i mean umezaa na mwanamke au ulimuachia mimba halafu hujui alipo?

7 kama ww ungepewa rungu la Jakaya ungeli2miaje kuokowa hili janga la mfumuko wa bei?

8 unaishi mji gani? kwa hapa TZ nina swali lenye maana kuhusu unapoishi bt nitakuuliza utakaponijibu

unaishi wapi. kwa sasa nikutakie majibu mema yenye hekima na busara

9 nawashauri wana kijiji wapunguze ukari wa maneno kwenye maswali ye2.

 

Dixon wewe mtoto wa mwisho nini?

Dixon una kaka na dada wangapi?

Nitajibu Maswali yako yote mawili kwa wakati mmoja!


Kwenye familia yetu.. Tupo watoto watano.. Wavulana wawili na wasichana warembo watatu..

Wakwanza ni Msichana.. Anaitwa Dada Joyce, Anafuata Kaka George, Alafu Dada Lilian, Tena Dada Dorice alafu mimi Kaka Dixon. Mimi ndiyo wa mwisho. Dada zangu wote waolewa tayari na Kaka yangu pia amekwisha oa pia! Mimi bado kidogo Mungu akinijaalia nitatangaza mchango.

Asante.

Mama Malaika said:

Dixon una kaka na dada wangapi?

Kaka Hongera kwa kwenda kupata Kikombe kwa Babu!
hahahaa..  Karibu!

Alfan Mlali said:
Kaka Hongera kwa kwenda kupata Kikombe kwa Babu!

Nimependa sana comment yako kuwa: Mapenzi hayachagui rangi, kabila, wala dini. Nimependa kwa sababu mimi imani yangu siku zote ni kuwa : Watu wote pasipokujali rangi, kabila, dini au hata utaifa ni wamoja. Na ndio maana pia napenda wimbo maarufu wa Hayati Lucky Dube "DIFFERENT COLOURS/ONE PEOPLE".

Nitafurahi sana siku nikiona wewe na shemeji yangu mtarajiwa toka Sweden, mkifunga pingu za Maisha, na labda niseme tu kuwa toka ndani ya moyo wangu, nakuombea kwa Mungu. PamoJah!
Dixon Kaishozi said:

Duh!!! Severin Naona umekuja kivingine kabisa! Kweli huu ndo utamu wa kuwa mdau wa wiki..


                        1. Kwanza huyu bado hajawa Mwanamke.. heheee.. Hatujapata mtoto bado! Huyu Msichana                                          ni MCHUMBA wangu,  Bado hatujawa mke na mume!

                       2.  Jibu la swali lako la kwanza pia linajibu hili la pili pia! Bado hatujafunga ndoa! Tupo kwenye kipindi cha uchumba!

                       3. Mpango wa kufunga ndoa UPO ndio maana tumekuwa wachumba hivi sasa.

                       4. Nimekuwa na mwanamke wa kizungu kwasababu.. Mapenzi hayachagui.. RANGI, DINI, KABILA WALA UTAIFA WA MTU.. Tumependana ndo maana niponae. Weusi wenzangu wapo, ila ni kwamba jicho langu limeona hapo!

                         5. Kuhusu familia yangu.. mwanzo tulipo kwenda nyumbani walihisi ni mapenzi ya "boyfriend na girlfriend".. hawakuipokea vizuri... ILA Walifurahi sana nilipo mpeleka nyumbani mara ya pila kwa baba na mama yangu kumtambulisha RASMI kama MCHUMBA.. kwani waliona sasa tumekuwa serious kwenye uhusiano wetu. Pili si kitu kigeni kwenye familia yangu.. Baadhi ya ndugu yangu pia wameoa na kuolewa nje!

 

Natumaini nimekujibu vizuri.. kama kuna mahali panaitaji ufafanuzi tafadhali usisite kuuliza!

      Severin said:

1.Hivi huyu mwanamke wa kizungu ni mkeo?

2.Mmefunga naye ndoa?

3.Kama bado,je unampango wa kufunga naye ndoa?

4.Kwa nini umeamua kuwa na mwanamke wa kizungu wakati weusi wenzio wapo?

5.Familia yako imekuchukuliaje kuwa na mwanamke wa kizungu?

Nawashukuru wote mlioshiriki katika kipengele hiki cha mdau wa wiki. Nadhani tumemfahamu Dixon vizuri zaidi ya hapo mwanzo. Jiandae kumpokea mdau wa wiki mwanzoni mwa mwezi wa April.

RSS

© 2021   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* \uascript type="text/javascript">\udinsert below header image\udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud \uascript type="text/javascript">\ud insert below header image \udif (typeof(x$) != 'undefined') {\ud var postHeaderImageAd = '\uadiv id="postHeaderImageAd ">\ua\ua/div>';\ud x$("#xg_masthead").after(postHeaderImageAd);\ud}\ud /*